KUZALIWA KWA YESU.

KUZALIWA KWA YESU.

kuzaliwa kwa Yesu kulikuwaje?


Mathayo 1:18 “Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

19 Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri.

20 Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

21 Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.

22 Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema,

23 Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.

24 Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwagiza; akamchukua mkewe;

25 asimjue kamwe hata alipomzaa mwanawe; akamwita jina lake YESU”.

Yesu mwokozi, kama si kuzaliwa kwake ulimwenguni, leo hii tungekuwa wapi? Kama sio kuimwaga neema yake duniani, tungepatia wapi ondoleo la dhambi?

Mamajusi walitoka nchi ya mbali, kwa furaha tu ya kumwona mwokozi wa Ulimwengu, ambaye hata hakuzaliwa katika nchi yao..lakini kwa kuiona tu nyota yake, hawakusubiri, wahadithiwe, walianza safari..

Lakini Swali la kujiuliza Je! Na wewe amezaliwa moyoni mwako?

Bwana Yesu lipoanza kuitenda kazi ambayo Baba yake amemtumia alisimama na kusema maneno haya..

Luka 4:18 “Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,

19 Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa”.

Hiyo ni kazi kubwa ambayo ilimleta duniani, na ndio maana mwishoni kabisa mwa kitabu cha Ufunuo alisema hivi..

Ufunuo 21:6 “Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure”.

Hivyo mpe leo Yesu maisha yako, ayaokoe, akufanye kuwa kiumbe kipya. Hizi ni siku za mwisho, Yesu yupo mlangoni kurudi.Dalili zote zinaonyesha, kuwa mimi na wewe tunaweza kushuhudia tukio la Unyakuo.

Bwana atusaidie sana.

Shalom.

Ikiwa utapenda mafundisho ya biblia yawe yanakufikia kwa njia ya whatsapp, basi tutumie ujumbe kwa namba hii: +255789001312

Mada Nyinginezo:

KWANINI YESU KRISTO ALIKUJA DUNIANI?

JIFUNZE NENO LA MUNGU KWA BIDII ZOTE.

EPUKA MUHURI WA SHETANI

https://wingulamashahidi.org/2018/07/19/nyakati-saba-za-kanisa-na-wajumbe-wake/

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

Kuhutubu ni nini?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator