Kadhalika na yule Mlawi nae, kumbuka mlawi naye anafanya kazi zinazofanana na za kikuhani katika nyumba ya Mungu, isipokuwa yeye haingii katika patakatifu pa Mungu, tofauti ya Mlawi na Kuhani ni kwamba Kuhani yeye ni Mlawi aliyeteuliwa kutenda kazi katika patakatifu pa Mungu, hivyo kwa cheo huwa anaanza Mlawi, kisha kuhani, na mwisho kabisa ni Kuhani Mkuu. Sasa huyu naye alipomuona yule mtu mwenye majeraha, pengine huruma ilimjia kidogo, lakini alipogundua kuwa hizo sio kazi za Walawi, akaamua naye kupita kando. Naye pia hakufanya kosa, ni kwasababu tu hakupata ufunuo wa “JIRANI HASA NI NANI?”.