Mpumbavu ni nani katika biblia? (Zaburi 14:1, Mithali 10:14)

Mpumbavu ni nani katika biblia? (Zaburi 14:1, Mithali 10:14)

Katika kitabu cha Zaburi na Mithali Neno mpumbavu linatajwa sana, naomba kufahamu mpumbavu ni mtu wa namna gani kibiblia?


Biblia haielezi moja kwa moja maana ya mpumbavu, bali inaeleza tabia zinazoambatana  na mtu mpumbavu, embu tupitie baadhi ya vifungu vinavyolizungumzia neno hilo na mwisho kabisa hivyo ndivyo vitakavyotusaidia kujua mpumbavu ni mtu wa nanma gani;

Zaburi 14:1 “Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema”.

Mithali 10:8 “Aliye na akili moyoni mwake atapokea agizo; Bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataanguka”.

Mithali 9:13 “Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu”.

Mithali 10:14 “Watu wenye akili huweka akiba ya maarifa; Bali kinywa cha mpumbavu ni uangamivu ulio karibu”.

Mithali 10:23 “Kwa mpumbavu kutenda maovu ni kama mchezo; Bali mtu mwenye ufahamu ana hekima”.

Mithali 12:15 “Njia ya mpumbavu imenyoka machoni pake mwenyewe; Bali yeye aliye na hekima husikiliza shauri”.

Mithali 12:16 “Ghadhabu ya mpumbavu hujulika mara; Bali mtu mwerevu husitiri aibu”.

Mithali 14:1 “Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe”.

Mithali 15:5 “Mpumbavu hudharau kurudiwa na babaye; Bali yeye aangaliaye maonyo hupata busara”.

Mithali 14:16 “Mwenye hekima huogopa, akajitenga na uovu; Bali mpumbavu ana ufidhuli, na kujitumai”.

Mithali 20:3 “Mtu kujitenga na ugomvi ni heshima kwake; Bali kila mpumbavu ataka kugombana”.

Mithali 14:3 “Katika kinywa cha mpumbavu mna fimbo ya kiburi, Bali midomo ya wenye hekima huwahifadhi”.

Mithali 15:20 “Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye; Bali mpumbavu humdharau mamaye”.

Hivi ni baadhi ya vifungu tu, lakini unaweza  kuona mpumbavu ni  mtu anayetajwa kuwa ana dharau, asiye na heshima, anayeropoka ropoka, asimcha Mungu, asiamini hata kama kuna Mungu, asiyetaka kurekebishwa, anayependa ugomvi,  anayesambaza habari za uzushi n.k.

Na tabia zote hizi huwa zinafanya na mtu mwenye dhambi, kwasasa ni mtu ambaye hajakombolewa na Yesu.

Hivyo tafsiri hasaa ya Neno mpumbavu, ni mtu ambaye hajazaliwa mara pili.

Kwahiyo  ikiwa wewe upo nje ya Kristo, haijalishi utakuwa msomi kiasi gani, au utakuwa tajiri kiasi gani, a utakuwa na ushawishi mwingi kiasi gani, wewe ni mpumbavu kibiblia, kwasababu hutakosa tabia mojawapo ya wapumbavu zinayozungumziwa katika biblia.

Ni Yesu pekee ndio mwenye uwezo wa kumgeuza mtu moyo wake na kumfanya kuwa mtu mwingine kabisa. Yeye mwenyewe alisema.. Wote wanaompokea anawapa UWEZO wa kufanyika watoto wa Mungu. (Yohana 1:12). Hii ikiwa na maana ukimkaribisha Yesu katika maisha yako, ni uhakika kuwa UWEZO huo utakuja ndani yako, wa kuweza kuzishinda tabia zote za wapumbavu,  yaani kushinda ulevi, kushinda uzinzi, kushinda anasa, kushinda usengenyaji n.k..

Hivyo kwanini usimpe leo YESU maisha yako ayaokoe, na utoke kuwa mojawapo ya wapumbavu mpaka kuwa mwana wa Mungu mteule, mbarikiwa aliyeandaliwa kwa ajili ya kuurithi uzima wa milele? Ikiwa upo tayari leo kuokoka, basi fungua hapa kwa ajli ya kuongozwa sala ya Toba na kupata maelekezo mengine  ya kiroho >>>>>  SALA YA TOBA

Bwana akubariki sana.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

HEKIMA NI NINI? NA UFAHAMU UNAPATIKANA WAPI?

Nini maana ya Usiwe mwovu kupita kiasi? (Mhubiri 7:17)

USIONDOE ALAMA YA MPAKA ILIYOWEKWA NA MABABA.

Wibari ni nani?(Mithali 30:26)

Maana ya huu mstari ni ipi? Mithali 14:4 ‘Zizi ni safi ambapo hapana ngombe;bali nguvu za ngombe zaleta faida nyingi’.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments