MTINI, WENYE MAJANI.

MTINI, WENYE MAJANI.

Mtini, wenye majani ni upi?

Jina kuu la mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe. Karibu tujifunze Neno la Mungu, Na leo tutajifunza somo lenye kichwa kinachosema “MTINI, WENYE MAJANI”..Unaweza usielewe kichwa hichi kina maana gani lakini twende pamoja mpaka mwisho naamini lipo jambo kubwa utajifunza.

Tunaona siku moja kabla Bwana Yesu kwenda kukaa na wanafunzi wake katika mlima wa mizetuni ili kuwaeleza habari za siku za mwisho, kuna jambo la kustaajabisha kidogo alilifanya mbele ya macho yako kwa makusudi kabisa..Na alifanya hivyo ili kuja kuwafundisha somo Fulani kesho yake..Na jambo lenyewe ni lile la “kuulaani mtini”

Akiwa anatoka Bethani asubuhi ili aende Yerusalemu hekaluni kufundisha alikutana na mtini njiani,(Mtini ni mti unaotoa matunda ya Tini) Embu tusome alichokifanya:..

Marko 11:12 “Hata asubuhi yake walipotoka Bethania aliona njaa.

13 Akaona kwa mbali mtini wenye majani, akaenda ili labda aone kitu juu yake; na alipoufikilia hakuona kitu ila majani; maana si wakati wa tini.

14 Akajibu, akauambia, Tangu leo hata milele mtu asile matunda kwako. Wanafunzi wake wakasikia”.

Mtini ni nini.

Mtini ni mti unaozaa matunda yanayoitwa TINI. Mti huu unastawi sana maeneo ya mashariki ya kati.

Sasa ukisoma juu juu unaweza kuona kama vile Bwana Yesu alikuwa hajui kuwa ule sio wakati wa TINI,.. na ndio maana akaulaani ule mtini kimakosa alipokosa matunda juu yake..Lakini alilifahamu hilo vizuri tutakuja kuona ni kwa namna gani hapo mbeleni kwa jinsi tunavyozidi kusoma. Lakini Kinyume chake alifanya vile kwa makusudi ili kuja kuwafundisha wanafunzi wake somo.. ambalo sisi watu kizazi hichi cha siku za mwisho ndio tunalolielewa vizuri..

Tukirudi kwenye ile Mathayo 24 yote, Bwana Yesu sasa akiwa na mitume wake pale katika Mlima wa mizeituni alianza kwa kuwaeleza dalili kuu za siku za mwisho,.. kwamba kutatokea manabii wa uongo na makristo wa uongo, kutakuwa na vita na habari za matetesi ya vita,kutaongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa, kutasimama chukizo la uharibifu, upendo wa wengi utapoa, habari njema ya ufalme itahubiriwa katika mataifa yote n.k.

Na karibu na pale mwisho kabisa akawaambia maneno haya kwa kuwakumbusha kilichotokea nyuma:

Mathayo 24:32 “Basi kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu;

33 nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni.

34 Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia.

35 Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe”.

Sasa embu tafakari vizuri tena kwa ukaribu pale anaposema, “tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu;”…Kumbe alijua mtini unapofikia hatua ya kuchipua, na matawi yake kuonekana basi wakati wake wa mavuno unakuwa upo karibu sana…Kumbe alilitambua hilo hata kwa ule mtini wa kwanza alioulaani, kwasababu ule ulikuwa katika hatua hiyo hiyo ya majani, lakini aliulaani usifikie hatua ya kufikia mavuno kwa haraka,, bali wa muda mrefu sana mbeleni alioufananisha na milele..

Inafunua nini?

Hii dunia ungekuta imeshakwisha tangu zamani za mitume, lakini Bwana YESU aliuvuta muda wa mavuno mbele ili zile dalili za mwisho wa dunia zisionekane kwa kipindi kile walichokuwa wanaishi…aliyakawiisha mavuno kwa mfano wa ule mtini alivyoukawiisha.

Kwasababu kumbuka MTINI huwa unapitia hatua kuu tatu,.. ya kwanza kupukutisha majani yake yote, ya pili ni kuchipua majani, na ya tatu ni kuzaa matunda…Sasa ile hatua ya kupukitisha, huwa unapukutisha majani yake kweli kweli na kuwa kama kijiti kikavu kilichonyauka… soma..

Ufunuo 6:12 “Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu,

13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi”.

Unaona hapo? Biblia inatoa picha jinsi nyota za mbinguni zitakavyoanguka katika siku za mwisho mfano wa mtini unavyopukutisha mapooza (majani makavu) yake.

Sasa kwasababu Bwana Yesu aliukawiisha wakati wa mavuno ndio tunaweza kuona tangu kipindi kile cha mitume hadi zaidi ya miaka elfu mbeleni,..hakukuwa na dalili za wazi zinazothibitisha kuwa mwisho upo karibu, kwa yale aliyoyazungumza katika Mathayo 24 kwamba manabii wa uongo watatokea, taifa kuondoka kwenda kupigana na taifa hayo hayakuwepo,… lakini tunaona kuanzia karne ya 20 yaani kuanzia mwaka 1900, mambo hayo yalianza kuonekana kwa kasi, vita kuu mbili za dunia zimepiganwa kwa mpigo ndani yah ii karne.., magonjwa ya kutisha ambayo hayakuwepo enzi za nyuma, yameonekana kwa kasi kuanzia karne ya 20, magonjwa ya ajabu yamezuka na bado yanaendelea kuzuka, kansa, ukimwi, ebola, zika, n.k…

Dalili zote zimetia:

Na dalili zile alizozingumzia pale zimeendelea kutimia kwa kasi, hadi sasa, mambo yote yameshatimia hususani katika hii karne ya 21 tuliyopo sasahivi.. karibu yote yameshatimia..

Hapo ndipo tunapojua sasa, wakati wa mavuno umeshafika..Ule mtini wa mwisho wa dunia umeshafikia hatua ya mavuno yake, matawi yake tunayaona…Wimbi kubwa la manabii wa uongo tunaloliona leo hii ungemweleza mtu wa mwaka wa 1980, angekushangaa na kusema hicho kitu hakiwezekani,.. lakini tazama hali ilivyo sasa, sodoma iliyopo sasa hivi duniani, ni zaidi ya ile ya Gomora..pornography mitandaoni, watu wanafanya uasherati na wanyama, simu za mikononi zimekuwa shimo refu la kuelekezea watu kuzimu n.k..Hii yote ni kutuonyesha kuwa Mtini umeshachipua..

Sasa Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake..mnyaonapo hayo CHANGAMKENI, mkaviinue vichwa vyenu, kwa kuwa ukombozi wenu umekaribia.”..(Luka 21:28)

Unyakuo wakati wowote utapita. Wale waliookolewa wanapaswa wafurahie kwasababu siku yoyote tutakuwa utukufuni, Lakini wewe ambaye upo dhambini Je! Wewe ambaye unautazama ulimwengu utakuwa wapi?… Mkimbilie Kristo ndani ya hichi kipindi kifupi tulichobakiwa nacho, acha kupoteza muda, ulimwengu haukujali kama unavyofikiria wewe…Tubu dhambi zako mgeukie Mungu, naye atakupokea, na kukupa Roho wake Makatifu bure,..Unasubiri nini?.

Fanya hivyo sasa hapo uliopo piga magoti utubu, na yeye anakusikia na yupo tayari kukusamehe bure bila gharama yoyote.., kisha baada ya hapo anza kutafuta ushirika na wakristo wenzako, tupa kila nguo mbaya yoyote uliyokuwa unavaa, vimini, suruali, ma-lipstik, acha matendo yote mabaya uliyokuwa unafanya..ili kumthibitishia Mungu kweli umeamua kutubu na kumgeukia yeye..Na yeye akishaona Imani yako na Nia yako kweli umeamua kugeuka…Hiyo tayari ni sababu tosha ya yeye kukupa Roho wake Mtakatifu… atakuvika uwezo wa ajabu ambao utakusaidia kuviondoa vile vilivyosalia..

Fanya hivyo na Bwana atakubariki..Kumbuka tena.. Tunaishi katika majira ya kuchipuka kwa mtini, hivyo mavuno yapo karibu ..

Bwana akubariki.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

 

Shalom.

Mada Nyinginezo:

USISIKILIZE DHIHAKA ZA SHETANI, ZITAKUKWAMISHA.

NAMNA YA KUMTAMBUA BIBI ARUSI WA KWELI WA KRISTO.

HATUTAACHA KUJIFUNZA NENO KILA INAPOITWA LEO.

YUDA ISKARIOTE! MTUME ALIYECHAGULIWA NA BWANA YESU.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Sephania
Sephania
1 year ago

AMINA

Anonymous
Anonymous
2 years ago

amen