Bwana Yesu alikufa akiwa na umri gani?

Bwana Yesu alikufa akiwa na umri gani?

Biblia inatuonyesha Bwana Yesu alianza huduma yake akiwa na umri wa miaka kama 30. Luka 3:23.

Sasa ili tujue alikufa na umri gani, ni vizuri kwanza tukajua urefu wa huduma yake ulikuwa ni miaka mingapi, na hiyo ndio itakayotusaidia kujua alikufa na umri gani.

Tukisoma  kitabu cha Yohana kinatuonyesha Bwana alihudhuria sikukuu za Pasaka zisizopungua tatu.

Ya kwanza tunaisoma katika Yohana 2:13, Ya pili katika 6:4, Na ya tatu tunaisoma katika 11:55-57

Kama tunavyojua pasaka hizi zilikuwa ni mwaka kwa mwaka, hivyo  tukijumlisha hapo, tunaweza kupata hesabu ya miaka miwili (2).Ili kuelewa vizuri, chukulia mfano sikukuu ya kwanza ilikuwa ni mwezi april mwaka huu,  sikukuu ya pili itakuwa ni mwezi April mwaka kesho, na sikukuu ya tatu itakuwa ni mwezi April mwaka kesho kutwa,. Hivyo ukianza kujumlisha tangu april mwaka huu, hadi April mwaka kesho kutwa utaona ni jumla ya miaka miwili mizima.

Lakini kutokana na kurekodiwa kwa matukio mengi ambayo aliyafanya Yesu, pamoja safari zake nyingi, wanazuoni walihitimisha  kuwa kulikuwa na pasaka nyingine ambayo haijaandikwa katika biblia ilipita hapo katikati.

Na pasaka yenyewe iliangukia kati ya ile pasaka ya kwanza (Yohana 2:13) na ile ya pili (Yohana 6:4)..Kufanya muda wa huduma ya Yesu Kristo kuwa ni miaka 3.

Lakini, pia yapo matukio mengine ambayo yalitendekea kabla ya ile pasaka ya kwanza kufika, tunaona tangu Bwana Yesu abatizwe pale Yordani na Yohana,  kulikuwa ni kipindi ambacho alifunga siku 40 kule jangwani, kulikuwa na wakati alisafiri kutoka Yordani, kwenda Kana, na baadaye kwenda Yerusalemu, kulikuwa na kipindi aliwaita wanafunzi wake na kuanza huduma ya kuhubiri, yote hayo yalichukua kipindi cha miezi kadhaa,kabla ya kuifikia ile pasaka ya kwanza. Na pia baada ya kufa na kufufuka kulikuwa na siku 40 ambazo aliwatokea watu wengi, kabla ya kupaa.

Hivyo tunaweza kusema, huduma ya Yesu Kristo, inakadiriwa kwenda kwa miaka mitatu na nusu.

Tukijumlisha na ile miaka 30 ya mwanzo, tunapata miaka thelathini na tatu na nusu. Hivyo Bwana Yesu alikufa akiwa na umri wa miaka hiyo (Thelathini na tatu na Nusu).

Lakini ni nini tunajifunza katika maisha ya Kristo?

Kristo Yesu Bwana wetu alikufa akiwa bado na umri mdogo  sana, kwa dunia ya sasa watu watasema amekufa kabla ya wakati. Lakini tunaona katika umri huo mdogo aliimaliza kazi ile aliyoitwa duniani, na hivyo mbinguni akaonekana ndiye aliyefanya kubwa na yenye faida kuliko wanadamu wote waliowahi  kuishi duniani, sio wale waliokufa wakiwa na miaka 900, wala wale waliokuwa na miaka 120, hakuna hata mmoja aliyefanya kazi kubwa yenye matunda mengi kama Kristo hapa duniani.

Siri ilikuwa ni nini?

Embu tafakari kwa maneno yake mwenyewe aliyoyasema katika vifungu hivi;

Yohana 9:4 “Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi”.

Yohana 11:9 “Yesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu”.

Yohana 4:33 “Basi wanafunzi wake wakasemezana, Je! Mtu amemletea chakula?

34 Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake”.

Mpaka hapo tunaweza kuona Bwana wetu alikuwa ni mtu wa namna gani.. Ni mtu ambaye aliuthamini muda wake akiwa hapa duniani, alijua kuwa muda hautakuwepo wakati wote, kuna siku giza litakuja na mtu asiweze kufanya kazi tena, aliichukulia kazi ya Mungu kama ndio chakula chake, kinachomfanya aishi hapa duniani, kwamba bila hicho atakufa, na kama tunavyojua mtu kula ni lazima kila siku.Hivyo yeye kuifanya kazi ya Mungu ilikuwa ni desturi yake kila siku na kila wakati..

Na ndio maana haikumchukua hata muda mrefu kumaliza huduma yake, hakusongwa na kitu chochote katika huu ulimwengu..

Je! Na  sisi tunaweza kufanana naye?. Bwana atutie nguvu tuwe kama yeye..  Kwa nguvu zake tu peke yake ndio tutaweza.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

MWANZO WA INJILI YA YESU KRISTO.

KWANINI NI YESU KRISTO WA NAZARETI?

MWINUE YESU KRISTO KATIKA MAISHA YAKO.

ALIPO NA ATAKAPOKUWEPO BIBI-ARUSI WA YESU KRISTO.

JINSI SHETANI ANAVYOZUIA MAJIBU YA MAOMBI YETU.

UTAWALA WA MIAKA 1000.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
John
John
2 years ago

Bwana akubariki kwa neno nzuri sana linanijenga sana.Ameen

Magdalena
Magdalena
2 years ago

BWANA AIKUZE NA KUIINUA HUDUMA HI YA KUIHUBIRI INJILI