nini maana ya haya maneno aliyosema Bwana ; Tuliwapiga filimbi wala hamkucheza; Tuliomboleza wala hamkulia?

nini maana ya haya maneno aliyosema Bwana ; Tuliwapiga filimbi wala hamkucheza; Tuliomboleza wala hamkulia?

SWALI 1:Bwana Yesu aliposema huu mfano alikuwa anamaanisha nini?..

“Lakini nitakifananisha na nini kizazi hiki? Kimefanana na WATOTO wanaokaa SOKONI,WANAOWAITA wenzao,wasisema,Tuliwapigia FILIMBI,wala hamkucheza; TULIOMBOLEZA,wala hamkulia.MAANA YOHANA ALIKUJA,HALI WALA HANYWI,WAKASEMA,YUNA PEPO.MWANA WA ADAMU ALIKUJA,AKILA NA KUNYWA,WAKASEMA,MLAFI HUYU,NA MLEVI,RAFIKI YAO WATOZA USHURU NA WENYE DHAMBI!” NA HEKIMA IMEJULIKANA KUWA INA HAKI KWA KAZI ZAKE”.(Mathayo11:16-19).


 JIBU: Mfano huo ni sawa ni kizazi cha sasa hivi tulichopo tuchukulie tu mfano, Mtu akitokea ni mtumishi wa Mungu kweli, maisha yake yote ameyachagua ni kukaa tu kanisani, au milimani kuomba, hafanyi kazi yoyote isipokuwa ni kuomba tu, na kuhudumu kanisani, hana pesa nyingi, nguo zake sio mpya sana, hana mke, wala marafiki, yeye kazi yake ni kumtumikia tu Mungu basi, kajikana maisha yake yote hataki chochote isipokuwa Mungu kajizuia kila kitu kwa ajili ya ufalme wa mbinguni ..Unadhani watu huku nyuma watamchukuliaje mtu kama huyo??..Si ajabu watamwita mlokole masalia, au kalogwa, watasema Mungu hayupo hivyo, Mungu anataka watumishi wake wawe na maisha ya kujifurahisha, kama vile Sulemani, na sio kuwa kama vichaa wa barabarani wasiokuwa na malengo..watamwambia hakika wewe utakuwa umeingiliwa na roho nyingine ambayo si ya Mungu….hivyo hatutaweza kukusikiliza mtu kama wewe maskini wa roho na kimawazo…sisi tunawasikiliza wahubiri wenye malengo, na mafanikio.

 Lakini watu hao hao, mfano wakimuona mtumishi wa Mungu kweli labda Mungu kampaka mafuta anahubiri Neno na Mungu katika kweli yote, kambariki na maisha mazuri ya duniani, labda kampa nyumba nzuri, nguo nzuri, kampa familia nzuri, kampa mali nyingi, analo kanisa kubwa, ..utashangaa watasema, watumishi wa Mungu huwa hawapo hivyo, watumishi wa Mungu hawawezi wakawa matajiri, huwa wanakaa tu milimani wanautafuta uso wa Mungu usiku na mchana, na sio kwenye majumba ya kifahari kama watu wa mataifa…..Kwahiyo kwao pia watasema hatuwezi kuwasikiliza nyie matapeli mnakula Fedha za waumini..

 Na ndivyo ilivyokuwa katika mfano huo, Mungu alipojaribu kuwapeleka Israeli nabii aliyejikana kwa kila jambo, (Yohana mbatizaji) wakasema mtu wa kawaida hawezi kuishi maisha kama hayo ya kutokula wala kujichanganya na wengine, ni lazima atakuwa anao pepo, Lakini Bwana alipokuja anakula na kunywa pengine akidhani kuwa labda watamsikia na yeye wakamwambia ni mlafi na mlevi, manabii wa Mungu hawawi hivyo…….Ndio mithali hiyo inakuja, walipopigiwa filimbi ili wacheze wakakataa, pengine wanahitaji maombolezo, lakini pia walipoombolezewa hawakulia,..sasa waelewekeje! Kwenye raha hawapo kwenye huzuni hawapo..Na ndivyo ilivyo katika kizazi hiki..hata kipewe ishara gani ya nabii hakitaamini isipokuwa wale tu waliokusudiwa tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu ndio watakaoamini ..

Ubarikiwe!


Mada zinazoendana:

BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA HAKUNA MTU ASHONAYE KIRAKA CHA NGUO MPYA KATIKA VAZI KUKUU?

WATU WASIOJIZUIA.

TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI:

SHETANI ANATOLEA WAPI FEDHA, ANGALI TUNAJUA FEDHA NA DHAHABU NI MALI YA BWANA?

HUYU AZAZELI NI NANI TUNAYEMSOMA KATIKA(WALAWI 16:8)


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Jacob Makono
Jacob Makono
3 years ago

Nazidi kubarikiwa sanasana na masomo yenu.Nimeanza kusoma saa 10 usiku..sasa ndio naona niishie hapa kwa Leo.Masomo yote yamenigusa,yamenionya,yamenijenga..natamani kwenda mbinguni kwa Mungu…lkn kuna kazi ya kudanya hapa duniani kwanza!!May God bless you richly!! Je, kuna no yenu ya simu kila mwezi niwatumie 5000(elfu tano?)Nitumieni no hiyo!