Je! ni halali kutoa cheti kwa wakristo wanaooa?

Je! ni halali kutoa cheti kwa wakristo wanaooa?

JIBU: Ndio ni halali, Tunapaswa tutofautishe kati ya yale maagano ya mwilini na yale ya rohoni. Tunapookoka na kubatizwa katika ubatizo halali, hapo ni sawa na tumefungishwa ndoa na kuwa mwili mmoja na Kristo, ni hiyo ni ndoa ya kimbinguni kwasababu haitambuliki katika mwili, hata karamu yake haifanyiki huku bali kule mbinguni, vivyo hivyo nacheti chake ni lazima kiwe cha kule, na cheti chenyewe ndio ule uzima wa milele, pale tunapojua majina yameandikwa katika kitabu cha uzima.

Lakini mtu anapooa, au anapoolewa, haowi mbinguni au haolewi mbinguni bali ni hapa hapa duniani, hivyo kuwa na ushahidi au uthibitisho wa uhalali wa ndoa hiyo ni muhimu kuwepo, ni moja ya vigezo vya kuzingatiwa katika hatua za mwisho za ndoa. Na sio lazima kiwe ni cheti kabisa lakini walau waraka wa makubaliano uliothibitishwa na mashahidi kanisani (Mchungaji wako na waumini). Ikiwa tu kitendo cha kuachana katika Israeli kilihitaji “hati/cheti” (Mathayo 19:7, Kumbu 24:1) si zaidi kukubaliana?.  

Na Hiyo faida yake ipo katika mwili, mojawapo ni hii unaweza kwenda mahali ugenini na mkeo, mkashindwa kuruhusiwa kuingia, au kushirikiana katika mambo Fulani, au kulala pamoja kwa kuwa tu hamna cheti cha ndoa, hususani katika nyumba za wageni.   Pili hata ikitokea mmojawapo amefariki, hatua za kimirithani, yaani urithishaji mali, kama hakuna cheti inamaanisha, Serikali ya kidunia inaweza kukuzuia usiwe na haki ya kumiliki mali za mwenza wako ambazo mlizichuma pamoja.   Hivyo japo katika roho cheti kinaweza kisiwe na maana yoyote, Na wala biblia haijaagiza lolote kuhusu hilo, lakini katika mwili kina umuhimu mkubwa, na pia ili kuiheshimisha ndoa yako, na kuipa thamani yake, ni vizuri ukapewa hati ya ndoa kanisani kwako.(Waebrania 13:4).

Bwana akubariki.


Mada Nyinginezo:

NDOA NA HARUSI TAKATIFU.

NDOA NA TALAKA:

MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.

MTI UANGUKAPO, PAPO HAPO UTALALA.

SIKU YA TAABU YA YAKOBO.

JE! MBINGUNI KUTAKUWA NA KULA NA KUNYWA?.

SIFA TATU ZA MUNGU.


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments