Karibu tujifunze Biblia.
Tukio la Ibrahimu kukubali kumtoa mwanawe kuwa sadaka ya kuteketezwa lilikuwa ni jambo gumu na la kishujaa sana…Kiasi kwamba ilihitajika kuwa mtu mwingine ndipo moyo huo mtu uweze kuwa nao.
Hebu jiulize leo itokee ni wewe umeambiwa hivyo kwamba ukamtoe mwanao wa kwanza wa kiume kuwa sadaka ya kuteketezwa..Kumbuka kwa wakati ule sadaka ya kuteketezwa ilikuwa ni unamkamata mbuzi au kondoo unamchinja, kisha unamkata kata nyama zake vipande vipande, kisha unamweka juu ya madhabahu ambayo ilikuwa inatengenezwa kwa mawe na kuni..halafu unawasha moto na kuichoma ile nyama mpaka iteketee kabisa kuwa jivu…harufu inayotoka ni kama ya nyama choma..Sasa piga mahesabu ni mwanao ndio unamfanyia hivyo, unamshika unamchinja akiwa mzima, anakuuliza baba ni nini unataka kufanya…halafu ghafla unaona machozi yanaanza kumshuka mashavuni.. kisha unamkata vipande vipande bila huruma na kuweka vipande vile juu ya kuni..na kuwasha moto…na kuichoma nyama yake mpaka iteketee kabisa…huku unatazama huku unaisikia ile harufu ya nyama ya mwanao. Utakuwa katika hali gani?
Bila shaka ni jambo gumu…lakini kwa Ibrahimu lilikuwa ni rahisi…Kwanini lilikuwa ni rahisi? Leo tutajifunza siri iliyomfanya Ibrahimu iwe rahisi kwake kutaka kumchinja mwanawe..
Na siri hiyo tunaipata katika kitabu cha Waebrania..
Waebrania 11:17 “Kwa imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaka awe dhabihu; na yeye aliyezipokea hizo ahadi alikuwa akimtoa mwanawe, mzaliwa pekee; 18 naam, yeye aliyeambiwa, Katika Isaka uzao wako utaitwa, 19 AKIHESABU YA KUWA MUNGU AWEZA KUMFUFUA HATA KUTOKA KUZIMU; akampata tena toka huko kwa mfano”.
Waebrania 11:17 “Kwa imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaka awe dhabihu; na yeye aliyezipokea hizo ahadi alikuwa akimtoa mwanawe, mzaliwa pekee;
18 naam, yeye aliyeambiwa, Katika Isaka uzao wako utaitwa,
19 AKIHESABU YA KUWA MUNGU AWEZA KUMFUFUA HATA KUTOKA KUZIMU; akampata tena toka huko kwa mfano”.
Umeona hapo mstari wa 19?…Siri ndio ipo hapo…Kwamba Ibrahimu alihesabu kuwa hata baada ya kumchinja mwanawe na kuwa jivu…Mungu huyo huyo aliyempa mtoto kimiujiza jiza wakati umri wake ukiwa umeshakwenda sana…anaweza kufanya muujiza wa kumtoa mwanawe kule kuzimu alipokwenda, na kuligueza lile jivu lililochomwa juu ya zile kuni kurudi kuwa vile vipande vya nyama, kisha akavirudisha vile vipande vya nyama vilivyokatwa katwa na kuwa mtu kamili na kuirudisha ile damu iliyomwagika kuwa mtu tena na hata anauwezo wa kulifuta lile wazo kwa mwanawe kwamba alikuwa anakwenda kutolewa sadaka..na Mungu kumpa tena mwanawe akiwa mzima bila dhara lolote kama alivyokuwa mwanzo…
Kwa Imani hiyo ya kumwamini Mungu kuwa anaweza kufanya hayo…ndiyo iliyomfanya Ibrahimu asipate shida kumtoa mwanawe kuwa sadaka ya kuteketezwa….alijua hata kama mwanawe atateketea, ndani ya dakika tano Mungu anaweza kumrudisha tena akawa wake…kwahiyo akahesabu kumtii Mungu ni bora kuliko kusikiliza hisia zake..
Na siri hiyo hiyo ndiyo itakayotufanya na sisi tuweze kumtolea Mungu wetu vilivyo bora pasipo kuangalia hasara tutakazozipata…Tutaweza kumtolea Mungu vilivyo vikubwa ambavyo vinatugharimu tukifahamu kuwa japokuwa tumevipoteza vyote kwa ajili ya Mungu…lakini Mungu bado ana uwezo kuturudishia vile vitu kufumba na kufumbua kama vilivyo…
Sio hilo peke yake…pia tunapomwamini Kristo na kujitwika misalaba yetu na kumfuata ni sawa na tumeyatoa maisha yetu kuwa sadaka kwake…Maana yake ni kwamba tunaishi Maisha ya kujitoa kwa Kristo na kuzipoteza nafsi zetu kwa ajili yake na hata kuifia imani tukiamini kuwa japokuwa tumezipoteza nafsi zetu katika ulimwengu huu kwa ajili yake, lakini bado Mungu wetu anao uwezo wa kutufufua na kutufanya upya tena na kuturudishia uhai wetu na kutupa Maisha marefu na mazuri kuliko haya tuliyonayo hapa duniani…Lakini tusipoamini kwa namna hiyo, kamwe hatuwezi kuyatoa Maisha yetu kwa Kristo kikamilifu. Tutaanza kusema aah..kuna faida gani kumtumikia Mungu…kuna faida gani kuyatoa Maisha yangu kwake na kuishi kuzishika amri zake..
Biblia inasema..
Mathayo 16:24 “Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. 25 Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona. 26 Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?”
Mathayo 16:24 “Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.
25 Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.
26 Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?”
Bwana atubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
NI WAPI MAHALI SAHIHI PA KULIPA ZAKA?
Je! habari ya Yusufu, inabeba ujumbe gani kwa agano jipya?
YA KALE YAMEPITA, TAZAMA YAMEKUWA MAPYA
NI NINI TUNAJIFUNZA JUU YA MT. DENIS WA UFARANSA?
ESTA: Mlango wa 5, 6 & 7
MOJA YA HIZI SIKU TUTAONA MABADILIKO MAKUBWA SANA.
SIKU ILE NA SAA ILE.
Rudi Nyumbani:
Print this post