JE NI KWELI MTU ANAWEZA KUTOKA NJE YA MWILI WAKE?.

JE NI KWELI MTU ANAWEZA KUTOKA NJE YA MWILI WAKE?.

Inawezekana mtu kutoka nje ya mwili?

Ipo Imani ya kwamba mtu anaweza kutoka nje ya mwili wake au kwa lugha nyingine inajulikana kama Astral projection. Ni kwamba mtu kwa mapenzi yake mwenyewe sio kwa kuhimizwa na nguvu nyingine tofauti na yake labda tuseme ya Mungu au shetani hapana, bali yeye mwenyewe anao uwezo wa kujiamulia kutoka nje ya mwili wake, na kusafiri na kwenda mbali, mahali popote anapotaka na kurudi.

Ni ukweli usiopingika kuwa imani hii siku za hivi karibuni imezidi kushamiri sana, wanasema kitendo hicho salama mtu yeyote anaweza kufanya hata akiwa tu chumbani kwake, kinachohitajika tu ni utulivu wa akili wa hali ya juu sana, yaani kuulazimisha ubongo ukae katika hali ya kutowaza kitu chochote kwa muda fulani, na kuhakikisha pia hakuna hofu yoyote moyoni.

Pia mwili uwe katika utulivu na hiyo inaweza ikafanyika aidha mtu akiwa amelala kitandani mwake chali, huku anaangalia juu. Au ameketi katika chumba chake chenye utulivu mkubwa sana, na kuweka kitu chochote mbele yake aidha mshumaa unaowaka, au akaweka mlio Fulani wa chini wa dansi , huku anapumua taratibu sana, na kukitazama bila kuhamisha mawazo yake mahali pengine popote. Hiyo inafanywa sana sana na dini za huko ASIA kama vile wahindu, na Wabuddha, kama ulishawahi kusikia kitu kinachoitwa YOGA, nayo ni njia mojawapo mafunzo ya kutoka nje ya mwili (Astral projection).

Imani ya Yoga/Astral projection.

Wanasema mtu yeyote ambaye anaweza kufikia hatua hiyo basi atajiona kidogo kidogo roho yake inaachana na mwili wake. Na baadaye kabisa atatoka na kuuona mwili wake umeketi pale chini au umelala pale pale kitandani alipokuwa. Hivyo kuanzia hapo anaweza kutembea mahali popote anapoweza kwenda. Anaweza kuzunguka maeneo ya uwani, anaweza akapaa, anaweza kuenda sehemu ambazo hajawahi kufika kabisa..Na baadaye anaweza akarudi tena katika mwili wak,.

Wanasema kitendo hicho cha kutoka nje ya mwili(Astral projection) hakina madhara yoyote, kwanza ni kizuri kinamfanya mtu ajiamini, pili kinamfanya mtu aburudike. Na tatu kinamfanya mtu akue kiroho, na nne kinamfanya awe na afya njema..

Lakini Je! Imani hiyo ni sahihi au Inapotosha?

Kwanza jambo la kwanza ambalo tunapaswa kufahamu ni kuwa ni kweli kabisa mtu anaweza akatoka nje ya mwili wake..Lakini sio kwa matakwa yake mwenyewe au kwa mapenzi yake mwenyewe..Sisi wanadamu Mungu alivyotuumba hakutupa uwezo huo, alituumba katika mwili, hivyo uwezo wa kuingia katika Roho na kwenda nje haiwezekani kama mtu hatawezeshwa na nguvu Fulani inayotoka rohoni. Na nguvu hiyo ni aidha inatoka kwa Mungu au kwa Shetani, basi hakuna hapo katikati.

Tukianzana na Nguvu ya Mungu,.

Tunasoma katika maandiko Mtume Paulo anashuhudia na kusema alinyakuliwa na kupelewa hadi mbingu ya tatu(Sasa huko kunyakuliwa ndio kutoka nje ya mwili), akasema alipofika huko alionyeshwa mambo ambayo hayajuzu mwanadamu kuyanena..

2Wakorintho 12.:1 “Sina budi kujisifu, ijapokuwa haipendezi; lakini nitafikilia maono na mafunuo ya Bwana.

2 Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu.

3 Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua);

4 ya kuwa alinyakuliwa mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwanadamu ayanene.”

Unaona Maneno haya yanathibitisha kweli kuwa mwanadamu anaweza kutoka nje ya mwili wake, jambo hilo hilo linaonekana pia kwa mtume Yohana alipokuwa katika kile kisiwa cha Patmo, naye alikuwa katika Roho.

Na hata leo hii Mungu anaweza kutoa watu na huwa anawatoa katika mwili na kuwapeleka sehemu nyingine kuwaonyesha mambo ya rohoni, hilo linawezekana lakini haliji kwa jinsi mtu anavyotaka yeye. Bali kwa jinsi Mungu anavyotaka yeye, hata kama mtu huyo ni nabii kiasi gani, au anayo mahusiano gani na Mungu, hajiamulii mwenyewe sasa nataka nione maono. Au nataka niingie katika roho, ni Mungu mwenyewe ndio anayepanga na inakuja kwa wakati asioutegemea.

Sasa Tukirudi katika upande wa pili wa nguvu za giza(Shetani).

Ni kwamba, pale mtu anapotaka kujaribu kutafuta au kujiingiza katika maarifa ya rohoni kwa matakwa yake mwenyewe. Hapo ndipo shetani anapopata mlango kirahisi wa kumwingia mtu huyo na kumdanganya..Kama ulikuwa hujui hivyo ndivyo watu wanavyozama katika uchawi na ushirikina,..

Zipo shuhuda nyingi sana siwezi kukuelezea zote hapa, na kama wewe ni msomaji mzuri wa vitabu nakuomba usome kitabu hichi ambacho kilipata umaarufu mkubwa duniani, na kimewasaidia watu wengi sana ambao walikuwa wamezama katika vifungo vya namna hiyo vya shetani na kutoka kinavyomweleza dada mmoja aliyeingia katika uchawi na kuwa malkia wa kuzimu na baadaye kukombolewa na Kristo.

Na kufunua njia zote na milango yote ambayo shetani anayoitumia kuwavuta watu wengi kwake..Kitabu hicho kipo katika lugha ya kiingereza kinaitwa, HE CAME TO SET THE CAPTIVES FREE. Ikiwa utakihitaji utaniambia nikutumie kwa njia ya email kwa mfumo wa pdf Ukisome, moja ya mambo anayoeleza huko ni pamoja na kuwaonya watu wasifanye hivyo kabisa (Astral Projection).

Na zipo shuhuda nyingi. Lakini hicho ni kizuri Zaidi.

Leo hii hata katika maeneo ya michezo na mazoezi (GYM). Wanafundishwa kufanya hivyo na kudai kuwa ni sehemu ya afya ya ubongo kufanya YOGA. Wanasema ukiweza kukaa katika hali hiyo bila kufikiria chochote au kuwaza chochote katika utulivu wa hali hiyo ya juu kwa muda mfupi tu hata wa nusu saa ni zaidi ya kupumzika kwa kulala usingizi. Nataka nikuambie usijaribu kufanya hivyo. Kwani shetani hapo ndipo anapopata upenyo kwa kupitia milango ya fahamu zako kukuteka na kukutoa katika mwili, na siku za mwanzoni utajiona kweli ni kama wewe unafanya lakini kumbe hujui tayari ni Pepo limekuchukua katika roho linakuzungusha. Unakuwa huna tofauti na mchawi anasafiri kwa ungo kutoka mji mmoja hadi mwingine kwa nusu saa.

Na kwa kuwa siku ya kwanza utapenda, kesho tena utataka ujaribu, na huko huko utakutana na mambo ya ajabu na nguvu za giza ambazo zitakupa maagizo zaidi ya kufanya ili uwe na uwezo huu au uwezo ule, na mwisho wa siku unajikuta umezama moja kwa moja katika uchawi wa hali ya juu.

Kumbuka mlango mmoja unafungua mwingine..

Kwamwe usikae umfungulie shetani mlango kama huo ukadhani unajaribu tu. Ukifanya hivyo ndio umepotea moja kwa moja…Na waganga wa kienyeji nao wanatoaga hayo masharti.

Shetani sikuzote anajua wanadamu wanapenda maarifa Fulani zaidi wa hayo waliyowekewa, hivyo anakuja na kitu kipya kwasababu anajua wakisikia hivyo watavutiwa nacho, ndicho alichofanya pale Edeni kumwambia Hawa Ati hivi ndivyo Mungu alivyosema, ukila matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya mtakufa?..Hakika hamtakufa kwasababu anajua siku mtakapokula MTAFUMBULIWA MACHO..

Vivyo hivyo leo hii anawaambia watu ukitoka nje ya mwili wako, basi utakuwa unajua kila kitu. Utakuwa unaweza kujiamrisha mwenyewe na kuongoza roho yako kwa jinsi unavyotaka..Lakini walioingia huko, wanahadhithia wanatamani kutoka lakini ni ngumu shetani kashawateka..

Hivyo epuka ujanja wa shetani. Mtu akikueleza habari hizo, tena mkemee. Dumu katika kulitafakari Neno la Mungu, na kuyatenda mapenzi yake, hiyo inatosha..Hizi ni nyakati za Hatari.

Mungu akubariki.

Tafadhali “Share” Ujumbe huu na kwa wengine.


Mada Nyinginezo:

JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.

DUNIANI MNAYO DHIKI.

LULU YA THAMANI.

NIKUPE WEWE URITHI WA BABA ZANGU?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

17 comments so far

LinusPosted on11:15 mu - Novemba 17, 2022

Naomba unitumie hicho kitabu kweny email yangu

Kingston BoyPosted on10:54 um - Novemba 4, 2022

Asante kwa mafundisho mazuri. Naomba unitumie hicho kitabu kwenye email yangu

PeterPosted on1:34 um - Januari 5, 2021

May god bless you Mr.
Nam nakuomba muongo said,,

AsiyejulikanaPosted on7:57 mu - Oktoba 27, 2020

Ubalikiwe kiongozi kwa elimu ulionayo unaeza ntumia hyo kitabu na mimi nipate kukuza maalifa. abdullauf90@gmail.com

Pagoda benardPosted on1:32 mu - Agosti 22, 2020

Naomba unitumie hicho kitabu mtumishi…
pagodabenard@gmail.com

Wilbert LucasPosted on12:31 mu - Juni 7, 2020

Samahani sana mtumishi, naomba nitumie hicho kitabu kama hutojali

SagumoPosted on10:40 mu - Februari 20, 2020

Nimekuelewa sana mkuu ktk hii mada yako sasa naomba kuuliza kitu kwamba kwnn sasa Mungu nae haangaiki kutafuta watu kama anavyoangaika shetani ikiwa yeye ndie ametuumba na kutuficha maarifa mengine ambayo sisi tulikuwa hatuyajui na shetani ndie anakuja kuyavumbua kuwa kumbe kuna uwezekano wa kufanya ili au lile alafu wakat huohuo ndio anakuteka sasa hebu naomba majibu mkuu
Japo hii topic ni ya muda mm ndio leo nimeipitia tafadhal ushirikiano

  AdminPosted on11:04 um - Februari 21, 2020

  Mungu wetu yupo karibu sana na sisi, kuliko shetani..Na tunayo nafasi ya kumkaribia Mungu zaidi kuliko shetani..Kinachowafanya watu waonekane wengi wapo upande wa shetani ni kwasababu “wao wenyewe wamechagua giza badala ya Nuru”. Yohana 3:19 “Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu”.

  Na kumbuka uamuzi wa mtu kufanya mema au mabaya ni mtu mwenyewe anaufanya na si shetani anamfanyia mtu wala Mungu anamfanyia mtu. Sauti ya Mungu inayomshawishi mtu asiibe, au asiue, au asizini ipo kila mahali hata katika sheria za nchi, lakini sauti ya shetani inayomshiwishi mtu aibe, au aue, au azini huwa inakuja kimaficho…Sasa katika hali kama hiyo mtu akiamua kuitii ile sauti ndani yake ya kimaficho inayomwambia akaibe, au aue..hapo anakuwa mwenyewe kwa hiari yake amelipenda giza zaidi ya Nuru. Lakini kinyume chake kama akiikataa anakuwa kaipenda Nuru zaidi ya giza. Na katika siku hizi za mwisho, biblia imetabiri kuwa watu wengi watalipenda giza zaidi ya Nuru.

  Nimewahi kukutana na mtu ambaye alikuwa anatafuta kujiunga freemasons..nikamweleza kuwa wote watakaojiunga humo watakwenda jehanamu ya moto, akajibu analijua hilo, nikamwuliza je upo tayari kwenda Jehanamu ya moto ya milele? Akajibu ndio yupo tayari..mtu huyu alikuwa anamaanisha kabisa!..Pamoja na kumwambia madhara yote na uongo wote wa kikundi hicho lakini msimamo wake ulikuwa ni ule ule..alipoona nazidi kumweleza habari za Yesu Kristo, Mkuu wa Uzima..alinikimbia..

  Sasa watu walio mfano wa hawa wapo wengi..kwa idhini yao wenyewe wameamua kumtumikia shetani, na huku wanajua madhara yote ya kufanya hivyo…hawa wamependa Nuru zaidi ya giza, Na wanatabiriwa kuwa wengi katika hizi siku za Mwisho..Bwana atusaidie.

  Mkuu wetu Yesu Kristo akubariki.

Leave a Reply