Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; Mstari huu unamaana gani?.

Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; Mstari huu unamaana gani?.

JIBU: Zipo thawabu za aina nyingi na tofauti tofauti katika biblia, Kuna thawabu za kukubali kushutumiwa au kuteswa kwa ajili ya Kristo (Luka 6:22),Si wengi wanazipenda hizi, Kuna thawabu ya kutenda mema (Luka 6:35), vilevile kuna thawabu za utumishi (1Wakorintho 3:8), kuna thawabu za wanaomtafuta Mungu kwa bidii tu(Waebrania 11:6), kuna thawabu ya kumfanyia Mungu kitu bila unafki, mfano kufunga, kusali, na kutenda wema,…Kuna thawabu za kuisapoti kazi ya Mungu(Malaki 3:10), na nyingine nyingi..Hivyo ni mtu tu kuchagua ni ipi au zipi zitakazomfaa. 

Vile vile zipo thawabu nyingine kama hizi, mfano kumpokea Nabii,(Akimaanisha watumishi wote wa Mungu), na kupokeo huko kupo kwa namna mbili, ya kwanza ni kumpokea kwa alichokibeba, na kumpokea kwa alichopungukiwa..kile alichokibeba ni ujumbe wa Mungu..

Mtu akiupokea ule ujumbe ambao mtumishi wa kweli wa Mungu anamletea, tayari moja kwa moja utayaathiri maisha yake na kumbadilisha,na kumbariki, hiyo ni thawabu ya kwanza iliyo kuu, lakini pia namna ya pili ni pale anaponyoosha mkono wake kwa kile alichopungukiwa, yaani kumuhudumia aidha kwa kwa malazi, mavazi, fedha, chakula, hiyo ni thawabu ya pili ambayo Mungu atahakikisha ni lazima amlipe mtu anayefanya hivyo. Halikadhalika, mtu akimstahi mwenye haki, (hapa anamaanisha mkristo mwenzake), atapokea thawabu kulingana na wema aliomtendea, vile vile haiishii hapo, hata akimstahi mzazi wake, atapata thawabu ya mzazi, akimstahi jirani yake, atapata thawabu ya jirani, akiwastahi maskini, Mungu atampa thawabu ya maskini, kipimo kile kile apimacho ndicho hicho hicho atakachopimiwa..hata ukiwastahi wanyama,mimea, mazingira utapata thawabu ya vitu hivyo.n.k. Lakini iliyokuu kati ya hizi zote, ni hiyo ya kuiendeleza kazi ya Mungu, na ya pili yake ni kuwastahi watumishi wake, kwasababu hapo utakuwa umemfanyia Kristo mwenyewe.. Na ndio maana ukisoma mstari wa juu yake na ule wa mwisho utaona anasema.. Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma…Na pia anasema..

Mathayo 10:40 “Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma.

41 Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; naye ampokeaye mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapata thawabu ya mwenye haki.

42 Na mtu awaye yote atakayemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa ngaa kikombe cha maji ya baridi, kwa kuwa ni mwanafunzi, amin, nawaambia, haitampotea kamwe thawabu yake.”..

Hapo anasema kwa kuwa ni “MWANAFUNZI”..sio kwa kuwa ni “maskini au mkulima” hapana bali kwa kuwa ni mwanafunzi….Ikiwa na maana kuwa kumpokea mtu wa Mungu kuna thawabu kubwa kuliko kuwapokea watu wengine wa kawaida.

Sehemu nyingine Bwana alisema maskini mnao sikuzote, lakini mimi hamnami (Yohana 12:8), hivyo unapoligawa fungu lako Mungu aliokubariki kwa wengine, aidha wazazi, maskini, marafiki, ndugu, ambao hao sikuzote unao, usisahau fungu lako kubwa kulirudisha mikononi mwa Mungu, kwasababu huko ndiko kwenye thawabu kubwa na nyingi zaidi tena zidumuzo.. 

Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:

UTALIPWA KATIKA UFUFUO WA WENYE HAKI.

TUZO UTAPEWA KULINGANA NA NAFASI YAKO.

VIGEZO VYA KUWA KARIBU NA YESU KRISTO KATIKA ULIMWENGU UJAO.

MWE NA HASIRA, ILA MSITENDE DHAMBI.

NAMNA GANI NITAPOKEA NGUVU ZA BWANA YESU?.

JINA LA MUNGU NI LIPI?


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments