Chetezo ni kifaa/chombo kidogo kilichotumika katika tendo la kuvukiza uvumba ndani ya Hema ya Mungu au katika hekalu la Mungu. (Tazama picha juu).
Wakati kuhani alipotaka kufanya kazi za kikuhani ndani ya hema/hekalu la Mungu. Kabla ya mambo yote ilikuwa ni lazima avukize uvumba ndani ya hema/hekalu, lengo la kufanya vile ni kukijaza chumba chote moshi wa ule uvumba.
Hivyo alitwaa kozi mbili za makaa ya moto ambayo yalikuwa yanapatikana katika madhabahu ndogo (ijulikanayo kama madhabahu ya uvumba), iliyokuwa inapatikana upande wa kushoto wa patakatifu pa patakatifu.
Na akiisha kuyachukua yale makaa, ndipo anayatia ndani ya hiko chetezo pamoja na manukato yenye kutoa harufu nzuri yaliyotengenezwa kwa viungo maalumu alivyoviagiza Mungu mwenyewe…
Kutoka 30:34 “BWANA akamwambia Musa, Jitwalie manukato mazuri, yaani, NATAFI, NA SHEKELETHI, NA KELBENA; VIUNGO VYA MANUKATO VIZURI PAMOJA NA UBANI SAFI; vitu hivyo vyote na viwe vya kipimo kimoja; 35 nawe utafanya uvumba wa vitu hivyo, manukato ya kazi ya ustadi wa mtengenezaji manukato, yatakuwa yamekolea, safi, matakatifu”.
Kutoka 30:34 “BWANA akamwambia Musa, Jitwalie manukato mazuri, yaani, NATAFI, NA SHEKELETHI, NA KELBENA; VIUNGO VYA MANUKATO VIZURI PAMOJA NA UBANI SAFI; vitu hivyo vyote na viwe vya kipimo kimoja;
35 nawe utafanya uvumba wa vitu hivyo, manukato ya kazi ya ustadi wa mtengenezaji manukato, yatakuwa yamekolea, safi, matakatifu”.
Na baada ya kuhani, kuvichoma viungo hivyo (manukato) pamoja na yale makaa ndipo moshi huo huo wenye harufu nzuri hupanda juu na kukijaza chumba chote, na hivyo Mungu hushuka kuipokea ibada hiyo. (Tendo hilo ndilo linaloitwa kuvukiza uvumba).
Ilikuwa ni kosa kubwa kufanya kazi ya kikuhani bila kuvukiza uvumba kwanza, vile vile ilikuwa ni kosa kubwa kuhani kutumia viungo vingine katika manukato au moto mwingine mgeni tofauti na ule wa madhabahuni katika zoezi la kuvukiza uvumba..(Soma Kutoka 30:9, Hesabu 3:4).
Kwa mapana zaidi kuhusu Kuvukiza uvumba fungua na ujumbe gani umebeba kiroho fungua hapa >>> KUFUKIZA UVUMBA NDIO KUFANYAJE?
Swali ni je katika agano jipya tuna amri/agizo la kufukiza uvumba katika nyumba za Ibada kama makuhani walivyofukiza katika nyumba ya Mungu katika agano la kale?
Jibu ni la!.. Katika agano jipya hatuna amri wala agizo hilo, kwasababu agano letu si tena la mwilini bali la rohoni, kama vile tusivyozitumia tena damu za wanyama katika ondoleo la dhambi bali damu ya YESU vile vile, hatuvukizi tena uvumba kwa namna yakimwili bali uvumba wetu sisi ni “maombi”.
Sasa CHETEZO kinawakilisha nini kiroho?.
“Chetezo” inawakilisha “moyo wa mtu” kama vile moto unavyowekwa ndani ya chetezo na uvumba kuvukizwa juu ndipo utukufu wa Bwana uonekane…Vivyo hivyo na sisi ni lazima Moto wa Roho Mtakatifu uwashwe ndani yetu na ndipo tuweze kumtumikia Mungu na kuomba sawasawa na mapenzi yake, kwa maana ule uvumba katika nyumba ya Mungu ni ufunuo wa maombi ya watakatifu katika agano jipya. (Ufunuo 8:3).
Je Moyo wako umeufanya safi?.. Biblia inasema tulinde mioyo yetu zaidi ya vyote tuwezavyo kuvilinda (Mithali 4:23).
Bwana atubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
SISI TU MANUKATO YA KRISTO.
MADHABAHU NI NINI?
USICHELEWE KUMPAKA BWANA MARHAMU!
MUNGU HATAZAMI MOTO WA KIGENI,KUWA MAKINI!
Marhamu ni nini? Na Manukato ni nini?
Rudi nyumbani
Print this post