IFAHAMU FAIDA YA KUMKIRI KRISTO UKIWA HAPA DUNIANI.

IFAHAMU FAIDA YA KUMKIRI KRISTO UKIWA HAPA DUNIANI.

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze biblia,

Bwana wetu Yesu alisema maneno yafuatayo…

Mathayo 10:32  “BASI, KILA MTU ATAKAYENIKIRI MBELE YA WATU, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni..”

Tunapomkiri Bwana Yesu hapa duniani tuna ahadi ya yeye kwenda kutukiri mbinguni mbele za Baba na Malaika lakini pia kuna faida ambayo tutaipata tukiwa hapa duniani kabla hatujafika kule mbinguni. Na moja ya faida hiyo ni ndio kama ile aliyoipata Mtume Petro, alipomkiri Bwana YESU katika usahihi wote mbele ya wote.

Tusome,

Mathayo 16:15  “Akawaambia, NANYI MWANINENA MIMI KUWA NI NANI?

16 Simoni Petro akajibu akasema, WEWE NDIWE KRISTO, MWANA WA MUNGU ALIYE HAI.

17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.

18 Nami nakuambia, WEWE NDIWE PETRO, NA JUU YA MWAMBA HUU NITALIJENGA KANISA LANGU; WALA MILANGO YA KUZIMU HAITALISHINDA.

19 Nami nitakupa WEWE FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni”.

Umeona?.. Kabla tu ya Bwana Yesu kwenda kumkiri Petro mbele za Malaika watakatifu mbinguni, tayari alianza kumkiri akiwa hapa hapa duniani kabla ya kufika kule, kwamba..“YEYE NDIYE PETRO,… NA AKAMPA FUNGUO ZA UFALME WA MUNGU”…kila atakalolifunga duniani litakuwa limefungwa mbinguni na atakalolifungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.

Na sisi tunapomkiri Yesu kisahihi mbele za watu, tunaanza kuvuna matunda yake tukiwa hapa hapa duniani,….vile vile tunaposhuhudia habari zake kisahihi mbele za watu, na kumtangaza kama jinsi anavyotaka, faida yake tunaanza kuipata tukiwa hapa hapa duniani kabla ya kufika kule mbinguni,.. majina yetu yanabadilishwa katika ulimwengu wa roho tukiwa hapa hapa duniani, tunapewa mamlaka nyingine ya kipekee, na funguo za mambo mengi.

Je! Umemkiri Yesu katika maisha yako? (Kumbuka Kristo hatumkiri kwa moyo, bali kwa Kinywa).. Ikiwa na maana kuwa ni lazima tuhusishe vinywa vyetu na sauti zetu katika kumkiri yeye.

Warumi 10:10 “Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na KWA KINYWA HUKIRI HATA KUPATA WOKOVU”.

Je unamtangaza Bwana Yesu mbele za watu?..

Kama bado hujafanya hayo yote, ni vizuri ukafanya maamuzi leo, kwa faida yako mwenyewe ya hapa duniani na katika ulimwengu ujao…Lakini ukimwonea haya naye pia atakuonea haya kuanzia hapa hapa duniani, kabla ya kufika kule mbinguni.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mada Nyinginezo:

USIISHIE TU KUPATA HAKI, BALI PATA NA WOKOVU.

MFALME ANAKUJA.

BADO UPO YERUSALEMU TU..GALILAYA HUTAKI KWENDA?

NJIA YA WOKOVU NDANI YA KITABU CHA WARUMI.

Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
STANSLAUS PAULO SANGA
STANSLAUS PAULO SANGA
19 days ago

Hii ni KAZI njema