Bustani ya Edeni ipo nchi gani?

Bustani ya Edeni ipo nchi gani?

Bustani ya Edeni ipo nchi gani kwa sasa duniani?


Mungu alipoiumba dunia, alichagua eneo moja, na kulifanya kuwa la kipekee na la kitofauti na maeneo mengine yote aliyoyaumba duniani. Eneo hilo akaliita Edeni. Edeni maana  yake ni eneo la furaha kuu, utulivu,paradiso ya Mungu.

Lakini hakuishia hapo tu bali ndani ya hiyo Edeni upande wa mashariki alitengeneza bustani nzuri sana,  ambayo inajulikana na wengi kama bustani ya Edeni. Bustani hii ndiyo  Mungu aliyomweka mwanadamu wa kwanza hapo aishi (yaani Adamu na uzao wake.)

Lakini kama tunavyosoma biblia, wazazi wetu wa kwanza walipoasi, walifukuzwa kutoka katika bustani ile, na kuanzia hapo, hakuna aliyejua makao halisi ya bustani ya Edeni yalikuwa wapi, vifunguu pekee vinavyotupa taswira ya eneo la bustani ya Edeni ni hivi;

Mwanzo 2:8 “Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya.

9 Bwana Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.

10 Ukatoka mto katika Edeni wa kuitilia bustani maji, na kutokea hapo ukagawanyika kuwa vichwa vinne.

11 Jina la wa kwanza ni Pishoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Havila, ambako kuna dhahabu;

12 na dhahabu ya nchi ile ni njema; huko kuna bedola, na vito shoham.

13 Na jina la mto wa pili ni Gihoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Kushi.

14 Na jina la mto wa tatu ni Hidekeli; ndio unaopita mbele ya Ashuru. Na mto wa nne ni Frati”.

Kama tunavyoona hapo, kulikuwa na mto uliokuwa unatoa maji kutoka bustanini na baadaye ukagawanyika katika vichwa vinne, na viwili kati ya hivyo (yaani Hidekeli na Frati) vinajulikana  mpaka sasa na vipo maeneo ya nchi ya Iraq, ili kusoma na kufahamu zaidi historia yao fungua hapa >>>> Mto frati na Hidekeli Na hiyo imewafanya masomi wengi wa biblia kudhania kuwa Edeni ilikuwa maeneo ya nchi ya Iraq au kando kando yake.

Lakini vile vingine viwili (yaani Pishoni na Gihoni) havijajulikana bado. Na iyo imewafanya wengine kudhani bustani ya Edeni ilikuwa nchi ya Uturuki ya sasa n.k.

 Hivyo, hakuna uthibitisho wa moja kwa moja wa kudhania kuwa Edeni ilikuwa Iraq, au Uturuki au sehemu nyingine yoyote. Na hiyo ni kwasababu ya mabadiliko makubwa ya nchi yaliyokuwa yanatokea wakati wa gharika na  ule wakati wa kugawanyika kwa nchi (Mwanzo 10:25). Historia inaonyesha kuwa dunia ilibadilika mwonekano wake kwa sehemu kubwa sana.

Lakini ni wazi kuwa Edeni haikuwa pengine zaidi ya mashariki ya kati, na sio Afrika kama wanasayansi wanavyoamini, nami naamini ilikuwa katika nchi Kaanani (Yaani Israeli ya sasa).

Lakini ikiwa biblia haikutupa maelezo ya kutosha kuhusu jeografia ya bustani ya Edeni baada ya wazazi wetu wa kwanza kuasi, ni wazi kuwa hakuna umuhimu sana wa kujua bustani hiyo iko wapi kwasasa, kwasababu hayo yalishapita. Bali sasa Mungu ametutilia mkazo hasaa kutufahamisha juu ya Edeni yetu ya mbinguni inayokuja.

Yaani ile Yerusalemu mpya, mji mtakatifu ushukayo kutoka mbinguni kwa Mungu. Na Yerusalemu hiyo itashuka juu ya mbingu mpya na nchi mpya zitakazoumbwa kwa wakati huo baada ya utawala wa miaka elfu moja kuisha. Kama vile tu ilivyokuwa  Edeni ilivyoumbwa juu ya dunia ya wakati ule. Kufahamu zaidi juu ya utawala wa miaka 1000 fungua hapa >>>  UTAWALA WA MIAKA 1000.

Lakini kisichojulikana na wengi ni kuwa, si kila mtu atakayeruhusiwa kuingia ndani ya mji huo. Bali wale watakatifu tu watakaoshinda ulimwengu huu.

Tujiulize, Je! Mimi wewe tutakuwa miongoni mwa hao watakaouingia huo  mji mpya wa dhahabu yaani Yerusalemu ya Mbinguni, Edeni halisi ya Mungu? Je! Mambo ya ulimwengu huu bado yanatusonga, mpaka siku ile itukute ghafla tukaachwa?. Je! Unajua kuwa unyakuo upo karibu sana, na dalili zote za kurudi Kristo duniani zimeshatimia?

Ikiwa wewe bado hujaokoka na leo hii utapenda kumkabidhi Kristo maisha yako ayaokoe na akupe uweza wa kufanyika mtoto wake, basi uamuzi huo utakuwa ni wa busara sana kwako ambao hautaujutia milele. Hivyo kama upo tayari, basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba>>>  SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

   Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

MTO YORDANI UKO NCHI GANI KWA SASA?

Israeli ipo bara gani?

ORODHA YA WAFALME WA ISRAELI.

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

UFUNUO: Mlango wa 1

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
7 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Ally Kinota
Ally Kinota
1 year ago

Bustana ya Eden ipo Tanzania mahali penye wanyama mito maziwa na matunda yote uyajuayo hustawi huko ndio taifa teule lenye aman na utulivu na furaha ndio sababu watu wote duniani huja huko kutembelea hiyo bustani nyongeza ni kwamba ndio eneo pekee lenye vithibitisho kuwa fuvu la binadamu wa kale lilipatikana huko unyayo upo huko na hata michoro ipo huko hivyo haitaji akili kubwa kutafakari bustani ipo kama ni zao alilolima Adam ni ngano ulezi vyote hulimwa huko

Pius Beichumila
Pius Beichumila
1 year ago

Wapi tuipate busitani ya edeni kwa sasa,

Anonymous
Anonymous
1 year ago

Vuvu la adam ilipatikana turkana kenya ilipelekwa wapi

Siprian Emason
Siprian Emason
3 years ago

Je hivyo vitasa7 ni nini?
Naomba nitumie domo hilo

Siprian Emason
Siprian Emason
3 years ago
Reply to  Siprian Emason

Je hivyo vitasa7 ni mini?
Naomba nitumie somo hilo