Bwana Yesu alikuwa na wanafunzi wengi, lakini alikuwa na Mitume 12 tu! Matume hawa 12 wote walichaguliwa kwa ufunuo wa Roho, kwani tunasoma kwamba Bwana kabla ya kuwachagua mitume hao alikwenda kuomba kwanza, ndipo akafunuliwa majina ya mitume hao.
Lakini jambo la kushangaza kidogo ni kwamba miongoni mwa hao mitume 12, alikuwemo mtume mmoja wa Uongo, ambaye aliitwa Yuda Iskariote. Sasa swali linakuja? kwanini Roho Mtakatifu amchague Mtume wa Uongo katikati ya mitume wa ukweli?..Ukitafakari hilo kwa makini kama ni mtu wa kufikiri mambo litakuogopesha kidogo!..Roho Mtakatifu anawapaka mafuta mitume wa uongo na kuwatuma?..Maana Yuda naye alikuwa anatumwa kuhubiri na kutoa pepo kama mitume wengine wote..Na Bwana alimpenda tu kama alivyowapenda mitume wengine…Na bila shaka endapo watu wangemwuliza Bwana eti huyu Yuda naye ni mwanafunzi wako? Ni wazi kuwa angejibu ndio! Asingemkana kwasababu ni yeye ndiye aliyemchagua.
Na ni wazi kuwa mahali pa siri ambapo Bwana alikuwa anakaa, mahali ambapo haruhusu watu wengine kufika isipokuwa mitume wake tu angemruhusu Yuda..Kwahiyo kwa ufupi ni kwamba upendeleo wote ambao Mitume wa kweli walikuwa wanaupata Yuda naye alishiriki.
Na cha ajabu ni kwamba Yuda Iskariote mwenyewe ambaye ni mtume wa Uongo, hakuna aliyekuwa anamjua kuwa ni mtume wa uongo, isipokuwa Bwana Yesu tu peke yake! Hata mitume wenzake walikuwa hawajui!..Ndio maana utaona wakati Bwana anawaambia mmoja wao atamsaliti…wale mitume 11, walishindwa hata kumhisi kuwa ni Yuda, walijihisi ni wao, kila mmoja alijidhania ni yeye!…ikionesha ni jinsi gani Yuda ilikuwa ni ngumu kumgundua.
Marko 14:18 “Nao walipokuwa wameketi chakulani, wakila, Yesu alisema, Amin, nawaambia, Mmoja wenu, naye anakula pamoja nami, atanisaliti. 19 Wakaanza kuhuzunika, wakamwambia mmoja mmoja, Je! Ni mimi?”
Marko 14:18 “Nao walipokuwa wameketi chakulani, wakila, Yesu alisema, Amin, nawaambia, Mmoja wenu, naye anakula pamoja nami, atanisaliti.
19 Wakaanza kuhuzunika, wakamwambia mmoja mmoja, Je! Ni mimi?”
Yohana 17:12 “Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie”.
Ni andiko gani hilo ili litimie? Ni hili:
Yohana 13:18 “Sisemi habari za ninyi nyote; nawajua wale niliowachagua; lakini andiko lipate kutimizwa, ALIYEKULA CHAKULA CHANGU AMENIINULIA KISIGINO CHAKE”.
Unabii huo uliandikwa katika kitabu cha Zaburi 41: 9 “Msiri wangu tena niliyemtumaini, Aliyekula chakula changu, Ameniinulia kisigino chake”.
Yuda akamwinulia kisigino Bwana, akamsaliti kwa vipande 30 vya fedha…akasema
Mathayo 26:14 “Wakati huo mmoja wa wale Thenashara, jina lake Yuda Iskariote, aliwaendea wakuu wa makuhani, 15 akasema, Ni nini mtakachonipa, nami nitamsaliti kwenu? Wakampimia vipande thelathini vya fedha.”
Mathayo 26:14 “Wakati huo mmoja wa wale Thenashara, jina lake Yuda Iskariote, aliwaendea wakuu wa makuhani,
15 akasema, Ni nini mtakachonipa, nami nitamsaliti kwenu? Wakampimia vipande thelathini vya fedha.”
Na Mitume hawa wauongo wapo katika hizi siku za mwisho ili kutimiza hili andiko ! Kazi yao ni kumgeuzia Bwana kisigino na kumwuza kwa vipande vya fedha!..wanawafuata watu na kuwaambia mna shilingi ngapi niwapatie Maji ya Upako?….kama Yuda alivyofanya..badala ya kwenda kuwahubiria wakuu wa makuhani watubu dhambi zao, na kumwamini Yesu, yeye anakwenda kuwahubiria injili ya kuwauzia Yesu..Mfano dhahiri wa mitume na manabii wa uongo wa leo…wanawahubiria watu injili za kumwuza Yesu, una shilingi ngapi nikutolee pepo, una shilingi ngapi nikupe maji ya upako, unashilingi ngapi nije kufanya maombi ya ufumbuzi nyumbani kwako n.k?
Ndugu, epuka injii ya Yuda Iskariote, ya mafanikio kila kukicha? Jiangalie tangu umeanza kutumia hayo maji, mafuta ni nini umenufaika katika roho yako?..Kama umeona yamekusaidia kuacha dhambi, kuacha usengenyaji, kuacha rushwa, kuacha wizi, kuacha matusi, kusamehe, kuacha uasherati basi yatumie lakini kama umeyatumia na hali yako ya kiroho ipo vile vile basi fahamu kuwa Umeuziwa Bwana Yesu kama Yuda alivyowauzia mafarisayo…na wewe umemnunua kwa dhumuni la kwenda kumsaliti na kumsulibisha mara ya pili kutokana na dhambi zako.
Ikiwa hujampa Yesu Kristo maisha yako na unataka kufanya hivyo bado hujachelewa, hapo ulipo, tubu kwa kudhamiria kuacha dhambi zako zote na kisha tafuta mahali ukabatizwe kama hujabatizwa, kumbuka ubatizo sahihi ni ule wa kuzama mwili wote na kwa jina la Yesu Kristo kulingana na Matendo 2:38, na Bwana mwenyewe atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu, na baada ya hapo hakikisha unadumu katika kujifunza Neno la Mungu, katika kusali, na kufanya ushirika na wakristo wengine kanisani, kama tulivyoagizwa katika Matendo 2:42
Shalom! jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
Naomba kujua watakaoenda mbinguni je! ni wengi au wachache?
Nifanyaje ili nijue kuwa uamuzi ninaokwenda kuchagua kufanya ni mapenzi ya Mungu?
FREEMASONS NI NINI? NA MTU ATATOKAJE HUKO?
KUWA MAKINI NA MITANDAO, NI SHIMO REFU.
Rudi Nyumbani:
Print this post
Shalom mtumishi? Hapo nimeweza kujua au kufahamu Jambo kumbwa Sana kuhusu utumiaji mbaya WA NENO la MUNGU,Kwa kuwa mtu atakwambia kuwa maandiko yanasema!! Nawewe pasipo kujua au kufikiri NI Kwa namna GANI mambo yanavyokuwa,unakimbililia KUMBE ndio kuanguka kwakundanganywa, ASANTE SANA MTUMISHI WA MUNGU na MUNGU MWENYENZI AKUMBALIKI Amina.
Amen BWANA YESU azidi kutubariki sote ndugu yetu…
Amen..azidi kukubariki nawe pia ndugu yetu
somo hili limenijibu swali langu , maana nilikuwa najiuliza inakuwaje mtu awaponye watu kwa jina la KRISTO halafu kumbe si wake. Mungu wa mbinguni awatie nguvu na kuwabariki zaidi