LITURJIA NI NINI? NA JE IPO KIMAANDIKO?.

LITURJIA NI NINI? NA JE IPO KIMAANDIKO?.

Liturjia/Litrujia ni mwongozo wa jinsi ya kufanya ibada unaotumiwa na makanisa mengi.

Ibada inaundwa na vitu vikuu vitano, ambavyo ni Maombi, Neno, Matoleo, Sifa, na Meza ya Bwana. Vitu hivi vitano ndivyo vinavyoiunda ibada.

Kwahiyo ukiwapo mwongozo wowote wa jinsi ya kuviendesha vitu hivi, na mwongozo huo ukawekwa kwenye kitabu maalumu..Mwongozo huo ndio unaojulikana na wengi kama Liturjia.

Kikawaida hakuna kanisa lisilo na mwongozo, na ni jambo la kimaandiko makanisa yawe na mwongizo fulani, ili mambo yote yafanyike kwa uzuri na utaratibu..

1 Wakorintho 14:40 “Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu”.

Kanisa lisilo na utaratibu, ni rahisi kushambuliwa na shetani na kuvurugwa.

Lakini sasa mwongozo huu unatakiwa ufanyika kwa kipimo fulani, sio uzidi mipaka hata kuchukua nafasi ya Roho Mtakatifu.

Mwongozo wa kanisa unapovuka mipaka, hata kuchukua nafasi ya Roho Mtakatifu ndani ya kanisa, mwongozo huo unageuka na kuwa sumu ya kuliharibu kanisa kiroho.

Kwamfano, kanisa linapoweka ratiba ya masomo na mahubiri ya mwaka mzima, na kuyaweka kwenye kitabu maalumu..kwamba jumapili hii, litasomwa Neno kutoka kitabu fulani, jumatano ni kutoka kitabu fulani, sura namba fulani, na mstari namba fulani..Hivyo kunakuwa hakuna ruhusa ya kufundisha jambo lingine lolote nje na utararibu huo (Liturjia hiyo).

Mfumo kama huo (Liturjia/Litrujia) unamzuia Roho Mtakatifu, na kumzimisha asifanye kazi ndani ya kanisa, na hivyo kudhoofisha nguvu ya kanisa..

Kwasababu hata Roho Mtakatifu akitaka kusema jambo lingine jipya kupitia mhubiri huyo, tayari kuna mfumo unaolizuia hilo unaosema, fundisha tu kilichopo kwenye liturjia.

Roho mtakatifu akitaka kuwafungua watu kwa njia ya maombezi, kunakuwa tayari kuna mfumo uliowekwa unaolizuia hilo, mtu akitaka kutoa unabii upo mfumo tayari unaomzuia, ambao unasema ni kusoma Neno tu, Roho akishuka na kuwaongoza watu kunena kwa lugha na kufasiri, kunakuwa na mfumo unaozuia hilo n.k.

Na maandiko yanasema..tusimzimishe Roho..

1 Wathesalonike 5:19 “Msimzimishe Roho”.

Sasa mfumo kama huo (au Litrujia hiyo), ni mpango wa adui.

Makanisa mengi sasa, hususani yale yanayojulikana sana ndio yamemzimisha Roho Mtakatifu kwa sehemu kubwa sana kupitia hizo Liturjia. Unakuta Kanisa kwa nje linapendeza, lina vutia, linawashirika wengi, lakini ndani halina Roho Mtakatifu..bali miomgozo ya wanadamu, na kanuni za kibinadamu.

Roho Mtakatifu ndio uhai wa kanisa, mtu yeyote au kanisa lolote likikosa Roho Mtakatifu hilo sio kanisa la Mungu tena, bali la wanadamu (Warumi 8:9).

Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba, Liturjia ni nini?.. ni mifumo ya wanadamu ya jinsi ya kufanya ibada, na katika zama hizi, Litrujia zote zimezidi kimo cha Kristo na hata kuchukua nafasi za Roho Mtakatifu.

Hivyo hatuna budi kufuata mwongozo wa Roho Mtakatifu na si Liturjia zetu zilizomzimisha Roho Mtakatifu.

Utaratibu bora ni ule wa kupanga muda wa ibada, siku za kukusanyika, utaratibu wa matoleo, ratiba za wakati wa maombi, na kujifunza biblia..(Na hata huo pia unaweza kugeuzwa kulingana na wakati na wakati, jinsi Roho atakavyo liongoza kanisa).

Na usiofaa ndio huo wa kupanga nini cha kufundisha cha mwaka mzima, na kukiweka kwenye kitabu… kamwe hatuwezi kumpangia Roho Mtakatifu nini cha kusema cha mwaka mzima, yeye anatoa ufunuo siku kwa siku, kwa jinsi atakavyo yeye..na sio sisi tumpangie cha kusema kupitia liturjia zetu, huo ni mpango wa adui wa kuliharibu kanisa.

Bwana atusaidie na kutubariki.

Maran atha!.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?

Kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?

AHADI YA ROHO ILIYOSALIA SASA KWA KIPINDI CHETU.

Nini maana ya kuabudu?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments