MARINDA KATIKA BIBLIA NI KITU GANI?

MARINDA KATIKA BIBLIA NI KITU GANI?

SWALI: Marinda yanayozungumziwa kwenye Yeremia 13:26 ni kitu gani?

Jibu: Tuanze kusoma kuanzia juu kidogo..

Yeremia 13: 24 “Kwa sababu hiyo nitawatawanya, kama makapi yapitayo, kwa upepo wa jangwani.

 25 Hiyo ndiyo kura yako, fungu lako ulilopimiwa na mimi, asema Bwana; KWA KUWA UMENİSAHAU, NA KUUTUMAİNİA UONGO.

26 Kwa ajili ya hayo, MİMİ NAMİ NİTAYAFUNUA MARİNDA YAKO MBELE YA USO WAKO, na aibu yako itaonekana.

27 Nimeona machukizo yako, naam, uzinifu wako, na ubembe wako, na uasherati wa ukahaba wako, juu ya milima katika mashamba. Ole wako, Ee Yerusalemu! Hutaki kutakaswa; mambo hayo yataendelea hata lini”.

Habari hiyo sio maonyo kwa wanawake, au wanaume wazinifu waliomwacha Mungu..La! Bali ni maonyo ya Taifa zima la Israeli lililomwacha Mungu..

Kama wewe ni mwanafunzi wa biblia itajua kuwa karibia mara zote, Mungu wa mbingu na nchi analifananisha kanisa lake na mwanamke, kadhalika alilifananisha Taifa lake la Israeli na mwanamke, Ndio maana utaona sehemu kadhaa anazungumza habari za binti Sayuni,..sasa binti Sayuni anayezungumziwa katika biblia sio binti fulani ambaye anaitwa Sayuni, au anayeishi mji unaoitwa Sayuni.. La!..bali binti Sayuni anayezungumziwa ni Taifa zima la Israeli. Yeremia 13:8-10. Kwa urefu kuhusu Binti Sayuni unaweza kufungua hapa >> SAYUNI

Sasa basi kama jamii ya watu wa Mungu, kwa ujumla inafananishwa na mwanamke, kibiblia jamii hiyo ikimwacha Mungu na kwenda kuifuata miungu mingine ya kigeni, mbele za Mungu jamii hiyo ya watu inaonekana kama inafanya ukahaba/inazini. Mbele za Mungu ni kama mwanamke anayezini..

Vifuatavyo ni baadhi ya vifungu vya biblia vinavyozungumzia habari ya Taifa la Israeli jinsi linavyofananishwa na Mwanamke, na jinsi linavyoonekana kama linazini pale linapomwacha Mungu…vifungu hivi unaweza kuvisoma binafsi.. (Kumbukumbu 31:16, Waamuzi 8:27, Isaya 23:17, Yeremia 3:1-7, 1Nyakati 5:24-26).

Kwahiyo tukirudi kwenye huo mstari unaozungumzia MARINDA.. Sasa marinda yanayozungumziwa hapo sio kitu kingine kinachoweza kudhaniwa, bali ni SKETI ZENYE MARINDA. Sketi za wanawake zamani na hata siku hizi zipo zinazotengenezewa na marinda.. Nguo za mabinti zote nyakati za zamani ni lazima zitengenezwe na marinda. Hivyo biblia inaposema hapo “ MIMI NAMI NITAYAFUNUA MARINDA YAKO MBELE YA USO WAKO”.. maana yake ni kwamba “Taifa hilo limemwacha Mungu na kwenda kuvua sketi zao na kufanya uasherati, kwa siri”… Basi Mungu atalifanya jambo hilo kwa wazi, atalivua nguo taifa hilo na aibu yake (au uchi wake) utaonekana.

Na kweli tunaona jambo hilo lilikuja kutimia kama lilivyo, pale wana wa Israeli walipomwacha Mungu na kukataa kutubu, na badala yake ikaenda kuabudu miungu migeni (yaani kufanya ukahaba)..Na baada ya kuonywa muda mrefu bila matunda yoyote, Mungu alilivua nguo taifa hilo kwa kulipeleka Babeli kwa aibu kubwa. (huko ndio kufunuliwa marinda).

Maombolezo 1:8 “Yerusalemu amefanya dhambi sana; Kwa hiyo amekuwa kama kitu kichafu; Wote waliomheshimu wanamdharau, Kwa sababu wameuona uchi wake; Naam, yeye anaugua, Na kujigeuza aende nyuma.

9 Uchafu wake ulikuwa katika MARINDA YAKE; Hakukumbuka mwisho wake; Kwa hiyo ameshuka kwa ajabu; Yeye hana mtu wa kumfariji; Tazama, Bwana, teso langu; Maana huyo adui amejitukuza.

10 Huyo mtesi amenyosha mkono wake Juu ya matamaniko yake yote; Maana ameona ya kuwa makafiri wameingia Ndani ya patakatifu pake; Ambao kwa habari zao wewe uliamuru Wasiingie katika kusanyiko lako.

Sio hilo tu, yapo pia baadhi ya Miji kama Ninawi, nayo pia Mungu aliyaonya na kuyapa ujumbe kama huo huo wa wana wa Israeli, kwamba yatubie uchafu wao,  lakini hayakufanya hivyo, na siku ilipofika marinda yao, yalifunuliwa kwa aibu na Mungu mwenyewe kama Israeli walivyofunuliwa.

Nahumu 3: 4 “Kwa sababu ya wingi wa ukahaba wa yule kahaba mzuri, yule bibi wa mambo ya uchawi, auzaye mataifa kwa ukahaba wake, na jamaa za watu kwa uchawi wake.

 5 Tazama, mimi ni juu yako, asema Bwana wa majeshi; NAMİ NİTAFUNUA MARİNDA YAKO MBELE YA USO WAKO; nami nitawaonyesha mataifa uchi wako, na falme aibu yako.

  6 Nami nitatupa uchafu uchukizao juu yako, kukufanya uwe mchafu, nami nitakufanya kuwa kitu cha kutazamwa kwa dharau.

7 Hata itakuwa, wote wakutazamao watakukimbia, wakisema, Ninawi umeharibika; ni nani atakayeuhurumia? Nikutafutie wapi wafariji?”

Mungu hajabadilika ni yule yule jana, leo na hata milele..alilowatendea wana wa Israeli, na Ninawi, kwa kumwacha yeye ndicho anachokifanya kwa wale wote wanaomwacha yeye na kufuata miungu yao wanayoijua..

Biblia inasema Roho Mtakatifu anatutamani kiasi cha kutuonea wivu. Wivu anaotuonea ni wivu kama ule wa mtu na mke wake..Unaweza kujua ni wivu mbaya kiasi gani, maana yake ni kwamba tunapomkataa Roho Mtakatifu tunamtia Mungu wivu sana na hivyo tunajitafutia kupata aibu kubwa kama hiyo waliyoipata wana wa Israeli na Ninawi na kufunuliwa marinda yao..

1Wakorintho 10:21  “Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.

22  AU TWAMTIA BWANA WIVU? Je! Tuna nguvu zaidi ya yeye?”

Kama hujampa Kristo maisha yako, fahamu kuwa unamtia Bwana wivu..ni wakati wako sasa wa kutubu na kusalimisha maisha yako kwake.. Kama upo tayari kutubu leo basi fuatisha sala hii kwa kufungua hapa >> SALA YA TOBA.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

Uasherati wa Kiroho maana yake nini?

MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.

Nini Tofauti kati ya uzinzi na uasherati ?

NI KWA NAMNA GANI ROHO HUTUTAMANI KIASI CHA KUONA WIVU?

WAFIRAJI KWENYE BIBLIA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments