MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.

MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.

Kufanya kitendo cha ndoa na mtu ambaye hamjaoana, ni kwenda kinyume na maagizo ya Mungu, kuwa na boyfriend au girlfriend na kujihusisha na vitendo vya kukutana kimwili kuna madhara makubwa sana kiroho.
Dhara la kwanza: Wote mnakuwa mwili mmoja.

Biblia inasema katika…

1 Wakorintho 6:16 “Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja. 17 Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye”.

Ili kuelewa juu ya kuwa mwili mmoja, hebu tutafakari ni kwa namna gani, kanisa ni mwili mmoja na Kristo, ndipo tuelewe ni madhara ya kuwa mwili mmoja na kahaba.
Maandiko yanasema..katika

Warumi 12:5 “ Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake.”

Hii ina maana kuwa watu wote waliomwamini Kristo na kubatizwa na kupokea Roho, hao wanafanyika kuwa viungo vya Kristo, yaani mwili wa Kristo, wanakuwa mwili mmoja na Kristo.
Sasa ni faida gani mtu anazipata anapokuwa mwili mmoja na Kristo?..Ni wazi kuwa Baraka zote Kristo alizokabidhiwa na Baba zinakuwa juu ya huyo mtu…

Waefeso 1:20 “..aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho;

21 juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia;

22 akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo

23 ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote”

Umeona Kristo aliwekwa juu sana kwaajili ya kanisa, ndio maana popote atakapokuwepo Kristo na sisi tupo naye, baraka zote alizobarikiwa Bwana Yesu na sisi tumebarikiwa nazo, enzi yote aliyopewa Bwana Yesu na sisi tumepewa, kwasababu sisi ni mwili wake, yeye ni kichwa. Ndio maana biblia inasema hakuna awezaye kutushitaki,

Warumi 8:31 “Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?

32 Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?

33 Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki.

34 Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea”.

Baraka zote hizo ni kutokana na kwamba tumeunganishwa kuwa mwili mmoja na Kristo. Lakini kinyume chake endapo Kristo angekuwa amelaaniwa nasi pia tungekuwa sehemu ya laana yake. Lakini Kristo hakulaaniwa bali alibarikiwa ndio maana nasi pia tumebarikiwa.Sasa kinyume chake mtu ambaye ni Kahaba, moja kwa moja anakuwa anaishi chini ya Laana ya Mungu, mtu huyu anapokwenda kukutana na mtu mwingine ambaye si kahaba kama yeye, na akalala naye, katika ulimwengu wa roho anafanyika mwili mmoja naye…Hivyo anashiriki laana zake zote kwa Yule mtu mwingine, Matatizo yake yote anakuwa anashiriki na yule aliyekutana naye kimwili, hapo ndio chanzo cha matatizo ya watu wengi yanapoanzia.

Unakuta mtu alikuwa ni mzuri tu na hana matatizo yoyote, lakini anapokwenda kulala na mtu mwingine ghafla hali yake inabadilika, hajui tatizo ni nini, kumbe katika ulimwengu wa roho, anashiriki matatizo yote, na laana zote, na mikosi yote ya yule mwenzake aliyoibeba….Mbele za Mungu wote wanaonekana ni mwili mmoja…Kama yule mtu alikuwa ni adui wa Mungu, pengine ni muuaji, au ni mshirikina, au mchawi, au mtu wa kudhihaki injili…na wewe unakwenda kulala naye…Hapo mbele za Mungu wote ni washirikina, wote ni wachawi, na wauaji…haijalishi hujawahi kuua, wala kwenda kwa waganga…kitendo tu! cha wewe kukutana kimwili na mtu mwenye matendo hayo, tayari mbele za Mungu wewe nawe ni mshirika.

Kama tu Ukimwi unaweza kumwingia mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa kitendo hicho, kwanini matatizo ya rohoni mtu usiambukizwe!..Watu hawaelewi kuwa kuna magonjwa ya rohoni ambayo nayo pia yanaambukizwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kwa vitendo kama hivyo.

Na kahaba sio tu mtu anayejiuza kule barabarani akitafuta fedha, la! Kahaba ni mtu yeyote ambaye yupo tayari kufanya kitendo cha kukutana kimwili kwa malipo au hata pasipo malipo..Kinachohuzunisha ni kwamba siku hizi kitendo hicho hata hakifanyiki kwa malipo, tofauti na zamani…kwahiyo makahaba wa siku hizi ni wabaya Zaidi kuliko wa zamani, mtu yeyote aliye na boyfriend au girlfriend na anaishi naye na hawajaoana, huyo ni kahaba! Haijalishi wana mpango wa kuoana huko mbeleni! Kitendo tu cha kukutana na mtu huyo kabla ya ndoa tayari huo ni uasherati!.

Unataka laana hizo zote zisikupate?..Jiepushe na uasherati!..utasema haiwezekani kujiepusha nao?..wapo mamilioni ya watu wanaoshinda uasherati! Na hawaishi Maisha ya zinaa hata kidogo! Shetani asikudanganye kwamba hakuna mtu anayeweza kushinda uasherati huo ni uongo!Dhara la Mwisho na Kubwa la uasherati ni ZIWA LA MOTO!Biblia inasema wazinzi wote sehemu yao ni katika lile ziwa la moto..

Ufunuo 21:8 “… Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili”.

Wagalatia 5: 19 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi …….kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu”.

1Wakoritho 6:9 “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,”

Hatima ya wote wanaofanya uasherati au uzinzi kwa siri, ni ziwa la moto.Ikiwa leo unaishi na mwanamume au mwanamke ambaye hamjafunga ndoa! Mwache haraka sana kama unataka kwenda mbinguni, au mwambie mkafunge ndoa …Ikiwa unaishi na mtu unayemwita girlfriend au boyfriend nataka nikuambie mpo chini ya laana, na endapo mkifa ghafla ni moja kwa moja kwenye ziwa la moto, hiyo ni kulingana na maandiko. Kaa mwenyewe mpaka wakati utakapofika wa wewe kuoa au kuolewa, kama uliweza utotoni kwanini usiweze ukubwani!! Epuka injili za shetani zilizozagaa huko zikikuambia ni ngumu kuishi bila hayo mambo, hizo zote zina lengo la kukupeleka kuzimu.

Bwana akubariki sana, kama hujampa Bwana Yesu Maisha yako, ni vyema ukafanya hivyo kabla siku zako hazijaisha za kuishi hapa ulimwenguni..kabla haijakaribia miaka utakaposema sina furaha katika hiyo (Mhubiri 12).

Maran atha!.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii 0789001312Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group


Mada zinazoendana:

“MOTO HUFA KWA KUKOSA KUNI’’..NA NDIVYO ILIVYO KWA UASHERATI

Nini Tofauti kati ya uzinzi na uasherati ?


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
16 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Jumanne sonah
Jumanne sonah
3 months ago

Barikiwa thana mtumishi,
Ni kweli dhambi ya uzinzi ndio inalitafuna thana kanisa la Mungu na shetani anaeneza injiri potovu eti huwezi hata kumaliza wiki au siku mbili hujafanya tendo la ndo huo ni upumbaaavu uliokithiri kabisa.
Vijana hawajaoa lakini wazoefu kama wapo kwenye ndoa kongwe na walio kwwnye ndoa wanachafua ndoa wakisema kuchanganya kadha Mungu awasaidie sana

Anonymous
Anonymous
1 year ago

Halleluya mt, barikiwa sana

Gaudencius Peter
Gaudencius Peter
2 years ago

Barikiwa sana

Maige
Maige
2 years ago

Ubarikiwe mno mtumish. Kuna wale waliofanya uasherati na wakapata watoto au mtoto, hapa neno la Mungu au guadhabu ya Mungu itawaepuka vipi!? Au warudi wakawaoe watu hao?

Jumanne sonah
Jumanne sonah
3 months ago
Reply to  Maige

Kama anamtoto lakini hajaoa wala kuolewa warudiane haraka na kupata kibar kwa Mungu ila kama walioa na kuolewa kwingine waendelee hukohuko ila wahalalishe kwa kupata kibali kwa Mungu vinginevyo hao bado wanahesabika wazinzi2

Baraka Richard
Baraka Richard
2 years ago

Asante Sana kwamasomo kwakweli yamenifungua nimepata ufahamu wakujua mengi ambayo sikuyajua Mungu awabariki Sana,Niliibiwa simu tangu mwenzi wapili nikawa sio wala kuyapata masomo haya kwakweli nilikuwa nakosa Amani Asante Sana kwamasomo manzuri.

Evance peter
Evance peter
2 years ago

Naitwa katekista evance nipo arusha. Barikiwa sana mungu akutie nguvu kwa mafundisho mazuri amina

Emmanuel emily
Emmanuel emily
3 years ago

Ubarikiwe sana mtumishi wa mungu.hapo umepiga kwa dhambi hiyo wengi wamejisahau wameona kutenda dhambi hiyo ni kawaida.hawamwogopi mungu.

Jonas
Jonas
3 years ago

Mimi hayo yote nimeshafanya, nimekuwa mzinzi, muasherati ninajuta sana kupitia hayo.. sijakuwa mtiifu wa Amri za Mungu …. Mtumishi niombee nami niwe katika sehemu ya watakatifu

mringo je2
mringo je2
3 years ago

hii kit imenisaidia sanaa na inafundisha vizuri sana

Jonas Manyika
Jonas Manyika
3 years ago
Reply to  Admin

Mimi hayo yote nimeshafanya, nimekuwa mzinzi, muasherati ninajuta sana kupitia hayo.. zinakuwa mtiifu wa Amri za Mungu …. Mtumishi niombee nami niwe katika sehemu ya watakatifu