Nini Tofauti kati ya uzinzi na uasherati ?

ByAdmin

Nini Tofauti kati ya uzinzi na uasherati ?

SWALI : Pale Bwana Yesu aliposema “Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.(Mathayo 5:32)” Alimaanisha nini?.


JIBU: Neno usherati kama linavyoonekana kwenye kamusi, tafsiri yake ni “kufanya kitendo cha ngono na mtu ambaye bado haujaoana naye”..hii ikimaanisha kuwa inaweza ikawa mtu yupo ndani ya ndoa au nje ya ndoa, tofauti na Neno UZINZI, ambao huo unakuja pale mtu anapofanya kitendo cha ngono na mtu ambaye si mwanandoa mwenzake (yaani kitendo cha kutoka nje ya ndoa na kwenda kufanya ngono). Hivyo tunaweza kusema Neno Usherati ni Neno la ujumla likimaanisha kitendo chochote cha zinaa kinachofanywa na mtu isivyopaswa yaani nje ya ndoa halali. Kwahiyo Bwana Yesu aliposema pale katika Mathayo 5:32 na Mathayo 19:9, kwamba lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi;.. kitendo kile alikilenga hasa kwa wanandoa, kwasababu habari iliyokuwa inazungumziwa pale ni ya watu ambao wapo katika mahusiano ya mke na mume. 

Pia kwa kuongezea hapo, ukisoma sehemu nyingi katika maandiko kwenye agano la kale na jipya, utaona Mungu alilitumia hilo neno Uasherati, kumaanisha uzinzi ambao watu wake walikuwa wanafanya katika roho, soma 〈2 Nyakati 21:10-14,〉 〈Ezekieli 16:27, 43, 58,〉 Ezekieli 22:11, 〈Ufunuo 17:1-5, 19:2 〉n.k. vipo vifungu vingi sana na vyote hivyo vinautaja uzinzi kama uasherati, ambao watu wa Mungu wameufanya na sanamu na machukizo yao…Uasherati ni Neno la Ujumla, ukitaka kushikilia tu Uasherati katika biblia unamaanisha kitendo cha ngono nje ya ndoa takatifu, basi biblia itakuwa haina maana sehemu nyingi, ikiwemo katika hivyo vifungu nilivyovitoa hapo juu. 

Hivyo biblia inaposema Ndoa na iheshimiwe na watu wote, ilimaanisha kweli kweli. huwezi kuingia tu kwenye ndoa halafu ukajifanyia tu mambo unayotaka ukaamua kwenda kuzini ukijifariji kuwa hiyo ndoa tayari imeshafungwa haiwezi kuvunjika..Ndugu nataka nikuambie Inaweza kuvunjika kwa kitendo hicho na isiwe makosa mbele za Mungu kwenda kuoa/kuolewa na mwingine.

 Lakini ifahamikie pia hilo halikuwa agizo kwamba kila kitendo cha kukosa uaminifu katika ndoa iwe sababu ya mtu kumwacha mkewe na kwenda kuoa mwingine hapana.. Mungu hapendi kuachana biblia imesisitiza hilo, na zaidi ya yote tumefundishwa kusamehe, kwani hata na sisi tunamkosea Mungu kwa mengi. Hivyo kusamehe ni msingi mkubwa sana wa ndoa kusimama. Na zaidi ya yote ni uaminifu na kuwa na hofu kwa Mungu, tukijua kuwa ndiye Mungu aliyeiunganisha, tusigeuke kuwa VIFO katikati yetu. mwanandoa aliweke hilo kichwani kuwa akienda kuzini amestahili kuachwa kibiblia na kusiwe na hatia zozote mbele za Mungu. 

Shalom.


Mada Nyinginezo:

MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.

‘’MOTO HUFA KWA KUKOSA KUNI’’..NA NDIVYO ILIVYO KWA UASHERATI

USIWE SABABU YA WATU KUMKUFURU MUNGU.

KITABU CHA UZIMA

MPINGA-KRISTO

MWENDO UNAOSHANGAZA SANA!


Rudi Nyumbani:

 

 

 

 

Print this post

About the author

Admin administrator

2 Comments so far

Sara UisoPosted on11:08 mu - Mei 13, 2020

Shalom.Mimi bado sijaelewa inamana mwanamke akiachwa kwa kosa hilo anaweza olewa Tena ndoa halali?

    AdminPosted on7:57 um - Mei 13, 2020

    Shalom…kama mwanamume anaweza kumuacha mwanamke aliyeshikwa katika uasherati endapo tu na yeye tangu afunge hiyo ndoa hajawahi kufanya uashetari na mwanamke mwingine yoyote…lakini kama na yeye alishawahi kufanya aidha kwa siri au kwa wazi na akamkuta mkewe katika uasherati hapo anapaswa amsamehe na hapaswi kumwacha kwa vyovyote vile akimuacha na kwenda kuoa mwingine anazini…

    Na ikitokea mwanamume hajawahi kuisaliti ndoa yake na akamkuta mkewe katika uasherati hapo yupo huru kumuacha na kwenda kuoa mwingine kulinga na maandiko..ingawa kitendo hicho sio cha heshima kwa huyo mwanamume kama tulivyojifunza hapo juu. Na mwanamke huyo aliyeachwa hapaswi kuolewa tena mpaka mwanamume huyo afe atabaki hivyo hivyo bila kuolewa..akienda kuolewa anazini…atabaki kuwa mfano wa wale wake wa mfalme Daudi ambao waliolala na mtoto wa Mfalme Daudi aliyeitwa Absalomu.

    Ubarikiwe.

Leave a Reply