Usingizi, unapopita kiasi, huletea hasara, na umaskini, biblia imeliweka wazi hilo (Mithali 6:9-11), na sio usingizi tu, bali mambo yote yanayoonekana mazuri kama vile chakula, tendo la ndoa kwa wanandoa, yakikosa kiasi huleta uharibifu, Lakini usingizi kama usingizi, sio jambo baya, endapo tutaliona kiroho.
Mungu alipomleta Mwanamke duniani, alitumia njia ya usingizi, kama kanuni ya kumtoa kwa mwanamume, ingewezekana kabisa Mungu kumchukua Adamu kwenye maono kama alivyomchukua Yohana kule Patmo, kisha amuumbe Hawa kwa njia hiyo, au angemwacha macho, ashuhudie kazi yote ya upasuaji inavyofanyika, lakini hilo hakulichagua bali alitumia usingizi.
Robo ya maisha yako, unakuwa usingizini, hivyo huo muda, sio kwamba hakuna chochote kinachoendelea, au muda wako unapotea kama wengi wanavyodhani.
Watafiti wa kisayansi wanasema mtu anapokea taarifa katika ubongo, anapokuwa macho, lakini pale anapolala, taarifa zile ndipo zinapokusanywa, na kuhifadhiwa. Sasa huo ni utafiti wao, ambao tunajua kwa sehemu una uhalisia, lakini sisi wa rohoni tunaona zaidi ya mwilini.
Usipojua kuuandaa usingizi wako vema, basi unaweza kuzuia kazi za Mungu kutimilika vizuri tulalapo, kama tu vile tunavyoweza kuzuika kazi za Mungu anazotenda ndani yetu wakati wa mchana, tusipofuata kanuni zake.
Ukiona mara nyingi usingizi wako unavurugika, hulali, wakati mwingi unataabika usiku, unaota tu ndoto mbaya kila siku, magonjwa ya usiku yasiyokoma, fahamu kuwa pia hali yako ya kiroho inadhoofika.
Ni nini Mungu hufanya usiku?
Ili mojawapo ya huduma hizi, au zote, zitimie ndani yetu, basi jifunze kufanya yafuatayo.
Siku zote omba, kabla ya kulala, Kwa kufuata mpangilio huu.
Sema, Bwana Yesu, yote uliyonifundisha kutwa nzima ninaomba usiku wa leo, yazamishe kwenye vyumba vya ndani vya moyo wangu, nisiyasahau.
Bwana Yesu lile agizo kuu, ulilosema nami kutwa nzima, au siku zangu za nyuma, lithibitishe tena kwa kupitia njozi zangu.
Bwana Yesu nijuze yote kuhusiana na mambo ya kesho na yale yanayokuja mbeleni kupitia njozi zangu.
Bwana ninakwenda kinyume ni mashambulizi yote ya usiku yatokayo kwa yule mwovu, ndoto za kipepo, magonjwa, na madhaifu ninavifuta kwa jina la Yesu Kristo. Amen
Sikuzote ona usiku wako, ni sehemu ya huduma. Jipe muda wa kupumzika, huku umeuandaa kwa maombi mazuri.
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ