KAMA MUNGU ANABORESHA KAZI ZAKE, KWANINI WEWE USIBORESHE ZA KWAKO?.

KAMA MUNGU ANABORESHA KAZI ZAKE, KWANINI WEWE USIBORESHE ZA KWAKO?.

Shalom, mtu wa Mungu, Biblia inasema mtu hataishi kwa mkate tuu, bali kwa kila Neno litokalo katika kinywa cha Bwana, hivyo pale tunapojifunza Neno la Mungu kwa dhati tuwe na uhakika kuwa Roho zetu zinanenepa na hivyo kujiongezea siku za kuishi hapa duniani (1Wafalme 3:14)..

UUMBAJI WA MUNGU

Tukisoma kitabu cha Mwanzo sura ya kwanza tunaona jinsi Bwana alivyofanya kazi yake ya kuumba ulimwengu kwa siku 6, na ilipofika siku ya 7 aliacha kazi zake zote akastarehe, tena akaibariki siku hiyo kuonyesha kuwa kila kitu kimekamilika, Vile vile ukisoma sura ya pili utaona jinsi Bwana anavyompa Adamu maagizo ya kuishi katika bustani ile, akamletea na Wanyama wote awape majina, naye akafanya hivyo, basi Maisha ya Adamu na viumbe vyake vyote yakaendelea hivyo siku zinakuja siku zinakwenda..

Lakini kilipita kipindi Mungu akamtazama Adamu akasema neno hili “SI VEMA”..Tunasoma hilo katika..

Mwanzo 2:18 “Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye”

Embu jaribu kufikiria mtu akisema Neno “si vema” anaashiria nini?, Ni wazi kuwa atakuwa ameona mapungufu, na hivyo anahitaji kufanya marekebisho fulani ili mambo yaende kama anavyotaka..

Ndivyo ilivyokuwa kwa Mungu, japo alikuwa tayari ameshamuumba mwanamke katika mawazo yake tangu siku nyingi, ukisoma Mwanzo 1:27-28 utalithibitisha hilo, Mwanamke alikuwa tayari kashaumbwa kabla hata ya uumbaji wenyewe kuanza, lakini Mungu aliruhusu kwa makusudi kabisa asitokee katika uumbaji ule wa mwanzo alipokuwa anamuumba Adamu na viumbe vyake vyote, kana kwamba alisahau hivi, ili tu alitumie hili neno SI VEMA, kutufundisha sisi jambo..

Mwanamke alikuja kuumba baadaye kabisa, Maisha yameshaendelea edeni kwa kipindi fulani pengine cha mwaka 1 au 10 au 100 hatujui, lakini mwanamke siku alipokuja kuumbwa, uumbaji ulikuwa umeshamalizika siku nyingi sana huko nyuma.

MUNGU ALIFANYA MAREKEBISHO

Kwanini Mungu alifanya hivyo? ni kwasababu alikuwa anatufundisha kuwa yeye anapendezwa na marekebisho, embu jaribu kufikiria marekebisho yake yake jinsi yalivyo na manufaa makubwa kwetu sisi leo hii, jaribu kuwazi hii dunia mfano isingekuwa na wanawake tungeishije ishije huku duniani, mfano usingeupata upendo wa mama leo hii wewe ungekuwaje, usingeupata upendo wa dada leo hii wewe ungekuwaje, usingeuonja upendo wa mke leo hii wewe mwanamume ungekuwa mtu wa namna gani? N.k, hakuna mnyama yeyote au kiumbe chochote kingeweza kukupa faraja duniani kama sio mwanamke..

Tunamshukuru Mungu kwa kutupa zawadi hii, lakini hiyo yote ni kutokana na marekebisho, kama Mungu angesema mimi nimeshamaliza uumbaji wangu, na siku ya 7 nimeshastarehe, hichi tunachokiona leo hii kisingekuwepo?.

Vivyo hivyo na sisi Mungu anatarajia tuwe tunafanya marekebisho katika ukristo wetu, katika huduma zetu za kuujenga ufalme wa mbinguni, tusione haya kusema SI VEMA…Mungu asiyeweza kukosea alisema hivyo wewe kwanini uone kila kitu kipo vyema?. Kwanini uridhike na ukristo ule ule ambao ulikuwa nao miaka 10 iliyopita, hadi leo unaendelea nao, na huku unaona kabisa unayo mapungufu mengi ndani yako ya kufanyiwa marekebisho?

JENGA UFALME WA MUNGU

Kazi ya Mungu inalala, miundo mbinu ya kanisa kila siku inaporomoka, kwanini usiseme SI VEMA hichi kiwe vile, au kile kiwe vile? Natoa mchango wangu wa fedha, au nguvu zangu kupakarabati hapa, au akili uzoefu wangu kufanikisha kile…Mungu anata tuwe hivyo..Unajuaje kuwa hicho unachokirekebisha kitakuwa na manufaa makubwa ya kuleta maelfu wa watu wa Kristo, kama vile mwanamke alivyo na manufaa makubwa sana leo hii kuleta roho nyingi za watu duniani?.

Ukiona umeokoka na muda mrefu upo vilevile, huongezi kiwango chako cha kusali huongezi kiwango chako cha kuwapelekea wengine injili, huongezi kiwango chako cha kufunga, basi ujue umeshatoka nje ya kusudi la Mungu alilotaka wewe uliendee…Tunapaswa tukue toka Imani, hadi Imani, toka utukufu hadi utukufu,..lakini tukiona kila kitu kipo sawa tu ndani yetu, tumeridhika basi tunajidanganya wenyewe.

Ni maombi yangu mimi na wewe, tutaanza kujifunza kusema SI VEMA, Na kuanzia leo kwa msaada wa Bwana tutahakikisha tunaboresha Maisha yetu ya rohoni pamoja na hudumu za kuipeleka injili.

Amen.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Tafadhali “Share” Ujumbe huu na kwa wengine, kama umeona pia SI VEMA, ushiriki baraka hizi peke yako.


Mada Nyinginezo:

KUWA MAKINI NA MITANDAO, NI SHIMO REFU.

KUOTA UMEPOTEA.

JE KUJIUA NI DHAMBI?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments