Bwana Yesu asifiwe. Karibu tujifunze neno la Mungu.
Paulo ni kielelezo kikubwa sana, kwa watu walio katika dhambi leo hii, ukiyatazama maisha Paulo, utajifunza mengi sana, Yeye mwenyewe anasema hapo zamani alikuwa ni mtukanaji, akiwa na maana alikuwa mtu asiyekuwa na maadili katika jamii, anasema tena alikuwa ni jeuri, kuonyesha kuwa alikuwa ni mtu mwenye kiburi kilichoshindikana,
Lakini ni heri angekuwa tu na tabia hizo ambazo ni za kawaida kuonekana kwa mwenye dhambi yeyote, kibaya zaidi alikuwa ni “mpinga-Kristo”, ile roho ya mpinga kristo ilikuwa tayari imeshamvaa, roho ya asi, mwana wa uharibifu, na kama tunavyojua kilele cha juu kabisa cha uasi wa dhambi ni kuwa adui wa Kristo, kama vile shetani alivyo, yaani kuwa mpinga-Kristo. Na ndio hatua ambayo mtume Paulo alikuwa ameshaifikia.
Yeye ndio alikuwa anaasisi mauaji yote ya watakatifu waliokuwa Yerusalemu kwa wakati ule, hata kifo cha Stefano yeye ndiye aliyetekeleza tukio lile zima, alikuwa ni katili wala alikuwa hana huruma na mtu yeyote aliyeitwa mkristo, Hiyo ikapelekea mpaka habari zake zikavuma kwenye makanisa yote ya wakristo, kiasi kwamba ilikuwa wakisikia tu Paulo yupo sehemu fulani, waliondoka na kwenda kujificha sehemu nyingine.
Hilo peke yake halikumtosha alianza kutanua mpaka na mipaka, akawa anaomba barua ili aende miji ya kando kando kwenda kuwakamata hao wayahudi wanaojifanya wanamwabudu Yesu, na kuwafunga. Hivyo kwa wakati ule alifanyika chombo kiteule cha ibilisi kupambana na uzao wa Mungu duniani. Unaweza tengeneza picha alikuwa ni mtu wa namna gani huyu. Huyu Unayemsoma kwenye nyaraka sio Yule Sauli wa zamani.
Lakini neema ya wokovu ilipomjia MARA MOJA TU. Na kutii, alipokea badiliko la ajabu sana. Badiliko ambalo lilimfanya awe Paulo na sio Sauli tena. Na kwa jinsi alivyoithamini ile neema, ndivyo Mungu alivyozidi kumwongezea neema juu ya neema mpaka, akawa zaidi hata ya wale mitume wengine ambao walionekana kama ni nguzo katika kanisa ambao mitume ambao walitembea na Yesu mwenyewe duniani.
1Timotheo 1:12 “Nami namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu, aliyenitia nguvu kwa sababu ALINIONA KUWA MWAMINIFU, akaniweka katika utumishi wake; 13 ingawa hapo kwanza nalikuwa MTUKANAJI, MWENYE KUUDHI WATU, MWENYE JEURI, lakini nalipata rehema kwa kuwa nalitenda hivyo kwa ujinga, na kwa kutokuwa na imani. 14 Na neema ya Bwana wetu ilizidi sana, pamoja na imani na pendo lililo katika Kristo Yesu. 15 Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi. 16 Lakini kwa ajili hii nalipata rehema, ili katika mimi wa kwanza, Yesu Kristo audhihirishe uvumilivu wake wote; NIWE KIELELEZO KWA WALE WATAKAOMWAMINI BAADAYE, wapate uzima wa milele. 17 Sasa kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu peke yake, na iwe heshima na utukufu milele na milele. Amina”.
1Timotheo 1:12 “Nami namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu, aliyenitia nguvu kwa sababu ALINIONA KUWA MWAMINIFU, akaniweka katika utumishi wake;
13 ingawa hapo kwanza nalikuwa MTUKANAJI, MWENYE KUUDHI WATU, MWENYE JEURI, lakini nalipata rehema kwa kuwa nalitenda hivyo kwa ujinga, na kwa kutokuwa na imani.
14 Na neema ya Bwana wetu ilizidi sana, pamoja na imani na pendo lililo katika Kristo Yesu.
15 Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi.
16 Lakini kwa ajili hii nalipata rehema, ili katika mimi wa kwanza, Yesu Kristo audhihirishe uvumilivu wake wote; NIWE KIELELEZO KWA WALE WATAKAOMWAMINI BAADAYE, wapate uzima wa milele.
17 Sasa kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu peke yake, na iwe heshima na utukufu milele na milele. Amina”.
Mtu ambaye hakuwahi kumwona Bwana Yesu akitembea duniani, mtu ambaye hakuwepo hata siku ile ya Pentekoste ya kwanza, mtu ambaye alikuwa ndio adui nambari moja wa msalaba, leo hii ndio tunasoma nyaraka zake akitufundisha sisi.
1Wakorintho 15:9 “Maana mimi ni mdogo katika mitume, nisiyestahili kuitwa mitume, kwa sababu naliliudhi Kanisa la Mungu. 10 Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja name”.
1Wakorintho 15:9 “Maana mimi ni mdogo katika mitume, nisiyestahili kuitwa mitume, kwa sababu naliliudhi Kanisa la Mungu.
10 Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja name”.
Hiyo ni kuonyesha kuwa Mungu, hatazami sana, ulimuudhi pakubwa kiasi gani huko nyuma, au uliiharibu kazi yake kiasi gani huko nyuma, anachoangalia ni jinsi gani umemaanisha leo hii kutubu, na kumgeukia, na kumtii yeye. Hapo hapo ndipo anapopatazama sana. Katika hali uliyopo anataka kuanzana na wewe hapo hapo
Na kwa jinsi utakavyoendelea kumaanisha ndivyo atakavyozidi kukupandisha viwango siku baada ya siku, mpaka unakuwa zaidi hata ya wale waliokutangulia katika imani zamani, hao ambao leo hii wanaonekana ni watu wa Mungu wakubwa. Hiyo ndiyo kanuni ya Mungu, hanaga, kwamba kisa huyu nilimtokea, au huyu nilizungumza naye kwa sauti, au huyu nilitembea naye kwa ishara, ndio maana ninampa neema..hilo hana.. ingekuwa ni hivyo asingemfanyia Mtume Paulo, angeendelea tu na wale wale mitume wake 12, kuwafanya wawe juu tu siku zote.
Pale pale unapotubu kwa kumaanisha kabisa kuacha maisha yako ya dhambi na kuanza maisha mapya naye.. Hapo hapo neema yake inaanza kumwagwa juu yako. Na viwango vyako vinapandishwa kuanzia dakika hiyo,.
Hivyo maanisha kumwamini Yesu, ishi maisha kama ya mtu aliyetubu. Onyesha bidii kwake, na wewe mwenyewe utakuwa shahidi kwa pale atakapokufikisha..
Paulo ni kielelezo tosha cha sisi, tunaomwamini Yesu leo, kwamba tutafanywa kama yeye au hata zaidi ikiwa tutakuwa waaminifu kama yeye.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Mharabu ni nani katika biblia?
FAHAMU UWIANO MUNGU ANAOHITAJI KUUONA KWETU.
ANGALIENI MWITO WENU.
IFAHAMU HUZUNI NA FURAHA YA MALAIKA.
Rudi nyumbani
Print this post
AMEN