UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?

UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?

Upendo ni kitendo cha kuonyesha hisia za tofauti za ndani kwa mtu mwingine, Ni hisia zinazoonyesha pengine umeridhishwa na mtu huyo, au umemkubali, au umemuhurumia, au unataka kumkaribia uwe karibu naye n.k.

Kibiblia kuna upendo wa aina tatu:

UPENDO WA KWANZA NI UPENDO UNAOTOKANA NA HISIA:

Upendo huu unajulikana kama “EROS” Ni upendo unaozaliwa na hisia, Upendo huu ni maarufu sana kwa mke na mume, katika biblia Sulemani alijaribu kuuleza upendo ya namna hii:

Wimbo 1:13 “Mpendwa wangu ni kama mfuko wa manemane Ukilazwa usiku maziwani mwangu.

14 Mpendwa wangu ni kama kishada cha hina, Katika mizabibu huko Engedi.

15 Tazama, u mzuri, mpenzi wangu, U mzuri, macho yako ni kama ya hua.

16 Tazama, u mzuri, mpendwa wangu, Wapendeza, na kitanda chetu ni majani;

17 Nguzo za nyumba yetu ni mierezi, Na viguzo vyetu ni miberoshi”.

Huu ni Upendo ambao hauwezi kufananishwa na upendo kama wa mtu na ndugu yake au Rafiki yake.

AINA YA PILI YA UPENDO NI UPENDO UNAOZALIWA KWA VITU VINAVYOENDANA:

Unajulikana kama “PHILEO”. Upendo huu unazuka kutokana na mahusiano Fulani mtu mmoja alionao na mwenzake, anaweza akawa ni ndugu, au rafiki, au mchezaji mwenzake, au mfanyakazi mwenzake. Ni upendo ambao kusipokuwa na mahusiano Fulani ya karibu au faida Fulani ambayo mtu anaweza kuipata kwa mwenzake, hauwezi kuzaliwa.

Tunapaswa tupendane sisi kwa sisi, biblia inatuambia hivyo katika (1Yohana 2:9-10), vilevile inatuambia tupendane sisi tulio ndugu katika Bwana, lakini upendo wa namna hii haupo tu kwa waaminio bali hata kwa watu waovu pia wanao..Bwana Yesu alisema:

Mathayo 5:46 “Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?

47 Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo”?

Unaona kwahiyo upendo huu bado hujafikia vile viwango vyenyewe.

AINA YA TATU YA UPENDO NI UPENDO USIO NA MASHARTI. UNAOJULIKANA KAMA “AGAPE” (UPENDO WA KI-MUNGU).

Huu ndio upendo Yesu Kristo aliokuwa anauzungumzia, ni upendo unaompenda mtu bila ya sababu yoyote, Ni upendo wa kiwango cha juu sana, unampenda mtu kwa kutokujali kama na yeye anakupenda au hakupendi, kama anakuchukia au hakuchukii, kama anakusema vibaya au hakusemi vibaya, kama anafaida yoyote kwako au hana faida yoyote kwako.

Upendo huu ndio YESU alikuwa nao kwetu, biblia pale inaposema “alitupenda Upeo”(Yohana 13:1),  ilimaanisha kusema hivyo Alitupenda upeo kweli kweli, sio kwasababu tulikuwa ni watakatifu, au kwasababu tulikuwa waovu…au kwasababu alikuwa anatafuta ukubwa kwetu hapana, alitupenda tu, tena ile wa kutoka moyoni hadi kufikia hatua ya kuutoa uhai wake kwa ajili yetu.

Na upendo wa aina hii ndio Bwana anataka kila mmoja wetu awe nao, Ni ngumu kuufikia, hususani pale tunapoona mtu Fulani anayetuchukia au anatuzungumzia vibaya halafu huyo huyo ndio tunapaswa tumpende, kuna kama ugumu fulani..Lakini Huo ndio Mungu anataka kuuona kwetu haijalishi tutawapenda wake zetu na waume zetu kiasi gani, au ndugu zetu wengi kiasi gani au rafiki zetu wengi kiasi gani kama hatujaweza bado kuufikia huu upendo wa AGAPE, mbele za Mungu bado hatuna upendo..

Hizi ndizo tabia za upendo wa AGAPE.

1Wakorintho 13:4 “Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;

5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;

6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;

7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.

8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika”.

Hivyo ili mimi na wewe tuweze kuufikia Upendo wa namna hii hatupaswi kuungojea kama hizo aina mbili juu, bali tunapaswa tuupapalilie kwa kuvumilia, kwa kutokurudisha baya kwa baya, kwa kutokusengenya, kwa kutokuhesabu mabaya ya mtu tu sikuzote, kuwaelewa watu ..n.k.

Tuombe Mungu atusaidie sote tufike hapo, kwasababu hapo ndipo Mungu mwenyewe alipo, na hiyo ndio inayojulikana kama karama iliyo kuu kuliko zote. Ukiwa nayo hiyo wewe ni zaidi ya nabii yoyote, au mwalimu yoyote, au mwinjilisti yoyote, au mtume yoyote duniani. Mungu anakuwa karibu sana na wewe.

Ubarikiwe sana.

Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/ +225789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

JIRANI YAKO NI NANI?

SAMEHE KUTOKA NDANI YA MOYO WAKO.

MPENDEZE MUNGU ZAIDI.

JE! UNAYO NAFASI MBINGUNI?

HERI, WALE MUNGU ASIOWAHESABIA MAKOSA YAO.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
52 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Jacob Elias
Jacob Elias
8 months ago

Mungu aendelee kuwatunza

Anonymous
Anonymous
9 months ago

Nimepend hiy topic

Jephason Daniel Simon
Jephason Daniel Simon
10 months ago

Mungu awabariki sana

Anonymous
Anonymous
1 year ago

Leave your message Amen

aureus kakogoto
aureus kakogoto
1 year ago

napenda sana vipaji vyenu

Bigaya Galuga
Bigaya Galuga
1 year ago

Jambo

Anonymous
Anonymous
1 year ago

Nafarijika sana na mafundisho haya mungu awabariki

Ezekieli
Ezekieli
23 days ago
Reply to  Anonymous

Naomba kuungwa 0743066039

Lavvino
Lavvino
1 year ago

Nimebarikiwa

Rachel clay
Rachel clay
9 months ago
Reply to  Lavvino

Ubarikiwe somo zuri

Prophet Gaston sanga
Prophet Gaston sanga
1 year ago

Bwana yesu asifiwe nimebarikiwa sana kunakitu nimekipokea

BARAKA PAUL
BARAKA PAUL
2 years ago

Naomba kujiunga nashilikalenu

Shilanga nijle
Shilanga nijle
1 month ago
Reply to  Admin

0752737336

NICHOLAUS MICHAEL
NICHOLAUS MICHAEL
2 years ago

AHSANTE KWA UJUMBE MZURII
NAOMBA KUUNGWA KWENYE GROUP
0753331634

Anonymous
Anonymous
3 years ago

X-MASS POA BRO

Anaher
Anaher
3 years ago

Amen

CEO
CEO
3 years ago

Ahsante mkuu ubarikiwe

Anonymous
Anonymous
3 years ago

Nimependa naomba kuungwa kwa group 0744777111

Rachel mathayo
Rachel mathayo
1 year ago
Reply to  Admin

Naomba uni add kwa group mpendwa 0682342682

Emmanue
Emmanue
1 year ago
Reply to  Admin

Naomb na mim uniunge 0747790771

John kitwana
John kitwana
3 years ago

Ujumbe Mzuri sana!

Barikiwa sana

Anonymous
Anonymous
3 years ago
Reply to  Admin

Amina!
Niunganishe kwenye Group lako

Elixha
Elixha
3 years ago
Reply to  Admin

Amina

Josephat
Josephat
3 years ago

Barikiwa mtumishi!!

Naweza kuyapata masomo haya kwa kupitia email yangu

Ibrahh
Ibrahh
3 years ago

Amina kwa ujumbe mzuri

Mongera Moses
Mongera Moses
3 years ago

Naomba msaada kuna sehemu nilisoma kwenye Biblia ikionyesha mtiririko wa vitu vya kupenda kwanza Mungu pili wazazi tatu mke/mme nne watoto n.k.

Fredy james
Fredy james
3 years ago
Reply to  Admin

Ujumbe mzuri nimeupenda,naomba uniunge kwenye group lako namba yangu ni 0768303021.

Annastazia A Kajange
Annastazia A Kajange
3 years ago

Amina nawe pia ubarikiwe

Valence sangu
Valence sangu
3 years ago

Amina

Aroni
Aroni
4 years ago

Mungu hawabariki Sana watu mungu

Kelvin
Kelvin
3 years ago
Reply to  Aroni

Amen pia na wewe

Kelvin Ngungulu
Kelvin Ngungulu
2 years ago
Reply to  Kelvin

Napenda Sana mafundisho yenu, Mungu awazidishie