Kwanini, tuimbe, je! kuna ulazima wowote wa kufanya hivyo?

Kwanini, tuimbe, je! kuna ulazima wowote wa kufanya hivyo?

SWALI: Bwana Yesu asifiwe wingu la mashahidi. Nmekutana na swali naomba upana wa somo hili. Kwa nini tunaimba na kuna sura nyingi zinasisitiza kuimba mfano Luka 19 :37-38 na vitabu vya zaburi na ufunuo. Na tofauti ya kuimba na kuongea au kusema mf ufunuo 5:12-14 n.k. naomba ufunuo juu ya mambo hayo. Amen.


JIBU: Shalom ndugu yangu..   Hatuimbi kwasababu tumeagizwa, lakini tunaimba kwasababu ni kitu tulichoumbiwa ndani yetu.. Ni kama vile kucheka, kukasirika, kuona huruma, hivi vitu haviji kwasababu tumeagizwa na Mungu, au tunapoambiwa tuvifanye. hapana bali ni vitu vinavyotoka vyenyewe ndani, ndivyo ilivyo katika kuimba kila mwanadamu haijalishi ni mwema au mwovu, atapenda tu kuimba, asipopenda kumwimbia Mungu basi atapenda kumwimbia shetani.…. Na hili ni lango la haraka sana linalomchukua mtu rohoni naweza kusema zaidi ya malango mengine, kama vile kufunga, …kuimba ni lango linalomwingiza katika roho haraka sana.  

Na ndio maana Mungu anapotuagiza tumsifu, anasisitiza tumsifu kwa nyimbo, kumbuka sifa za Mungu kiuhalisia sio nyimbo, sifa ni kitu kinachokuja kutoka ndani ya moyo na hiyo ni aidha baada ya kuuona uweza na ukuu wa Mungu, au kuona wema wake kwako..hapo ndipo sifa zinapokuja, na hizo zinaweza kudhihirishwa nje kwa njia mbali mbali aidha kwa kuzungumza au kwa vitendo mfano kuruka ruka mbele zake, kusujudu, au kuimba, ambapo kunajumuisha kuabudu.  

Lakini kwanini Mungu anasisitiza tumsifu kwa nyimbo, ni kwasababu kuimba kunaleta bubujiko la haraka zaidi kuliko kuzungumza kwasababu kuimba kunahusisha na hisia za mtu za ndani kabisa..Wanaomwimbia shetani, wakiimba nyimbo zao huwa wanakuwa kama vichaa, ni kwasababu wanamwimbia katika roho, Na ndio maana Mungu anasisitiza tumsifu yeye kwa aina mbalimbali za vinanda na ustadi wa kila namna umpendezao..kwa kadri ya wingi wa ukuu wake.  

Zab 150: 1 Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake. 2 Msifuni kwa matendo yake makuu; Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake. 3 Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi; 4 Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi; 5 Msifuni kwa matoazi yaliayo; Msifuni kwa matoazi yavumayo sana. 6 Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana. Haleluya.  

Ubarikiwe.

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments