Watakaodanganywa baada ya miaka 1000,watatoka wapi?

Watakaodanganywa baada ya miaka 1000,watatoka wapi?

Swali linaendelea….Angali tunajua ndani ya ule utawala kutajawa na watakatifu tu? sasa hawa watu ambao shetani atawadanganya watatokea wapi kama tunavyosoma katika Ufunuo 20:7 “Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake; 8 naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari. 9 Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala.”

JIBU: Katika utawala wa miaka 1000 biblia inarekodi kuwa wenye dhambi watakuwepo, lakini dhambi haitatawala dunia kwasababu mkuu wa ulimwengu ule atakuwa ni MFALME WA AMANI yaani Yesu Kristo, tofauti na dunia ya sasa ambayo mkuu wa ulimwengu huu ni shetani. Hivyo Dhambi na wenye dhambi watakuja kuondolewa wote mara tu baada hukumu ya kile kiti cheupe cha Mungu ambayo itakuja mara baada ya utawala wa miaka 1000 kuisha. Kwahiyo kama vile biblia inavyosema Kristo atatawala kwa fimbo ya chuma pamoja na sisi ukisoma..

Ufunuo 2:26 ″Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa,

27 naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu.”

(fimbo ya ni kwa ajili gani? na ni kwanini iwe ya chuma?. >> Ni dhahiri kuwa Ufalme wowote ni lazima uongozwe kwa mamlaka fulani, na utii chini ya kila kitakachoamriwa pasipo majadiliano wala mahojiano na ndivyo itakavyokuwa katika utawala wa Bwana wa miaka 1000, hivyo kwa yeyote atakayekaidi atalazimika kutumikia adhabu kali ). Hautakuwa utawala wa kimabavu bali ni wa amani na utaratibu lakini kwa watakaokuwa wanaenda kinyume na sheria ya MFALME (KRISTO) na watakatifu wake wataangukia laana. Kwa muda wako binafsi unaweza ukasoma Zekaria 14 yote, inaelezea adhabu zitakazowakuta mataifa yote wasiokwenda kumwabudu mfalme mwaka kwa mwaka Yerusalemu,

Ukisoma pia Isaya 65:17-20 Inasema..;

“17 Maana, tazama, mimi naumba mbingu mpya na nchi mpya, na mambo ya kwanza hayatakumbukwa, wala hayataingia moyoni.

18 Lakini furahini, mkashangilie daima, kwa ajili ya hivi niviumbavyo; maana, tazama, naumba Yerusalemu uwe shangwe, na watu wake wawe furaha.

19 Nami nitaufurahia Yerusalemu, nitawaonea shangwe watu wangu; sauti ya kulia haitasikiwa ndani yake tena, wala sauti ya kuomboleza.

20 Hatakuwapo tena mtoto wa siku chache, wala mzee asiyetimia siku zake; kwa maana mtoto atakufa mwenye umri wa miaka mia; BALI MTENDA DHAMBI MWENYE UMRI WA MIAKA MIA ATALAANIWA.”

Hivyo tunaona atakayetawaliwa hapo kwa fimbo ya chuma sio mkristo bali watakuwa ni watu wengine watakaokuja kuzaliwa ndani ya huo utawala wa miaka 1000. Na ndio maana huo mstari unasema “mtenda dhambi mwenye umri wa miaka mia atalaaniwa” ikimaanisha kuwa ndani ya huo utawala kutakuwa na makundi mchanganyiko. Kwasababu kumbuka ile siku ya mwisho ya Bwana inayowaka kama Tanuru, atakayokuja pamoja na sisi(Bibi-arusi) kuuharibu ulimwengu wa sasa haitamaliza watu wote bali kuna watu wachache sana watakaosalia,soma Isaya 13:9-13

Tazama, siku ya Bwana inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.

10 Maana nyota za mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze.

11 Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali;

12 nitafanya wanadamu kuadimika kuliko dhahabu safi, na watu kuliko dhahabu ya Ofiri.

13 Kwa hiyo nitazitetemesha mbingu, na dunia itatikiswa itoke katika mahali pake, kwa sababu ya ghadhabu ya Bwana wa majeshi, na kwa sababu ya siku ya hasira yake kali.”

Umeona hapo watu wataadimika kuliko dhahabu,ni jinsi gani watakavyobaki wachache sana na hao ndio watakaopata neema ya kuingia katika utawala wa miaka 1000 katika miili yao ya asili( Na hawa ndio watakaokuwa wakizaa na kuzaliana) lakini sisi tutakao kuja na Kristo kutakuwa hakuna kuzaa wala kuzaliana kwa sababu tutakuwa na ile miili ya utukufu iliyotoka mbinguni. Na pia wale waliouawa na mpinga-kristo (wanawali wapumbavu) nao watafufuliwa na kuhukumiwa kisha wataingia katika utawala wa miaka 1000. Ufunuo 20:4.

Sasa baadhi ya hawa watu (watakaozaliwa kwenye huu utawala) baadaye Shetani atakapokuja kufunguliwa kuwajaribu, shetani atawadanganya ndio watakaotaka kufanya vita dhidi ya watakatifu, kama biblia inavyosema moto utashuka kutoka mbinguni na kuwameza wote. ndipo hukumu ya kiti cheupe itafuata kwenye ufufuo wa pili. ambapo waovu wote watahukumiwa na kutupwa katika ziwa la moto pamoja na shetani na kisha tutaingia katika umilele ambapo dhambi haitakuwepo tena wala waovu.

Ubarikiwe sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

UTAWALA WA MIAKA 1000.

Kati ya Unyakuo wa kanisa, Dhiki kuu, Vita vya har-magedoni, Utawala wa miaka 1000, Vita ya gogu na magogu, hukumu ya kiti cha enzi cheupe. Je, ni nini kinaanza na kingine kufuata kwa mpangilio wa matukio hayo?

Wale Watakatifu waliofufuka na Bwana Yesu WALIKUWA WAPI KABLA YA KUFUFUKA kwao je! walikuwa Peponi au ni wapi?.

Je! ni kweli dunia iliumbwa takribani miaka 6000 iliyopita? na je! Shetani alikuwepo duniani wakati dunia inaumbwa?

JINA LA MUNGU NI LIPI?

JE! UNA MASIKIO YANAYOSIKIA?


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments