Wagalatia 1:10
[10]Maana, sasa je! Ni wanadamu ninaowashawishi, au Mungu? Au nataka kuwapendeza wanadamu? Kama ningekuwa hata sasa nawapendeza wanadamu, singekuwa mtumwa wa Kristo.
Kuna dhambi moja ya kale, ambayo imekuwa sugu sana, na kibaya zaidi imekuwa tishio kubwa kwa mwanadamu, hata kumfanya ashindwe kabisa kuyatenda mapenzi ya Mungu, haijalishi atamaanisha kiasi gani, dhambi yenyewe si zile tunazozifahamu, kama vile uzinzi, uongo, n.k., Hapana bali ni dhambi ya “kuwapendezesha wanadamu”
Ni dhambi ya kufanya jambo kwa hofu ya kuchikiwa na watu, kufikiriwa vibaya na watu. Hofu ya Kutengwa na watu, kudharauliwa na watu.
Ni kufanya jambo ili machoni pa watu ili utukuzwe, uonekane mkuu, uonekane ni wa rohoni, uonekane unajua kuliko wengine… ni kuwa radhi kuvumiliana na vilivyo kinyume na Mungu ilimradi tu mbele za watu, usipoteze heshima yako.
Bwana Yesu alijua moyo wa mwanadamu unafurahia hali hii, upo radhi kufanya vitu kinafki, bila kujali haja ya Mungu ni nini.
Mathayo 6:2,5
[2]Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu… [5]Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao.
[2]Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu…
[5]Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao.
Ni hali mbaya sana, Mahali pengine waliogopa kumkiri hadharani kwasababu watapoteza heshima zao za kikuhani machoni pa watu..
Yohana 12:42-43
[42]Walakini hata katika wakuu walikuwamo wengi waliomwamini; lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakumkiri, wasije wakatengwa na sinagogi.
Madhara ya dhambii hii ni kwamba, Tunaweza tukayapindisha maandiko tusiongee ukweli wote, tuhubiri injili ya juu juu, injili ya vichekesho, tusikemee aina Fulani ya dhambi kwasababu zitawafanya watu wainamishe vichwa vyao, matokeo yake wasije kabisani.
Hali hii inatufanya tuwe na kigeugeu, ilimvaa hata Petro, wakati ule alipoketi na wayahudi, anasema hivi, alipokutana wa Watu wa mataifa anasema vingine kwa hofu ya wayahudi, mpaka Paulo alipomwona akamkemea mbele ya wote. (Wagalatia 2:11)
Tunaogopa kuvaa mavazi ya kujisitiri yasiyokuwa na mvuto machoni pa watu, lakini mbele za Mungu yanapendeza, kisa tutaonekana washamba, wazee. Nuru yetu inashindwa kuangaza ulimwenguni.
Ijapokuwa Bwana Yesu aliwapenda sana wanadamu, lakini hakuishi kwa kuziangalia hisia zao zinasemaje, kwasababu sifa za wanadamu, hazitabiriki, leo watakusifia, kesho watakuchukia.. Alipoingia Yerusalemu walimwita mbarikiwa Hosana, wiki moja baadaye wakasema Asulubiwe.. Lakini katika nyakati zote hizi hatuoni Bwana Yesu akigeuka, akipindisha pindisha msimamo wake, alipotukwana, hakutazama umati unasemaje, aliutazama utukufu wa Mungu unamwelekezaje.
Hii huitwa hofu ya mwanadamu, Tunasahau kuishi kwa hofu ya Mungu, yaani Mungu anasemaje, Anajisikiaje, tunawaza sana wanadamu wanasemaje, wanafikirije..Hatupaswi kuwafanya watu sanamu zetu.
Ili tushinde hii hali kwanza ni lazima tujue kuwa kumpendezesha kila mtu ni jambo ambalo haliwezekani, hivyo usiogope kufikiriwa kivingine pale unapokusudia kuishi maisha yampendezayo Mungu.
Lakini pia ni lazima ufahamu, wanadamu hawana sifa za kweli, za kudumu, hivyo acha kufanya vitu, kuwaridhisha, ilihali unajua wewe mwenyewe unaumia ndani kwa ndani, na mwisho jitahidi kufanya mambo yako kwa msukumo wako mwenyewe sirini, bila watu kukutazama, hapo utaua sifa za wanadamu, utaanza kuishi kwa kumwangalia Mungu.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Mafundisho mengine:
MWONGOZO WA MAOMBI YA WAHUDUMU/ WASIMAMAO MADHABAHUNI.
Kuwaogopa wanadamu huleta mtego,(Mithali 29:25)
USIONDOE ALAMA YA MPAKA ILIYOWEKWA NA MABABA.
Print this post
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ