Masheki ni nini?(Zaburi 105:22, Ayubu 29:10)

Masheki ni nini?(Zaburi 105:22, Ayubu 29:10)

Masheki ni watu wenye hadhi ya juu sana, wenye jina kubwa na heshima katika jamii au taifa,

Neno hilo utalisoma katika vifungu hivi katika biblia;

Ayubu 29:9 “Wakuu wakanyamaa wasinene, Na kuweka mikono yao vinywani mwao;

10 Sauti yao masheki ilinyamaa, Na ndimi zao zilishikamana na makaakaa yao”.

Zaburi 68:31 “Masheki watakuja kutoka Misri, Kushi itamnyoshea Mungu mikono yake mara”.

Zaburi 83:11 “Uwafanye wakuu wao kama Orebu na Zeebu, Na masheki yao wote kama Zeba na Zalmuna”.

Zaburi 105:22 “Awafunge masheki wake kama apendavyo, Na kuwafundisha wazee wake hekima”.

Hata Kristo atakaporudi mara ya pili hapa duniani na kutawala kama BWANA WA MABWANA na MFALME WA WAFALME, Atakuwa na masheki wake chini yake. Watu ambao atawapa heshima kubwa kuwa makuhani wake na wafalme katika enzi yake yote duniani kote.

Na watu hao watakuwa si wengine zaidi ya watakatifu walioshinda zamani, na watakaoshinda sasa ulimwengu huu mbovu.

Hizi ni baadhi ya ahadi alizowaahidia watakaoshinda.

Ufunuo 2:26 “Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa,

27 naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu”.

Ufunuo 3:12 “Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya”.

Ufunuo 3:21 “Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.

22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa”.

Je! Mimi na wewe tupo miongoni mwa watakaoshinda? Kama bado, Je! Upo tayari kumpa Yesu maisha yako leo? Ikiwa jibu ni ndio basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba >>> SALA YA TOBA

Bwana atutie nguvu.

Maran Atha.

Tazama maana ya maneno mengine ya biblia chini.

Na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Kicho ni nini? (Waefeso 5:21, 2Samweli 23:3)

MARINDA KATIKA BIBLIA NI KITU GANI?

Nini maana ya “chakula hakituhudhurishi mbele za Mungu”?

FANYIKA SIPORA WA KRISTO, UNYAKUO UPO KARIBU.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments