Je mtu anaweza kuwa “roho moja na Mungu”?.. jibu ni ndio!.
1Wakorintho 6:17 “Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye”.
Sasa ni kwa namna gani mtu anakuwa roho moja na Mungu?..
Jibu: Ni kwa namna ile ile ambavyo mtu anaweza kuwa mwili mmoja na mwenzake..
Marko 10:7 “Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; 8 NA HAO WAWILI WATAKUWA MWILI MMOJA; HATA WAMEKUWA SI WAWILI TENA, BALI MWILI MMOJA”.
Marko 10:7 “Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe;
8 NA HAO WAWILI WATAKUWA MWILI MMOJA; HATA WAMEKUWA SI WAWILI TENA, BALI MWILI MMOJA”.
Kama mwanaume na mwanamke wanavyokuwa mwili mmoja baada ya ndoa, nasi tunakuwa roho moja na MUNGU baada ya kuokoka kikweli kweli.
Kwanini hatuwi mwili mmoja na MUNGU na badala yake tunakuwa Roho moja naye?..
Ni kwasababu MUNGU ni ROHO (soma Yohana 4:24), na kwakuwa nasi( wanadamu) pia tunazo roho basi tunapomgeukia MUNGU tunaunganishwa naye na kuwa roho moja naye.
Na tunapokuwa roho moja naye maana yake sisi na yeye tunafanana?.. na mfanano wa kwanza ni “usafi na utakatifu”.. Kama Mungu alivyo mtakatifu nasi tutakuwa watakatifu kama yeye.
Mambo ya Walawi 20:26 “Nanyi mtakuwa watakatifu kwangu mimi; kwa kuwa mimi Bwana ni mtakatifu nami nimewatenga ninyi na mataifa, ili kwamba mwe wangu”.
Ukiona bado uasherati upo ndani yako basi ni dhahiri kuwa bado haujaungwa na Bwana, ukiona wizi upo ndani yako basi ni dhahiri kuwa bado haujaungwa na Bwana kwasababu MUNGU sio mwizi..na ukiona mambo yote yaliyotajwa katika kitabu cha Wagalatia 5:19-20 bado yapo ndani yako maana yake bado haujaungwa na Bwana.
Pia aliyeungwa na Bwana atafikiri daima habari za kuwavuta watu kwa MUNGU (yaani injili), kwasababu MUNGU naye anasikitishwa na maovu na anataka watu wote watubu, kadhalika na mtu aliyeungwa naye atakuwa na maazimio hayo hayo, kila siku atafikiri jinsi ya kuwavuta watu waiamini injili aidha kwa kuhubiri (mitaani, makanisani, mashuleni, masokono, mitandaoni au mahali pengine popote), au kama hatasimama basi ataiwezesha injili kwa mali zake kwa kadiri awezavyo, akijua kwamba hata kama hatasimama kuhubiri basi kawezesha injili kwa mali zake.
Lakini kama bado ndani yako huoni kiu wala hamasa ya kuhubiri/ kushuhudia watu waokoke au kuishika injili kwa mali zako, basi ni wazi kuwa bado haujaungwa na BWANA, kwasababu Neno la MUNGU linasema kuwa yule Roho wa MUNGU pamoja na Bibi arusi (yaani mtu aliyeokoka), kwa pamoja wanasema Njoo!.. yaani njoo upokee msamaha wa dhambi kwa kutubu na kuacha njia mbaya..
Ufunuo 22:17 “Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure”.
Je kwa maandiko haya, unajiona kwamba umeungwa na MUNGU, au umeungwa na vitu vingine?
Kama unajiona kwamba umeungwa na vitu vingine na si MUNGU, habari njema ni kwamba unayo nafasi ya kujitenga na muunganiko huo haramu, na kujiunganisha na MUNGU, kwa njia ya kutubu kwa kumaanisha kabisa kuacha dhambi, na kubatizwa kwa maji mengi kwa jina la BWANA YESU KRISTO na kwa ROHO MTAKATIFU, na kuanzia hapo na kuendelea utukufu wa MUNGU utakushukia.
Bwana YESU Akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
AMBATANA NA WALIO HAI ROHONI.
MISTARI YA KUOMBEA AMANI YA FAMILIA.
PONGEZI NA MAONYO YA BWANA KWA WATAKATIFU.
IMEANDIKWA NINI KATIKA TORATI? WASOMAJE?
HAPANA HATA MMOJA ATAKAYEIONJA KARAMU YANGU.
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ