Nini maana ya K.K, na B.K?  (B.C na A.D).

Nini maana ya K.K, na B.K?  (B.C na A.D).

Hivi ni vifupisho vya nyakati.

K.K – Maana yake ni  Kabla ya kuzaliwa Kristo Yesu. Kwa kiingereza (B.C – Before Christ)

Na

B.K  ­- Maana yake ni Baada ya kuzaliwa kwake Kristo Yesu. Kwa kiingereza (A.D– Anno Domino- Katika mwaka wa Bwana )

Lakini mahali pengine wanatumia kifupi cha K.W.K kumaanisha K.K. na  WK kumaanisha B.K. Husasani kwa watu ambao sio wakristo, au hawaamini habari za Yesu Kristo, Lakini maana ni ile ile moja.

K.W.K maana yake ni Kabla ya wakati wa kawaida. Kwa kiingereza (B.C.E – Before the common Era)

Na,

W.K Maana yake ni Wakati wa kawaida. Kwa kiingereza (C.E– Common Era)

Kwamfano unaweza kukutana na habari fulani ya historia kwa mfano inasema kitabu cha Danieli kiliandikwa mwaka 600 KK, au 600 KWK, Hiyo inamaanisha kuwa kiliandikwa miaka 600 kabla ya kuzaliwa kwa Kristo.

Au utakutana na habari inasema Hekalu la Yerusalemu lilibomolewa mwaka 70 BK, Au 70 WW. Maana yake ni hekalu lilibomolewa mwaka wa 70 baada ya Kristo kuzaliwa duniani.

Hivyo tunaposema huu ni mwaka fulani wa 2000 + haimaanishi tangu dunia iumbwe ni miaka elfu mbili imepita hapana, bali ni miaka 2000 baada ya kuzaliwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Kabla ya hapo kulikuwa na miaka mingine mingi iliyopita, zaidi ya 4000, ambayo ndiyo inahesabika kama miaka kabla ya Kristo.

Bwana akubariki.

Je! Umeokoka? Je! Unahabari kuwa hatuna muda mrefu sana, mpaka unyakuo upite? Yote yaliyotabiriwa yameshatimia, na kwamba pengine kizazi chetu kitashuhudia tukio zima la mwisho wa dunia? Swali la kujiuliza je na sisi tumejiwekaje.

Ikiwa upo nje ya Kristo na unataka leo ayageuze maisha yako. Basi uamuzi huo utakuwa ni wa busara sana kwako. Fungua hapa kwa ajili ya Sala ya Toba na maelekezo mengine >>> SALA YA TOBA

 Na Bwana akubariki sana.

Pia Tazama maana ya maneno mengine ya kibiblia chini.

Kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Nini Maana ya Hosana?

Mataifa ni nini katika Biblia?

Wakaldayo ni watu gani?

Bustani ya Edeni ipo nchi gani?

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

NAMI NINAZO FUNGUO ZA MAUTI, NA ZA KUZIMU.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments