JIBU: Biblia haijaeleza kwa mapana na marefu mambo yatakayokuwa yanaendelea mbinguni baada ya unyakuo kupita, na ndio maana mtume Paulo anasema katika 1Wakorintho 13:9 “Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu;..”
Hivyo kuhusu kama watakatifu watakula au hawatakula na kunywa biblia haijatoa jibu la moja kwa moja lakini tunaweza kutazama baadhi ya mistari inaweza kutusaidia kupata picha fulani. Tukisoma:
Marko 14.23 “Akatwaa kikombe, akashukuru, akawapa; wakakinywea wote.24 Akawaambia, Hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi.25 Amin, nawaambia ninyi, Sitakunywa tena kabisa uzao wa mzabibu, hata siku ile nitakapounywa mpya katika ufalme wa Mungu.26 Nao walipokwisha kuimba walitoka kwenda mlima wa Mizeituni”.
Marko 14.23 “Akatwaa kikombe, akashukuru, akawapa; wakakinywea wote.
24 Akawaambia, Hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi.
25 Amin, nawaambia ninyi, Sitakunywa tena kabisa uzao wa mzabibu, hata siku ile nitakapounywa mpya katika ufalme wa Mungu.
26 Nao walipokwisha kuimba walitoka kwenda mlima wa Mizeituni”.
Tunaona katika habari hiyo hapo, Yesu akiwaagiza mitume wake kwa habari ya kunywa katika ufalme wa mbinguni, Lakini pia tukimtazama Bwana baada ya kufufuka kwake alikuwa na mwili wa umilele wa utukufu usioweza kufa tena, wala kuugua, mwili ambao uliweza kufanya mambo makubwa zaidi yasiyoweza kufanywa na mwili wowote wa asili, ule mwili uliweza kupotea na kutokea mahali popote, uliweza kuchukua sura tofauti tofauti, uliweza kupaa, na mpaka sasa unaishi n.k. Na kumbuka pia biblia inatuambia “siku atakapodhihirishwa tutafanana naye (1Yohana 3:2)”..Sasa jambo ambalo utaliona pale alipowatokea mitume wake baada ya kufufuka kwake aliwaambia wampe chakula chochote ale.
Luka 24.41 “Basi walipokuwa hawajaamini kwa furaha, huku wakistaajabu, aliwaambia, Mna chakula cho chote hapa? 42 Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa.43 Akakitwaa, akala mbele yao”.
Luka 24.41 “Basi walipokuwa hawajaamini kwa furaha, huku wakistaajabu, aliwaambia, Mna chakula cho chote hapa?
42 Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa.43 Akakitwaa, akala mbele yao”.
Hiyo inatupa picha kwa sehemu jinsi miili hii ya utukufu itakavyokuwa, haitakuwa na mipaka Fulani kwamba kwasababu ni ya umilele haitaweza kula wala kunywa. Ni kweli kabisa uzima wa hiyo miili hautakuwa tena katika vyakula, inaweza kuendelea kuishi bila ya njaa wala chakula wala kutegemea chochote kile,kwasababu asili yake ni ya kimbinguni lakini hiyo haimaanishi kuwa haitaweza kunywa wala kula. Pia kumbuka Adamu kwa asili kabla ya kuasi alikuwa mtu wa umilele, asiyeweza kufa, wala kuugua, wala kuzeeka, lakini pamoja na ukamilifu wake Mungu bado alimuumbia ndani yake kula na kunywa katika ile bustani ya Edeni. Hivyo tusubiri tuone, tukifika huko tutajua zaidi, kikubwa tu tunachopaswa kufanya sasahivi ni kujitahidi kuishi maisha ya ushindi yampendezayo Mungu ili siku ile itakapofika tusikose kuyaonja hayo mambo mazuri Mungu aliyotuandalia ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia.
Ubarikiwe.
Mada Nyinginezo:
JE! MBINGUNI KUNA MALAIKA WA KIKE?
CHAGUA NI JIWE LIPI LITAKALO KUFAA KWA UJENZI.
ALAMA KATIKA VIPAJI VYA NYUSO.
USIONDOE ALAMA YA MPAKA ILIYOWEKWA NA MABABA.
JIHADHARI NA ROHO ZIDANGANYAZO.
UMUHIMU WA KUISHI MAISHA YAMPENDEZAYO MUNGU SASA.
MPENDE JIRANI YAKO KAMA NAFSI YAKO.
Rudi Nyumbani:
Print this post
Je, kuna siku Yesu au Roho takatifu ilifundisha kuhusu maisha ya mbinguni ? Je, malaika au viumbe walio mbinguni wanakula ?