SWALI: 2 Wafalme2:12; `Naye Elisha akaona,akalia,Baba yangu,baba yangu,GARI LA ISRAELI NA WAPANDA FARASI WAKE! Asimwone tena kabisa;’ ” Hapo anaposema “Gari la Israeli na wapanda farasi wake!-Anamaana gani?”
JIBU: Hilo ni swali la kujiuliza ni kwanini mwisho wa safari ya Eliya linatokea gari kutoka mbinguni na wapanda farasi wake, na si isiwe kitu kingine labda ngazi, au upepo au aishie kutoweka tu asionekane mpaka litokee gari la vita?, Hizi ishara zinazotokea mwisho za washindania Imani, zinakuwa na maana kubwa sana kwetu, ni sawa na Bwana wetu Yesu alivyoondoka tujiulize ni kwanini WINGU lilimpokea na si gari au malaika..lipo jambo Mungu anatuonyesha katika haya matukio.
Lakini tukirudi kwenye tukio la Eliya, Kulitokea gari la Vita, Elisha ndio alivyoliona, hii kuonyesha kuwa Eliya alikuwa vitani Duniani anapigana, na sasa mwisho wa vita vyake umefika, Ushindi ameshaupa, vita kavipiga, mwendo kaumaliza, Umefika wakati wa kuondoka, Hivyo ni wajibu lile jeshi lililokuwa linapigana naye yeye kama Jemedari wao siku zote za maisha yake, lije kumchukua na kumpeleka nyumbani kwa vishindo vikuu vya ushindi. Vivyo hivyo hata leo kwa mtakatifu yoyote atakayemaliza kazi yake duniani kwa ushindi , siku ile anayokufa, katika Ulimwengu wa Roho lile Gari la Israeli [yaani Jeshi la ki-mbinguni] ambalo siku zote za maisha yake amekuwa akitembea nalo kupigana vita litamchukua moja kwa moja mpaka Paradiso kule watakatifu wengine walipo. Lakini hiyo ni mpaka mtu apigane na ashinde, asiposhinda hakuna atakayekuja kumchukua, huyo atabakia kaburini, Na ndio maana Mtume Paulo mwisho wa safari yake aliandika hivi:
2Timotheo 4:6 “Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika. 7 Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;8 baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake”.
2Timotheo 4:6 “Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika.
7 Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;8 baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake”.
Hivyo na sisi pia tujitahidi tukaze mwendo, siku ile tuondoke na ushindi mnono duniani. Kwasababu yapo mema mazuri Mungu ametuandalia huko tuendako.
Ubarikiwe.
ROHO YA ELIYA KATIKA AGANO JIPYA INATENDAJE KAZI?
NITAONGEZAJE NGUVU ZANGU ZA ROHONI?
JE! MBINGUNI KUTAKUWA NA KULA NA KUNYWA?
JE! NI HALALI KUTOA CHETI KWA WAKRISTO WANAOOA?
Rudi Nyumbani:
Print this post
Mungu ni mwema kila wakati
hakika ni mwema siku zote.