DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.

DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.

Shalom, karibu tujifunze Biblia Neno la Mungu…

Roho Mtakatifu atusaidie leo tena katika kuyatafakari maneno yake.Kama tunavyojua kuwa matukio mengi ambayo yaliwahi kutokea nyakati za kale na kurekodiwa katika biblia…mengi ya matukio hayo ni unabii wa mambo yatakayokuja kutokea baadaye…Kwamfano tunaweza kuona tukio la kugharikishwa dunia wakati wa Nuhu..Bwana Yesu alisema katika siku za mwisho maovu yatakuwa kama yalivyokuwa katika siku za Nuhu..Na kwa namna ile ile gharika ilivyowajia kwa ghafla wakafa wote ndivyo itakavyokuwa katika siku za mwisho wakati watu wanasema kuna amani na salama ndipo hapo hapo uharibifu unapokuja kwa ghafla.

Kadhalika tunaweza kujifunza tukio mojawapo ambalo pia litatupa picha kujua ni nini kitatokea kipindi kifupi kabla kanisa la Kristo kunyakuliwa.

Siku chache kabla ya kuja kwa Bwana Yesu duniani yaani kabla ya kuzaliwa kwake…Shetani alikuwa ameshauona ule ujauzito wa Mariamu hivyo akaanza kutengeneza njia ya kumwondosha Bwana Yesu. Kabla ya kuzaliwa au kipindi kifupi tu baada ya kuzaliwa.

Ghafla tu wazo likamwingia Kaisari ambaye ndiye aliyekuwa mfalme wa dunia nzima…wazo likamwingia aandike orodha ya majina ya watu wote ulimwenguni…Kwa ufupi maana yake ni kwamba kila mtu anapaswa kwenda mjini kwao kuchukua namba ya utambulisho.

Ni wazi kuwa kuna mambo fulani fulani yalitokea duniani wakati huo mpaka yakahimiza sensa hiyo ifanyike..pengine ukusanyaji wa kodi ulikuwa mgumu hivyo ikahitajika kila mtu asajiliwe, au pengine walitaka kutathimini na kudhibiti kiwango cha watu wanaozaliwa duniani.. Au pengine kulitokea watu waovu ambao walikuwa wanavuruga amani, hivyo ili kuwadhibiti ilihitaji sensa kufanyika na kwa kupitia sensa hiyo kila mtu apate kitambulisho chake.

Ni kama leo matapeli wa mitandao wanavyoongezeka inalazimu serikai itoe tamko la kila mtu kusajili laini ya simu yake kwa alama za vidole, ili kuwadhibiti…na kuongeza usalama.

Sasa harakati kama hizi zilianza kipindi kabla hata ya kuzaliwa kwa Bwana Yesu lakini zilifikia kilele kipindi kifupi kabla ya kuzaliwa Bwana Yesu…Watu wote wakapokea namba.

Luka 2:1 ‘Siku zile amri ilitoka kwa Kaisari Augusto ya kwamba iandikwe orodha ya majina ya watu wote wa ulimwengu.

2 Orodha hii ndiyo ya kwanza iliyoandikwa hapo Kirenio alipokuwa liwali wa Shamu.

3 Watu wote wakaenda kuandikwa, kila mtu mjini kwao.

4 Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi;

5 ili aandikwe pamoja na Mariamu mkewe, ambaye amemposa, naye ana mimba.

6 Ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia,

7 akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni”.

Lakini kama wengi wetu tujuavyo…Ndani ya sensa ile kulikuwa na mpango wa Mungu wa Bwana Yesu kwenda kuzaliwa Bethlehemu ili maandiko yatimie…lakini pia kulikuwa na mpango wa Ibilisi mkubwa sana wa kumwangamiza BWANA YESU katika uchanga wake pamoja na mama yake na Baba yake. Alikuwa anasuka mpango wa kwenda kummaliza Bwana Yesu kule mjini kwake Bethlehemu..Ndio maana Herode alitoa tamko la kwenda kutafutwa Bwana Yesu lakini walipomkosa aliagiza watoto wote waliopo Bethlehemu wauawe…Jiulize kwanini si miji mingine yote duniani bali Bethlehemu tu!..shetani naye ana target..hapigi huko na huko ovyo ovyo tu..

Mathayo 2:11 “Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane.

12 Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine.

13 Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize.

14 Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake usiku, akaenda zake Misri;

15 akakaa huko hata alipokufa Herode; ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii, akisema, Kutoka Misri nalimwita mwanangu.

16 Ndipo Herode, alipoona ya kuwa amedhihakiwa na wale mamajusi, alighadhabika sana, akatuma watu akawaua watoto wote wanaume waliokuwako huko Bethlehemu na viungani mwake mwote, tangu wenye miaka miwili na waliopungua, kwa muda ule aliouhakikisha kwa wale mamajusi.

Utajiuliza pia kwanini Bwana Yesu alisema, ole wao wenye mimba na wanyonyeshao siku hizo ?(Mathayo 24:19), Alisema hivyo akifananisha jinsi wanawake wale walivyoshikwa na uchungu wakati wa kuja kwake mara ya kwanza, ndivyo itakavyokuwa katika siku za kuja kwake hata mara ya pili, embu fikiria jinsi watoto wale, walivyokuwa wakichinjwa kama kuku mbele yao, wapendwa wako wanauawa kikatili,..Ni uchungu kiasi gani Na ndivyo itakavyokuwa katika siku za mwisho..

Mathayo 2:17 “Ndipo lilipotimia neno lililonenwa na nabii Yeremia, akisema,

18 Sauti ilisikiwa Rama, Kilio, na maombolezo mengi, Raheli akiwalilia watoto wake, Asikubali kufarijiwa, kwa kuwa hawako”.

Sasa kile kipindi kikikaribia kufikia dalili za watu kuingizwa katika kumbukumbu za mpinga kristo zitaanza…Mpinga-Kristo ataagiza watu wote kwenda kusajiliwa katika mfumo mpya wa kipinga-Kristo ambao huo utahusisha chips, kadi, vitambulisho vipya n.k..Kama vile Kaisari alivyotoa tamko kuandikwa orodha ya majina ya watu wote duniani ..(Na ndani yake kutakuwa na alama ya 666) Kila mtu atakwenda katika mji wake au makazi yake ya kudumu aliyopo kuhakiki taarifa zake kama vile Kaisari alivyotoa agizo la watu wote kwenda kuhesabiwa mjini kwao.

Wakati zoezi hilo lipo mbioni kutendeka hapo katikati unyakuo utatokea… Bwana atakuja mawinguni na kuwachukua walio wake na kuwaepusha na hiyo chapa..kama tu vile Yesu alipotokea duniani, alivyoondoshwa yeye pamoja na Mariamu na Yusufu kutoka Bethlehemu kukimbilia Misri mbali na ghadhabu ya Herode na Kaisari. Na kusababisha wale waliosalia walichinjwa kama kuku..

Mathayo 2:12 “Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine.

Vivyo hivyo wakristo watakaokosa unyakuo, ambao watabaki na kuikataa ile chapa watateswa na mpinga-Kristo kwa dhiki ambayo haijawahi kuwepo tangu kuumbwa ulimwengu. Na Kama tu vile wakati dhiki inaendelea Bethlehemu, inaendelea Yesu pamoja na wazazi wake walikuwepo Misri, Vivyo hivyo wakati dhiki kuu inaendelea, Yesu pamoja na watakatifu wake watakuwa mbinguni.

Je wewe ni familia ya Bwana Yesu Kristo ambaye siku ile utaepushwa na dhiki siku ile na kwenda mbinguni? Kama Mariamu mamaye Yesu na Yusufu walivyoepushwa?…Utauliza nitakuwaje Baba au Mama wa Yesu mimi, na hapo hapo niwe mtoto wa Yesu?

Jibu la swali hilo lipo hapa.

Mathayo 12.46 “Alipokuwa katika kusema na makutano, tazama, mama yake na ndugu zake walikuwa wakisimama nje, wataka kusema naye.

47 Mtu mmoja akamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kusema nawe.

48 Akajibu, akamwambia yule aliyempasha habari, Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni akina nani?

49 Akawanyoshea mkono wanafunzi wake, akasema, Tazama, Mama yangu na ndugu zangu!

50 Kwa maana ye yote atakayeyafanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu”.

Je unafanya mapenzi ya Bwana Yesu? Au mapenzi ya shetani…mfano wa mapenzi ya shetani ni haya ulevi, uasherati, uzinzi, ufiraji, ulawiti,utoaji mimba, kujichua, kutazama picha za ngono mitandaoni, uabuduji sanamu, wizi, ulaji rushwa, usengenyaji n.k Biblia imetabiri watu wa namna hii hawataikwepa dhiki kuu…labda wawe wamekufa kabla ya hiyo siku kufika..lakini pia hata huko walipo hawapo sehemu salama…Hivyo suluhisho ni kukubali kubadili mtindo wa maisha yetu.

Kama hujaokoka okoka leo usisubiri kesho..Huwa Adui shetani akishaona umeujua ukweli kama huu unaousoma leo na akishaona unashawishika kumgeukia Kristo, anaweza hata akakusababishia kifo cha ghafla ili tu ufe ukiwa hujaokoka…hivyo usipuuzie habari njema za Yesu zinapoletwa mbele yako ambazo hutozwi hata senti kuzisikiliza unapewa bure kabisa…Jiulize ukifa leo utakuwa wapi? Jibu unalo matumaini yangu ni utamgeukia Kristo leo.

Bwana akubariki sana.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii 0789001312

Mada Nyinginezo:

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

MTINI, WENYE MAJANI.

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

UNYAKUO.

MPINGA-KRISTO

Mungu anasema hatagharikisha dunia na maji tena,.Kwanini watu wanasema dunia itaangamizwa?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Michael Mutuku
Michael Mutuku
1 year ago

Kwanza kabisa,namshukuru Mungu kwa wema wake na fadhili zake.
Jambo la pili,Nawashukuru kwa mafundisho mazuri.
Mungu awabarki na awape hekima zaidi,na awatimizie ndoto zenu,maono yenu na malengo yenu,
Mwisho,nitaendelea kusoma haya mafundisho,hata ingawa wakati mwingine era za kununua mjazo sinakosekana,lakini kwa imani nitazidi kusoma na ninaomba Mungu na mimi nifundishe wengine kupitia haya mafundisho.God bless you all AMEN.