Uradhi wa Mapenzi yake ni nini? (Waefeso 1:5)

Uradhi wa Mapenzi yake ni nini? (Waefeso 1:5)

Jibu: Tureje..

Waefeso 1:5 “Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe WANAWE kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na URADHI WA MAPENZI YAKE”.

Maana rahisi ya “Uradhi wa Mapenzi” ni “Mapenzi ya Hiari”..

Mtu anayefanya kazi fulani kwa Hiari yake mwenyewe na kwa mapenzi yake yote bila kusukumwa, kulazimishwa wala kuhamasishwa mtu huyo ni sahihi kusema amefanya kazi ile kwa “Uradhi wa Mapenzi”.

Na Mungu ametupenda alituchagua sisi tuwe “Watoto wake”.. Kwa mapenzi yake ya Hiari.. na kwa furaha ya Moyo wake, Maana yake ni jambo linalompa raha na furaha sisi kuwa watoto wake, sio uamuzi wa majuto kwake..

1Yohana 3:1 “Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, KWAMBA TUITWE WANA WA MUNGU; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye”.

Kwahiyo ni bahati na upendo mkubwa sana MUNGU kutufanya sisi kuwa watoto wake, na Kuwa Mtoto wa Mungu maana yake ni lazima utabeba tabia za Uungu, na ndio maana wana wa MUNGU wanaitwa miungu..

Yohana 10:34 “Yesu akawajibu, Je! Haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, NDINYI MIUNGU?

35 Ikiwa ALIWAITA MIUNGU wale waliojiliwa na neno la Mungu; (na maandiko hayawezi kutanguka)”.

Ni hii ni kweli kabisa mwana ni lazima afanane na Baba, hata mtoto wa Mtu ni Mtu, mtoto wa kondoo ni kondoo, na mtoto wa simba ni simba..vivyo hiyo ni mtoto/watoto wa MUNGU ni miungu.

Je umefanyika mtoto wa MUNGU?.. Na je unaijua kanuni ya kufanyika kuwa mtoto wa MUNGU?.. Si nyingine zaidi ya ile tunayoisoma katika Yohana 1:12..

Yohana 1:12 “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake”

Mpokee leo YESU nawe utapata uwezo huu mkuu wa kuwa mwana wa Mungu na mrithi wa ahadi za MUNGU… kwasababu ni Uradhi wa mapenzi yake tuwe hivyo.

Waefeso 1:9 “akiisha kutujulisha siri ya mapenzi yake, sawasawa na uradhi wake, alioukusudia katika yeye huyo”.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

nini maana ya haya maneno aliyosema Bwana ; Tuliwapiga filimbi wala hamkucheza; Tuliomboleza wala hamkulia?

JE! UMEFIKIA VIGEZO VYA KUWA BABA ROHONI?

Siku ya kujiliwa inayozungumziwa katika  1Petro 1:12, ni ipi?

HEKIMA YA KIMUNGU, INAINGIAJE MIOYONI MWETU?

NIFANYE NINI ILI NIPENDWE NA MUNGU?

Print this post

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply