Jina la Bwana YESU libarikiwe, karibu katika kujifunza Neno pamoja na Maombi.
Utangulizi: Kusoma Neno bila Kuomba, au kuomba bila Neno la kusimama nalo ni sawa na kitamba cha bendera kisicho na mlingoti, kitapelekwa huku na kule na kupotea…
Kupitia mfululizo huu na tafakari hizi tutapata mwongozo sahihi wa kuomba kwa kusimama na maandiko matakatifu ya Biblia.
Yuda 1:2 “MWONGEZEWE REHEMA na AMANI na UPENDANO”.
Mambo haya matatu ni muhimu kuwa nayo kama watu tuliokokoka
1. OMBI LA REHEMA (Tumia dk 45):
Rehema kwa tafsiri rahisi ni kibali ambacho mtu anaweza kukipokea kutoka kwa MUNGU au kwa Mtu mwenzake, ambacho kinazaa Msamaha, ufadhili, huruma, au msaada.
Kwamfano Mtu aliyerehemiwa na MUNGU, anakuwa amesamehewa makosa yake, au kupewa kibali na Baraka..
Zaburi 78:8 “Lakini Yeye, KWA KUWA ANAYO REHEMA, Husamehe uovu wala haangamizi. Mara nyingi huipishia mbali ghadhabu yake, Wala haiwashi hasira yake yote”.
Na rehema za MUNGU ni mpya kila siku.. na zilikuwepo tangu zamani (Zab. 25:6) na zitaendelea milele..
Maombolezo 3:22 “Ni huruma za Bwana kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi. Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu”
Kwahiyo chukua nafasi hii kuomba REHEMA za MUNGU ziongezeke juu yako, kwani utazipokea ikiwa utaomba kwa kumaanisha na kwa imani..
Kutoka 20:6 “nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu”.
Waebrania 4:16 “Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji”
Lakini pia tunaweza kuwa watu wa Rehema kwa wanadamu wenzetu.
Kama MUNGU anavyoturehemu tunapomwomba, ni lazima na sisi tuwe watu wa kurehemu wengine,
Mathayo 8:32 “Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi; 33 nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe?”.
Mathayo 8:32 “Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi;
33 nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe?”.
Faida ya kuwa watu wa rehema kwa wenzetu, ni sisi pia kurehemiwa na MUNGU..
Kwahiyo chukua nafasi hii kuomba MUNGU akakuongezee Rehema ndani yako kwa wengine.
2. OMBI LA AMANI. (Tumia dk. 45)
Ipo amani ya MUNGU na amani ya ulimwengu.
Yohana 14:27 “Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga”.
Maandiko yanasema pasipo upendo sisi sio kitu, katika Sehemu ya pili ya darasa letu hili la Neno na Maombi tulijifunza mwongo sahihi wa kuombea Upendo..Kwahiyo fungua link ifuatayo kupata mwongozo huo.
NENO NA MAOMBI~ Sehemu ya 2 (AMRI YA UPENDO)
Usikose sehemu ya tano (05) ya darasa letu hili la Neno na Maombi.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
NENO NA MAOMBI~ Sehemu ya 1 (MAPENZI YA MUNGU)
NENO NA MAOMBI~ Sehemu ya 3 (UTAKASO WA KINYWA)
FAIDA ZA MAOMBI YA USIKU
MWONGOZO WA MAOMBI YA ASUBUHI.
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ