Furaha ni nini?

Furaha ni nini?

Furaha kwa tafsiri ya kawaida, ni muhemko chanya wa kihisia unaotakana na aidha kuridhishwa na jambo fulani au kupata kitu fulani.

Kwa mfano katika biblia Wale mamajusi walipoina tena ile nyota  ya Bwana kule Bethelehemu, walifurahi.

Mathayo 2:10 “Nao walipoiona ile nyota, walifurahi furaha kubwa mno”.

Utaona pia wale waliokwenda kaburini kwa Yesu,Na kukuta ameshafufuka, Biblia inasema walifurahi sana.

Mathayo 28:8 “Wakaondoka upesi kutoka kaburini, kwa hofu na furaha nyingi, wakaenda mbio kuwapasha wanafunzi wake habari”.

Hata mbinguni malaika wanapoona mtu mmoja ametubu dhambi, huwa wanafurahi pia.

Luka 15:10 “Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye”.

Kwahiyo utaona hapo furaha tunayoijua,  huwa inazaliwa kutokana  na kupatikana kwa kitu fulani kilichokuwa kinatarajiwa au jambo fulani.

Lakini furaha halisi ya ki-Mungu.  Ni furaha inayozidi mipaka, , hata katika shida furaha hii ipo. Ni furaha ambayo huwezi kuielezea kwa upatikanaji tu, kama furaha nyingine, inazidi mipaka hiyo.. Kwa kifupi ni kuwa haiathiriwi na hali au mazingira.

Na furaha yenyewe inaletwa na KRISTO YESU mwenyewe.

Ikiwa na maana mtu anayempokea Kristo, kama Bwana na mwokozi wa maisha yake. Mungu anakuwa na jukumu la kumininia furaha hii kwa Roho Mtakatifu atakayempokea kipindi hicho.

Warumi 15:13 “Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu”.

1Nyakati 16:27 “Heshima na adhama ziko mbele zake; Nguvu na furaha zipo mahali pake”.

Wagalatia 5:22 “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,

23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria”.

Luka 2:10 “Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote;

11 maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana”.

Yokobo 1:2 “Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;

3 mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi”

1Petro 4:13 “Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe”.

Kwa muda wako pitia vifungu hivi

1Petro 1:8, Yohana 17:13

Na wewe ikiwa ni mmojawapo wa wale wanaotaka kuonja FURAHA hii ya Ki-Mungu ambayo si watu wote wanaweza kuonjeshwa utakuwa umefanya uamuzi wa busara sana. Kwasababu ni kwake tu peke yake ndipo Furaha inapopatikana, hakuna mwingine, Bwana anasema hivi;

Zaburi 5: 11 “Nao wote wanaokukimbilia watafurahi; Watapiga daima kelele za furaha. Kwa kuwa Wewe unawahifadhi, Walipendao jina lako watakufurahia”.

Zaburi 51:12 “Unirudishie furaha ya wokovu wako; Unitegemeze kwa roho ya wepesi.

Unaona? Basi fungua leo moyo wako, Kristo aingie ndani yako, kukusamehe, na kukuwekea furaha idumuyo. Ikiwa Upo tayari leo kutubu dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kuziacha, basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba.

Bwana akubariki.

Wafilipi 4:4 Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?

Utii ni nini? na ni nani tunayepaswa kumtii au kutokumtii?

Unyenyekevu ni nini?

Gombo ni nini?

Vifungu vya biblia kuhusu Uongozi.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments