Vifungu vya biblia kuhusu Uongozi.

Vifungu vya biblia kuhusu Uongozi.

Aina za Uongozi

Uongozi umegawanyika katika aina kuu tatu. 1) Uongozi wa Madhabahuni, 2) Uongozi wa kiserikali na 3) Uongozi wa kijamii.

          1. Uongozi wa Madhabahuni

Uongozi wa madhabahuni, ndio uongozi wa ngazi ya juu kuliko mwingine wowote ule. Uongozi huu ndio unahusisha Wachungaji, Wainjilisti, Waalimu, mitume na Manabii. Watu hawa ndio Mungu kawachagua katika kulingoza kanisa lake (Waefeso 4:11), na katika uongozi wa kanisa, ni wanaume tu ndio waliopewa hiyo dhamana.. Maana yake, biblia haijaruhusu wanawake, kuwa wachungaji wala waalimu.

1Timotheo 2:11 “Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna.

12 Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.

13 Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye”.

               2. Uongozi wa Kiserikali.

Uongozi wa kiserikali ndio unahusisha, viongozi wote wa kimamlaka.. mfano, Raisi, Mawazili, wabunge, madiwani, wakuu wa mikoa, mameya, wenyekiti wa mitaa, na hata wajumbe.

Hawa maandiko yanasema pia ni watumishi wa Mungu, lakini katika utumishi wa mambo ya kimwili.

Warumi 13:1 “Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu.

2 Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu”.

Na Mkristo yeyote Yule anaweza kushika mojawapo ya hizi nafasi, lakini Haiwezekani kutumika katika nafasi ya Uongozi wa madhabahuni na uongozi wa kiserikalini kwa wakati mmoja.. Haiwezekani kuwa Mchungaji na hapo hapo kuwa Raisi au mbunge.

Majukumu ya kiongozi wa Serikali kibiblia ni yapi?

  1. Kuwa Mwaminifu kwa Mungu aliyeruhusu uishike hiyo nafasi.

 mfano wa akina Shedraki, Meshaki na Abednego.. Ambao walikuwa ni mawaziri wa Mfalme Nebukadneza, siku walipoambiwa waisujudie sanamu ya Nebukadneza, walimheshimu Mungu zaidi ya mwanadamu, na hivyo Mungu akawaokoa na lile tanuru la Moto.

  1. Kuwa Mwaminifu kwa aliyekupa dhamana ya uongozi.

Kama umepewa dhamana hiyo na wananchi, basi kuwa mwaminifu kwao kwa kutekeleza yote uliyowaahidi kwa wakati, na kama umepewa dhamana hiyo kwa kuteuliwa na kiongozi aliye juu yako, basi kuwa mwaminifu katika hiyo nafasi kwa kutenda yale yote uliyoteuliwa kuyafanya, kwa uaminifu wote na utakatifu.. Mfano wa Danieli.

Danieli aliwekwa kuwa kama Waziri mkuu katika ufalme wa Uajemi, lakini siku zote alikuwa mwaminifu kwa mfalme, na wala hakuwahi kula rushwa kama maliwali wengine.

Danieli 6:1 Ilimpendeza Dario kuweka juu ya ufalme maliwali mia na ishirini, wawe juu ya ufalme wote;

2 na juu yao akaweka wakubwa watatu, na Danielii alikuwa mmoja wao; ili maliwali hawa watoe hesabu kwao, mfalme asipate hasara.

3 Basi Danielii huyo alipata sifa kuliko wakubwa na maliwali, kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote.

4 Basi mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Danielii kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake.

         3. Uongozi wa kijamii

Mfano wa uongozi wa kijamii ni ule wa kifamilia, au kikabila.. Baba anaweza kuwa kiongozi wa familia, kadhalika mtu fulani anaweza kuwa kiongozi wa kabila fulani, mwanafunzi anaweza kuwa kiongozi wa wanafunzi wenzake (yaani kiranja) n.k

Majukumu ya kiongozi wa aina hii yanafanana na hayo ya uongozi wa kiserikali. Maana yake unahitaji UAMINIFU, kwa aliyekupa hiyo dhamana.

Hayo ndio mambo muhimu katika uongozi ya kuzingatia. Kumbuka tena jambo hili, siku zote “Uongozi ni dhamana”. Hivyo ukitaka ufanikiwe katika uongozi wa aina yeyote ile basi huna budi kuwa mwaminifu kwa aliyekupa hiyo dhamana, iwe ni Utumishi wa madhabahuni au wa kiserikali au kijamii, UAMINIFU NDIO SILAHA.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

WAOMBEENI WANAOWAUDHI.

Kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?

INJILI YA MANENO LAINI ITAKUGHARIMU.

YANAYOENDELEA SASA KATIKA MADHABAHU YA MUNGU ROHONI.

Konzi ni nini?(Mhubiri 4:6)

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments