USHIRIKINA NA MADHARA YAKE.

USHIRIKINA NA MADHARA YAKE.

Ushirikina na madhara yake, rohoni ni yapi?


Ushirikina ni kitendo cha kwenda kutafuta msaada wa kiroho au wa kimwili katika mamlaka ya giza. Nikisema mamlaka ya giza namaanisha kwa shetani na mapepo na majini yake yote yanayofanya kazi kupitia watu wanaoitwa waganga au wachawi.

Sasa unapoumwa, halafu badala ya kwenda kuwa Mungu upate msaada, wewe unakimbilia kwa waganga wa kienyeji ili upate msaada ya kiganga, hapo moja kwa moja tayari umeshashirikiana na mashetani katika ulimwengu wa roho.

Au unapopitia matatizo Fulani aidha ya kifamilia, au ya kikazi, au unahaja ya jambo Fulani pengine masomo, au ndoa, au cheo, halafu wewe moja kwa moja unakimbilia kwa mganga akusaidie kutatua tatizo lako, ujue kuwa tayari umeshaingizwa katika mtandao wa Mashetani.

Jambo ambalo wengi hawajui ni kuwa, walau kwa mtu wa kawaida yeyote, kunakuwa na ka-ulinzi Fulani kutoka kwa Mungu, ambacho anazaliwa nacho hicho kanamfanya shetani asiweze kujiamulia tu jambo lolote atakalo juu ya huyo mtu, vinginevyo ungekuwa shetani kashawamaliza watu wote duniani, kwa kuwaua, Ndio ni kweli ataweza baadhi  lakini sio yote. Sasa pale mtu anapokwenda kwa shetani mwenyewe kumwomba msaada, maana yake ni  kuwa anasaini naye mkataba rasmi kuwa kuanzia sasa, huy mtu ni wangu na naweza kufanya jambo lolote juu yake.

Haya ndio madhara ya moja kwa moja ya ushirikina.

  1. Unaingiliwa na mapepo:

Angalia vizuri utaona asilimia kubwa ya watu wanaoudhuria kwa waganga wanakuwa wanasumbuliwa na nguvu za giza, au wengine wanapata ulemavu Fulani ambao hapo kabla hawakuwa nao, au ugonjwa Fulani, ambao hauponi, hiyo yote ni kutokana na mtu kujishughulisha na ushirikina.

  1. Unakuwa hatarini kufa:

Kutokana na kuwa tayari umeshajihalalisha kwa shetani, basi shetani kazi yake kubwa iliyobakiwa nayo kwako ni kukuua,..Kwasababu ndio dhumuni lake hapa duniani, kuua biblia inasema hivyo…

Yohana 8:44 “Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake”.

  1. Chochote unachokifanya hutafanikiwa:

Hata kama kitaonekana kukuletea matokeo mazuri kiasi gani mwanzoni, kumbuka hiyo ni gia tu ya shetani kukuvuta kwake, ili usimwache, lakini katika kipindi cha muda mrefu, hakitakufikisha popote, kama ulikuwa umekwenda kutafuta mali, hizo mali zitapotea tu baada ya kipindi Fulani, kama ulikuwa umekwenda kutafuta kazi, hiyo kama unaweza usiipate, na hata ukiipata haitadumu, utakuwa ni mtu ambaye anafanya jambo lakini baada ya muda mrefu haoni faida ya jambo hilo, au haoni maendeleo yoyote. Na mwisho wa siku unajikuta ni heri usingeenda.

Mithali 11:21 “Hakika, mtu mwovu hatakosa adhabu; Bali wazao wa wenye haki wataokoka”.

Ayubu  21:13 “Siku zao hutumia katika kufanikiwa, Kisha hushuka kuzimuni ghafula”.

  1. Unapoteza Utu na uwezo wa kupambanua mambo ya rohoni:

Kumbuka pale unapokwenda kwa waganga, ni unaonyesha kuwa humuhitaji Roho Mtakatifu kukusaidia, na kazi ya Roho Mtakatifu ni kuwavuta watu kwa Mungu, na kuwapa macho ya rohoni, Hivyo unapojihusisha na ushirikina na uchawi, ni kuwa unapoteza huo uwezo, na matokeo yake unakufa kiroho.. Hapo ndipo unaanza kufanya hata yale mambo ambayo mwanadamu wa kawaida hawezi kufanya,..Hayo unaweza usiyaone leo, lakini kwa jinsi siku zitakavyozidi kwenda mabadiliko hayo utayaona, kwasababu nguvu za giza wakati huo zitakuwa zinakutawala.

2Wakorintho 4:4 “ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu”.

 

  1. Ukifa unakwenda motoni.

Washirikina wote, wachawi wote, biblia inasema sehemu yao ni katika lile ziwa la moto. Ukifa leo na upo katika hali hiyo , basi ni moto wa milele unakuongoja.

Ufunuo 21:8 “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili”.

 

Sasa kwanini hayo yote yakukute?

Lakini Habari njema ni kuwa, hata kama umeingia huko, bado unayo nafasi ya kutengenezwa upya. Na anayeweza kufanya hivyo, si mwingine zaidi ya YESU KRISTO tu peke yake..Huyo ndiye aliyetiwa mafuta na Mungu, ili kuwatoa watu katika vifungo vya giza, mwingine yeyote hawezi….

Isaya 61:1 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.

Hivyo kama ulishaingia humo, au bado hujaingia, lakini Kristo bado hayupo ndani yako, basi leo hii fanya uamuzi huo, wa kumkaribisha ndani yako ayaokoe maisha yako moja kwa moja, haijalishi wewe ni muislamu, Yesu anawaokoa wote, wanaomkimbilia yeye kwa moyo wa dhati.

Akikuweka huru, amekuweka huru kweli kweli, haachi hata alama ya uovu ndani yako, akikusamehe amekusamehe kweli kweli, kana kwamba hukuwahi kumkosea, kwa lolote. Atakufungua kutoka katika malango hayo ya mauti ya ibilisi yaliyokufunga, na kukuletea katika ufalme wa wana wa Mungu. Roho Mtakatifu akiingia ndani yako, hakuna pepo lolote litakaloweza kukaa ndani yako, Ukimkaribisha leo hii atakufanya huru, na kuna amani itaingia ndani mwako, ambayo utashangaa imetoka wapi..Huyo ndio Yesu mwokozi.

Hivyo kama upo tayari leo hii kutubu dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kuacha, na kusema kuanzia sasa namfuata Yesu, sitaki ushirikina, sitaki dhambi, Namfanya Yesu kuwa kiongozi wa maisha yangu basi uamuzi huo ni mzuri na wa busara, basi, fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala fupi ya Toba..>>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Ubarikiwe sana.

Mada Nyinginezo:

NINI KINATOKEA BAADA YA KIFO?

EPUKA MUHURI WA SHETANI

JINSI WATU WANAVYOZAMA KATIKA USHIRIKINA NA UCHAWI.

JE NI KWELI MTU ANAWEZA KUTOKA NJE YA MWILI WAKE?.

MAONO YA NABII AMOSI.

DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator