Binadamu wa kwanza alikuwa ni “Adamu” na maandiko yanasema aliishi miaka 930.
Mwanzo 5:5 “ Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa”.
Adamu, hakuwa mtu aliyeishi miaka mingi kuliko wote. Maandiko yanarekodi kuwa Methusela ndiye aliyeishi miaka mingi zaidi, miaka 969 (Mwanzo 5:27).
Na mtu wa kwanza kuishi duniani, hakuwa “Nyani” kama Sayansi inavyosema, bali mtu wa kwanza alikuwa ni Adamu, ambaye aliumbwa na Mungu, na baadaye Hawa, na baada ya hapo, ndipo vizazi vya wanadamu vikatokea kupitia Adamu na Hawa.
Kwahiyo binadamu wa kwanza aliishi miaka mingapi?..Jibu: Aliishi miaka 930, na tangu Adamu mpaka sasa hivi karne hii ya 21, ni tofauti ya miaka takribani elfu sita (6,000), ambayo imegawanyika katika vipindi vitatu.
Kipindi cha kwanza ambacho kwa madirio ni miaka elfu mbili, ni tangu Adamu aumbwe mpaka Gharika ya Nuhu, na baada ya Gharika ya Nuhu mpaka kipindi cha kuzaliwa kwa Bwana Yesu ni tofauti ya miaka mingine elfu mbili, na baada ya Bwana Yesu mapaka sasa ni miaka zaidi ya Elfu mbili mingine, hivyo Jumla ya miaka tangu Adamu mpaka sasa katika karne hii ya 21, ni miaka takribani elfu 6 na miaka kadhaa.
Lakini yote katika yote, Adamu mtu wa kwanza alikufa, ila yupo mwingine ambaye anajulikana kama Adamu wa pili, ambaye anadumu milele, alikufa akafufuka na sasa anaishi, na hafi tena, na huyo si mwingine zaidi ya Yesu Kristo.
Huyo ndiye wa kumtegemea katika wakati huu wa sasa, kwasababu mamlaka yote ya mbinguni na duniani kakabidhiwa yeye, baada ya Adamu kuyapoteza pale Edeni.
Hivyo kila mtu amwaminiye Yesu, anapata ondoleo la dhambi, na ahadi ya uzima wa milele, na asiyemwamini atahukumiwa.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.
JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.
KUJIPAMBA NI DHAMBI?
Bwana Yesu alikufa akiwa na umri gani?
Rudi nyumbani
Print this post
Nashukuru kwa ujumbe