by Admin | 30 January 2024 08:46 am01
Ifuatayo ni mistari michache ya biblia inayohusu maombi.
Zekaria 10:1 “Mwombeni Bwana mvua wakati wa masika, naam, Bwana afanyaye umeme, naye atawapa manyunyu ya mvua, kila mtu atapewa nyasi kondeni.”
Mathayo 7:7 “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;
8 kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.”
Marko 13:33 “Angalieni, kesheni, [ombeni], kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo”
Luka 22:40 “ Alipofika mahali pale aliwaambia, Ombeni kwamba msiingie majaribuni.”
Yohana 15:7 “Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.”
Yohana 16:24 “Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu”
Wafilipi 4:6 “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu”.
Marko 11:24 “Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu”.
Wakolosai 4:2 “Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani”
Waefeso 6:18 “kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote”
1Wathesalonike 5:17 “ombeni bila kukoma;”
1Yohana 5:14 “Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia”.
1Timotheo 2:1 “Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote”
Yakobo 5:16 “Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii”
Kwa mwongozo wa maombi ya kujikuza kiroho fungua hapa >> MWONGOZO WA MAOMBI YA KUJIKUZA KIROHO.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Nijapokuwa sipo kwa mwili, lakini nipo pamoja nanyi kwa roho,
MISTARI YA BIBLIA KUHUSU NDOA.
MISTARI YA BIBLIA KUHUSU BARAKA
IFAHAMU FAIDA YA KUMKIRI KRISTO UKIWA HAPA DUNIANI.
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/01/30/mistari-ya-biblia-kuhusu-maombi/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.