KWANINI NI YESU KRISTO WA NAZARETI?

KWANINI NI YESU KRISTO WA NAZARETI?

Jina la Bwana wetu libarikiwe daima. Nakukaribisha katika kujifunza Maneno ya Mungu. Leo kwa ufupi tutatazama sehemu ya maisha ya Bwana wetu Yesu jinsi yalivyokuwa hapa duniani. Kama tunavyojua maisha yake ni ufunuo tosha wa kanisa la Kristo jinsi linavyopaswa liwe.

Tukisoma maandiko tunaona Bwana Yesu alitabiriwa kuwa atatokea katika uzao wa Daudi, na pia katika  mji wake ujulikanao kama Bethlehemu (kasome Mika 5:1, na Mathayo 2:6), na kama tunavyojua ni kweli yalitimia kama yalivyotabiriwa, alizaliwa Bethlehemu ya Uyahudi. Lakini Yesu hakuishi katika mji huo wa Daudi (Bethlehemu) au katikati ya wazao wa Daudi, bali alikwenda kuishi katika mji mwingine mmoja mdogo huko Galilaya ulioitwa Nazareti, ulio mbali kabisa na mji wa Bethlehemu. Nazarethi uli

Mji huu ulikuwa kaskazini mwa Israeli, na ndio wa mwisho kabisa kimaendeleo kuliko miji yote iliyokuwa Israeli wakati ule, ni mji ambao haukuandikiwa unabii wowote katika biblia nzima, japo Mungu tayari alikuwa ameshautolea unabii wake kupitia vinywa vya manabii wake (Mathayo 2:23). Ni mji ambao haukuwa na watu wengi, mji ambao haukuwa machachari, mji uliosahaulika kabisa, wala hakuna mtu aliyetazamia kuwa mtu yeyote mkuu angeweza kutokea huko?

Na ndio maana utaona hata Filipo alipokuwa anamwelezea Nathanieli habari za masihi, Nathanieli alimwambia Je! Inawezekana kweli jambo jema kutokea Nazareti, Mji kama ule ambao hauna sifa yoyote nzuri, iweje Masihi atokee huko, maandiko yanatuambia masihi atatokea mji mtakatifu kule Bethelemu, Yuda, iweje utuletee habari ya kijiji hichi ambacho hata hakina sifa yoyote nzuri,

Yohana 1:46 “Nathanaeli akamwambia, Laweza neno jema kutoka Nazareti? Filipo akamwambia, Njoo uone”.

Lakini hapo ndipo mahali sahihi ambapo Mungu alipachagua mwokozi wa ulimwengu aishi kwa miaka karibia 30. Karibia asilimia 90 ya maisha ya Bwana Yesu yalikuwa katika mji huu uliosahaulika, na ndio maana utaona kila mahali watu walikuwa wanamtambulisha kama Yesu wa Nazareti (Mathayo 26:11), Hiyo yote ni kwasababu maisha yake mengi aliyaishia huko. Na sio tu watu na mitume peke wao walimtambulisha kwa jina hilo,  Pilato naye alimtambua kwa jina hilo, Mapepo nayo yalimtambua kwa jina hilo..

Marko 1:23 “Na mara palikuwapo ndani ya sinagogi lao mtu mwenye pepo mchafu; akapaza sauti,

24 akisema, Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je! Umekuja kutuangamiza”?

Hata yeye mwenyewe Bwana, alijitambulisha kwa jina la mji wake siku ile alipomtokea Sauli alipokuwa anakimbilia Dameski;

Matendo 22:6 “Ikawa nilipokuwa nikisafiri, nikikaribia Dameski, wakati wa adhuhuri, ghafula nuru kuu ilitoka mbinguni, ikanimulikia pande zote.

27 Nikaanguka nchi, nikasikia sauti ikiniambia, Sauli, Sauli, mbona unaniudhi?

8 Nikajibu, Wewe u nani, Bwana? Akaniambia, Mimi ni Yesu Mnazareti, ambaye wewe unaniudhi”.

Inawezekana na sisi tunamtambia Bwana Yesu kwa jina hilo, lakini tumekuwa hatujui ni kwanini tunamwita wa Nazareti, tunapaswa tujue ni kwanini iwe Nazareti na sio Bethlehemu, au Korazini, au Kapernaumu?

Mungu anataka  na sisi, tujue mazingira yetu, sio sababu ya yeye kutotimiza ahadi zake juu yetu. Kuna wengine wanasema ni kwasababu nipo kijijini, laiti ningekuwa mjini ningefanya hiki au kile kwa ajili ya Mungu, hiyo isiwe sababu ndugu, mkumbuke Yesu, Yule Yesu wa Nazareti na sio Yesu wa Bethlehemu..upate kujifunza!.

Pengine utasema kwasababu nimezaliwa Afrika, ningezaliwa ulaya ningemfanyia Mungu makubwa, ndugu mkumbuke Yesu wa Nazareti.

Tusiwe na sababu zozote zile, Bwana wetu alizaliwa katika hori la kulishia ng’ombe, alikuwa maskini biblia inatuambia hivyo, aliishi katika mji usiokuwa na maendeleo yoyote. Lakini kutoka katika mji huo dunia nzima imejua kuwa yeye ni mwokozi Yule Yule aliyetabiriwa na manabii.

Hivyo na sisi katika mazingira yoyote tuliyopo, haijalishi ni mazuri au mabaya, haijalishi ni ya kisasa au ya kale, tanaweza kulikamilisha kusudi la Mungu kikamilifu, kama Mungu alivyokusudia, endapo tukiwa waaminifu kwake kama Mwokozi wetu alivyokuwa mwaminifu kwa Baba.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

KUNA WAKATI YESU ATAPITA NA WATU HAWATAJUA.

NI KWANINI MUNGU HAONEKANI?

KUZALIWA KWA YESU.

TAZAMA, MWISRAELI KWELI KWELI, HAMNA HILA NDANI YAKE!

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments