Kuwaogopa wanadamu huleta mtego,(Mithali 29:25)

Kuwaogopa wanadamu huleta mtego,(Mithali 29:25)

SWALI: Naomba kufahamu maana ya mstari  huu”

Mithali 29:25 “Kuwaogopa wanadamu huleta mtego, ..”
Ni mitego gani hiyo hukupata iwapo utamwogopa mwanadamu?..


JIBU: Ukiendelea kusoma inasema..
Mithali 29:25
[25]Kuwaogopa wanadamu huleta mtego;
Bali amtumainiye BWANA atakuwa salama.
Hofu ya kwamba mwanadamu atakuonaje, ukitenda jambo fulani la haki..hofu ya mwanadamu atakuchukuliaje siku ukivaa mavazi ya kujisitiri ,hofu ya wazazi,  watakupokeaje pale unapoamua kuokoka..n.k kwa kawaida hofu kama hizi za kuwapendeza wanadamu mwisho wa siku huwa zinakupeleka katika mtego wa kupotea..
Kwamfano..
Sauli aliupoteza ufalme wake kwa kuwaogopa watu na kumwacha Agagi hai. 1Samweli 15:25
Haruni alikuwa katika hatihati ya kuuliwa na Mungu kwa kosa la kuwapendeza wana wa Israeli pale walipomwomba awatengenezee ndama wa dhahabu wamwabudu.
Kutoka 32:22-24
Herode alimwua Yohana mbatizaji kwa kumpendeza mke wake na binti wake Marko 6:21-27..
Herode mwingine naye alimuua Yakobo mtume wa Bwana..pamoja na kumfunga Petro kwa lengo tu la kuwapendeza wayahudi.Matendo 12:1-4
Umeona wote hawa waliishia katika mitego mibaya kwa hofu za wanadamu…
Lakini kinyume chake ni kuwa wanaomtumaini Mungu watakuwa salama.
Shedraka, Meshaki na Abednego walikaidi amri ya mfalme na kumtii Mungu japokuwa walitupwa katika tanuru la moto lakini walitoka salama..
Danieli kwa hofu ya Mungu alikuwa tayari kutupwa katika tundu simba lakini Mungu alitomtoa salama huko nako..
Bwana Yesu alisema  …
Yohana 5:44
[44]Mwawezaje kuamini ninyi mnaopokeana utukufu ninyi kwa ninyi, na utukufu ule utokao kwa Mungu aliye wa pekee hamwutafuti?
Na sisi ili tuwe salama tuutafute utukufu unaotoka kwa Mungu..tukubali njia Kristo aliyoichagua  hata kama dunia nzima itatutenga..na njia yenyewe ni ile ya wokovu na kujikana nafsi.
HivyoTubu dhambi zako ikiwa wewe ni mwenye dhambi. Yesu yupo mlangoni kurudi. Unyakuo ni wakati wowote, kwasababu tunaishi katika kizazi kilichoshuhudia kutimia kwa dalili zote za kurudi kwake mara ya pili.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

MTEGO HUTEGWA BURE, MBELE YA MACHO YA NDEGE YE YOTE.

Nini maana ya “yasiyokuwapo hayahesabiki”(Mh 1:15)

SIKU YA HOFU YANGU NITAKUTUMAINI WEWE.

AOGOPACHO MTU ASIYE HAKI NDICHO KITAKACHOMJILIA.

Waoga ambao hawataurithi uzima wa milele ni watu wa namna gani?(Ufunuo 21:8).

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Irene
Irene
2 years ago

Eimen ubarikiwe sana mtumishi