Je! kuchora tattoo ni dhambi?

Je! kuchora tattoo ni dhambi?

JIBU: Biblia inasema katika kitabu cha Mambo ya

Walawi 19: 28 “Msichanje chale yo yote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala MSIANDIKE ALAMA MIILINI MWENU; mimi ndimi Bwana”.

Bwana alikataza watu kuchanjwa chale kwasababu chale zote zinahusiana na ibada za wafu, au ushirikina, Bwana hajawahi kuwaagiza wana wa Israeli wanapopatwa na matatizo fulani au wanapohitaji kinga ya jambo Fulani wachanjwe chale..Hizo zilikuwa ni ibada za kipagani ambazo tunaona hapa Bwana anawaagiza wana wa Israeli wasizifuate hizo desturi…Bwana aliwaagiza kuwa tiba ya magonjwa yao ni kuzishika sheria zake basi na sio kwenda kujichanja mwilini.  

Lakini pia aliwaagiza wasiandike alama zozote katika miili yao (tattoo). Sasa wengi hawajui asili ya tattoo…watu wa zamani walikuwa hawachori tattoo kwa lengo la urembo kama sasahivi, watu wa zamani walikuwa wanachora tattoo kwenye miili yao kwa lengo hilo hilo kama la kuchanja chale, (kwa lengo la ibada) ilikuwa ni ibada za miungu, na walikuwa wanafanya hivyo kufuata maagizo ya miungu yao kuwa wanapotaka wapate jambo Fulani, au wajikinge na hatari Fulani, ni lazima wachore alama hizo katika miili yao..  

Hivyo zinaweza kuwa ni michoro ya aina Fulani ya wanyama kama vile nyoka, ndege, au wakati mwingine majina Fulani ya lugha zisizoeleweka, au alama za jua, au mwezi n.k. Na kwasababu shetani ndiye aliyekuwa nyuma ya mambo hayo basi kila aliyefanya hivyo alikuwa ananufaika kwa sehemu Fulani kwa masuala ya kishetani..ni kama tu mtu aliyechanjwa chale au anayetembea na hirizi leo, anakuwa anatembea na pepo Fulani linalomkinga dhidi ya mambo Fulani yanayohusiana na anachokiamini.   Lakini miaka ilipokwenda mbele watu waliwaona watu wanaojichora tattoo kuwa wanapendeza, hivyo pasipo kuchunguza asili la lile jambo ni ipi nao pia wakaenda kuiga mioyoni mwao wakidhani kuwa wanaweka urembo tu kwenye miili yao kumbe wanaweka uchawi na mapepo kwenye miili yao pasipo wao kujijua..wanajiongezea roho Fulani za yule adui katika maisha yao.   Kwahiyo mwili wowote wenye tattoo tayari una pepo fulani ndani yake, kwasababu asili ya tattoo au chale sio urembo bali kinga Fulani za kichawi..

Na Biblia imetuonya kuwa miili yetu inapaswa iwe hekalu la Roho Mtakatifu.  

1Wakorintho 6: 19 “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;

20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu”.  

Kumbuka hapo biblia haijasema miili yetu sisi tuliomwamini Bwana YESU kuwa ni NYUMBA YA KAWAIDA, bali ni HEKALU, hekalu ni tofauti na nyumba za kawaida, kuna nyumba za aina nyingi, zipo za kulala wageni(guest house), nyumba za kuhifandhia mizigo, nyumba za kiofisi nk lakini HEKALU ni nyumba maalumu kwa ajili ya Ibada tu!!..sasa nyumba yenye chale au yenye tattoo itakuwaje hekalu la Mungu,?..Unaona?

kwahiyo kuchora tattoo ya aina yoyote ile sio sahihi.   Kama ulijichora tattoo huko zamani, au ulichanjwa chale udogoni na sasa umempa Bwana maisha yako hiyo ni vizuri sana, ile roho nyuma ya hiyo tattoo imeondoka lakini shetani bado atakuwa na visababu vichache vichache vya kukushitaki mbele za Mungu, hivyo chukua uamuzi wa kwenda kuvifuta hivyo vitu ili shetani asipate sababu yoyote ya kukushitaki..na pia mwili wako usitumike kuitangaza kazi za shetani, kwasababu usipofuta ni sawa na kampuni fulani la matangazo..   Hivyo futa tattoo zote mwilini mwako, uuwekwe mwili wako wakfu kwa Mungu sasa ili autumie..  

Ubarikiwe.

Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp


Mada Nyinginezo:

JE! KUBET NI DHAMBI?

JE! KUSHIRIKI AU KUJIHUSISHA KWENYE MICHEZO NI DHAMBI?

JE! KUFANYA MASTURBATION (PUNYETO) NI DHAMBI?

AMPOKEAYE NABII KWA KUWA NI NABII, ATAPATA THAWABU YA NABII; MSTARI HUU UNAMAANA GANI?

NJIA SAHIHI YA KUFUNGA.

JE! SISI NI WAFALME NA MAKUHANI KWA NAMNA GANI?

UNYAKUO.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Micchael Paul
Micchael Paul
1 year ago

Mbarikiwe sana kwa somo zuri

Michael Matho
Michael Matho
1 year ago

Like these messages to assist me on my servant ship.