Jina kuu la Bwana wetu Yesu Kristo
libarikiwe. karibu tujifunze Neno la Mungu ambalo ndio taa iongozayo
njia zetu. Biblia inasema “Mjue sana Mungu ili uwe na Amani (Ayubu 22:21)”..Siku zote ukijua sababu ya jambo Fulani basi unapata amani. Amani inakuja baada ya kujua sababu ya jambo Fulani.
Leo
tutajifunza juu ya vyanzo vya matatizo, na namna ya kuyatatua. Kama
tunavyojua wengi wetu vyanzo vya matatizo mengi ni shetani..huo ni
ukweli usiopingika. Lakini je! Shetani analetaje matatizo?.
Tukijifunza Mfano wa Ayubu, tunaweza
kupata majibu baadhi, tunaona shetani alimshambulia Ayubu baada ya
kupata kibali maalumu kutoka kwa Mungu, hiyo ikifunua kwamba shetani
hawezi kumgusa mtu yeyote wa Mungu pasipo ruhusa yeyote kwa Mungu..
Hivyo
Mungu anaporuhusu mtu ajaribiwe…anachokifanya ni kutoa ulinzi wake juu
ya Yule mtu, na akishatoa ulinzi wake maana yake shetani anapata nafasi
ya kumwingia. Hivyo anamshambulia.
Na shetani huwa ana njia kuu mbili za kuwashambulia watu.
1) Anatumia mapepo…Katika njia hii mtu atajikuta tu ameingia matatizoni pasipo kujua chanzo ni nini. Kumbe ni majeshi ya mapepo wabaya yamemvamia.
2) Na njia ya pili anatumia watu..(Na
watu atakaowatumia ni aidha watumishi wake wa uongo wanaovaa mavazi ya
kondoo lakini ndani ni mbwa-mwitu wakali…au atatumia wachawi na
waganga)….atatumia watumishi wa uongo kuwajaribu wale wanaomjua Mungu,
na atatumia wachawi na waganga kuwajaribu wale wasiomjua Mungu…au wakati
mwingine atatumia vyote viwili kuwajaribu wale watu wanaomjua Mungu.
Sasa
tukirudi kwenye mfano wa Ayubu..baada ya ulinzi wa kiMungu kuondoka juu
yake…shetani alimletea majaribu wengi… Kama haikuwa ni kazi ya mapepo
moja kwa moja basi kuna uwezekano mkubwa sana shetani alitumia watu
Fulani kumfanyia Ayubu yale mambo…Alichofanya shetani baada ya kuona
ukingo wa kiMungu umeondoka juu ya Ayubu ni pengine aliwatupia roho ya
wivu watu baadhi waliokuwa wanamzunguka…na ile roho ilipowaingia
pengine ikawasukuma kumwendea hata kwa waganga… labda walikwenda kwa
mganga fulani maarufu kwa kipindi hicho mwenye nguvu, wakaenda na picha
yake na za watoto wake..na nyayo zake labda..Na wakiwa kule wakaona
wanafanikiwa kumwona kwenye kioo chao cha kichawi, na pengine huyo
mganga akafanya mambo yake na kutuma kimbunga cha kichawi juu ya watoto
wake wakiwa karamuni, na kwasababu ulinzi wa kiMungu umeondoka juu ya
Ayubu jambo lile likafanikiwa na Kuwaua watoto wake wote. Na magonjwa ni
hivyo hivyo ni kikundi Fulani cha maadui zake Ayubu kilihusika kumletea
yale magonjwa.
Sasa
labda baada ya tukio hilo pengine Ayubu aliona tabia Fulani za watu
wanaomzunguka kufurahi..na pengine walisema vimaneno Fulani kuonyesha
kuwa wao ndio walifanya vile. Sasa kwa jicho la haraka haraka kama Ayubu
angekuwa sio mtu wa rohoni…angesema maadui zake wamemfanyia
visa..Lakini Bwana alimpa jicho la Mbali kujua mwanzo wa Matatizo yake
hayakuwa ni wale watu..bali alijua yalikuwa ni Mungu mwenyewe…kutoa
ulinzi juu yake. Ndio maana aliishia kusema “Bwana alitoa na Bwana
alitwaa, jina lake libarikiwe”…Alijua maisha yake ni makamilifu
isipokuwa ni Mungu tu katoa ulinzi juu yake kwa makusudi Fulani. Angalia
jinsi alivyouamini uhusiano wake na Mungu, kiasi cha kwamba hakuweza
kuyumbishwa ni kitu chochote, na sisi je! tunaweza tukawa hivyo?.
Na
mambo hayo hayo yanaendelea leo hii, watu wanatumiwa na shetani
kukuharibu, pengine ni wachawi au waganga…na kushindwa kuelewa chanzo
cha mambo yote ni nini?…chanzo cha mambo yote sio watu kukuonea wivu,
au wachawi kukuchukia hapana!..chanzo cha matatizo yote ni Ulinzi wa
kiMungu kuondoka juu yako..Usianze kupambana na watu wanaokuchukia, anza
kutafuta mzizi wa tatizo ni wapi..kama Ayubu.
Ayubu
alijua chanzo cha matatizo yake, kuwa ni Bwana ndiye kayaruhusu hayo
lakini njia zake ni kamilifu…alijua sio dhambi ndani yake iliyosababisha
ulinzi wa kiMungu uondoke juu yake.
Kadhalika
na sasa tunapaswa tujitathmini, kama kuna jambo Fulani limetokea ambalo
halipo sawa…chanzo chake ni nini?..Je! ni kama Ayubu? (Njia zetu ni
kamilifu isipokuwa ni Bwana anatujaribu tu) au ni kwasababu ya dhambi
zetu, kwasababu kitu pekee kinachotoa ulinzi wa kiMungu juu ya mtu ni
dhambi…
Ukiwa
mwasherati magonjwa yatakusumbua na wachawi watakusumbua sana, mapepo
yatakusumbua sana hakuna namna utaweza kuwashinda, hata uombewe kiasi
gani hakuna namna utaweza kuchomoka mikononi mwao…ukiwa mtazamaji wa
pornography na mfanyaji wa masturbation ni hivyo hivyo…ukiwa ni mzinzi,
ni shoga ni msagaji ni hivyo hivyo, watakusumbua na hakuna namna utaweza
kuwashinda…Usidanganywe kuwa kuna mchungaji yeyote duniani mwenye uwezo
wa kukuombea wachawi au mapepo yasikufikie wala kukudhuru, wala
usidanganyike kuwa kuna maji yoyote au mafuta yoyote ya upako
yanayowazuia wachawi wasiweze kufika nyumbani kwako…Usidanganyike
kabisa ndugu…
Kitu pekee kinachoweza kufukuza na kuzishinda nguvu za giza juu ya maisha yako ni MAISHA YA UTAKATIFU katika
Kristo Yesu, Uhusiano wako na Mungu ni wa kiwango gani, hicho tu! Wala
hakuna kingine….Maisha unayoishi ndio yanayoamua ulinzi wa kiMungu uwe
juu yako au uondoke.
Fanya
uamuzi sahihi leo, usitazame wachawi, wala waganga, kama ndio chanzo
cha matatizo yako…wala usiende kutafuta suluhisho kwa kuombewa, wala
kupakwa mafuta..Suluhisho lipo kwako ambalo ndio chanzo cha mambo
yote…suluhisho ni KUBADILIKA na kuishi maisha ya utakatifu, ambayo hayo
yanakuja kwa kutubu kwanza dhambi zako zote, na kudhamiria kuziacha
kabisa kuanzia sasa na kuendelea na kwenda kubatizwa na kisha kupokea
Kipawa cha Roho Mtakatifu ambaye atakusaidia kushinda dhambi.
Ukifanya
hivyo, ulinzi wa kiMungu utakuwa juu yako, haihitaji wewe kwenda
kuombewa wala kupakwa mafuta, wala kuwaogopa wachawi…Utaishi kwa Amani
sana, na wala hakuna chochote kitakachokugusa. Kwasababu nguvu iliyopo
ndani yako ni kubwa kuliko ya kwao..Bwana Yesu alisema..
Luka 6.17 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio;…… watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa;…”
Bwana akubariki sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
JINSI WATU WANAVYOZAMA KATIKA USHIRIKINA NA UCHAWI.
HUDUMA YA (ELIFAZI, BILDADI, NA SOFARI).
JE! MUNGU ANASABABISHA AJALI?
Rudi Nyumbani
Print this post