Je! mbinguni kuna malaika wa kike?. Na je! tukifika mbinguni tutafanana wote?

Je! mbinguni kuna malaika wa kike?. Na je! tukifika mbinguni tutafanana wote?

JIBU: Neno jinsia kwa mara ya kwanza limeonekana kwa wanadamu, Pale Mungu alipomtoa Hawa ubavuni mwa Adamu na kumwita jina lake mwanamke, hapo ndipo jinsia mbili zilipozaliwa yani ya kike na ya kiume, Hapo kabla Adamu alikuwa ni mwanadamu mwenye maumbile yote ndani yake, yaani ya kike na ya kiume,sasa siku alipotolewa ubavu wake, ile sehemu ya uzuri iliondolewa na kuumbwa mwanamke yeye akawabakiwa na ile sehemu ya misuli tu.

Hivyo tukirudi kwa upande wa malaika,ni kwamba suala la malaika wa kike, au wa kiume hilo halipo, japo biblia inawatambulisha kwa vyeo vya kiume, hata majina yao Mikaeli, Gabrieli, n.k yote hayo ni majina yenye asili ya kiume, hata Mungu wetu naye anachukua cheo cha kiume, tunamwita Baba japo yeye sio mwanaume, wala mwanamke.Ni kwanini basi wanatambulika kama wanaume na si wanawake, Ni kwasababu jinsia ya kiume ni jinsia inayoonyasha ukuu, na uweza, na mamlaka, na kutawala kuliko ile ya kike, na hivyo ili kuonyesha kuwa mbingu ndio inayotawala dunia hivyo kulikuwa hakuna budi, viumbe vyote vya kimbinguni vitambulike kwa jinsia ya kiume, ikiwemo Mungu wetu mwenyewe.Mkuu ya vyote.

Laiti kama pale mwanzo Adamu ndiye angetoka kwa Hawa, Na mwanamke angekuwa ni kichwa cha vyote dunia basi mbingu nayo ingejitambulisha kwetu kwa vyeo na majina ya KIKE..Kuna watu wanaosema, wapo malaika wa kike na wa kiume, na ndio maana kipindi kile cha Nuhu walishuka baadhi wakajitwalia wake na wanadamu na hivyo kuzaa yale majitu/wanefili (Mwanzo 6). 

Lakini huo mtazamo sio wa kimaandiko, kwani Bwana Yesu anatuambia tutakapokwenda mbinguni tutafanana na malaika hakuna kuoa wala kuolewa. (Marko 12:25). Kuonesha kuwa malaika hawana jinsia, tulizonazo sisi, viungo vya uzazi viliwekwa kwa lengo la kuzaliana kujiaza nchi, na si kwa jambo lingine.Vile vile na sisi je! tutakapokwenda mbinguni tutafanana wote?. Jibu ni hapana, Mungu alishamaliza kumuumba mwanaume na mwanamke, hivyo kama wewe ni mwanaume utakuwa na asili ya uanaume milele katika huo mwili wa utukutu utakaopewa, na kama wewe ni mwanamke vilevile utakuwa na asili ya uanawake milele katika huo mwili wa utukufu utakaopewa, isipokuwa tu katika masuala ya uzazi ndio tutafanana na malaika..hakuna kuzaa wala kuzaliana,wala kuoa au kuolewa.

Lakini maumbile yetu, yatakuwa kama yetu wenyewe, na malaika kama yao wenyewe kwa jinsi walivyoumbwa na Mungu.

Ubarikiwe sana.


Mada Nyinginezo:

 KUWAHUDUMIA MALAIKA PASIPO KUJUA.

JE! BAADA YA ULIMWENGU HUU KUISHA MALAIKA WATAKUWA NA KAZI GANI TENA?

KUNDI LA MALAIKA WALETAO MABAYA.

NITAJUAJE KAMA NDOTO NI YA MUNGU AU YA SHETANI?

FIMBO YA HARUNI!

USIWE SABABU YA WATU KUMKUFURU MUNGU.


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Isaac
Isaac
3 months ago

Nashukuru sana Ila je Mungu alitolewaka wapi ?

Ellen Kagosi
Ellen Kagosi
2 years ago

I really appreciate you in helping these successful questions is such of evengalism you are doing may God bless you alot