Je! baada ya ulimwengu huu kuisha malaika watakuwa na kazi gani tena?

Je! baada ya ulimwengu huu kuisha malaika watakuwa na kazi gani tena?

SWALI: Moja ya kazi ya Malaika ni kumlinda Binadamu na Mapepo, Sasa baada ya hukumu kazi ya malaika itakuwa ipi kama shetani atakuwa kashatupwa na mwanadamu kainuliwa kiwango cha juu sana?. ( Inamaana Malaika watapotezwa au wataachishwa kazi zao?).


JIBU: Kama ulivyosema “MOJA” ya kazi ya malaika ni kutulinda sisi…kumbe hiyo ni mojawapo ya kazi zao, ikiwa na maana kuwa pia zipo kazi nyingine nyingi wanazozifanya…Ikumbukwe kuwa Malaika ni sehemu ya familia ya Mungu na Mungu aliwaumba wale miaka mingi kabla yetu sisi, Mungu hakungoja kutuumba sisi kwanza kisha awaumbe wao ili wapate kazi ya kufanya hapana..  

Mbinguni kuna shughuli nyingi sana zinazoendelea biblia haujatueleza kwa urefu mambo ya mbinguni yahusianayo na kazi za malaika kwa Mungu, tunachojua tu ni kwamba kuna wakati Bwana Yesu alitaka kutufunulia walau kwa sehemu mambo yanayoendelea mbinguni lakini aliacha hakutuambia na hiyo yote ilikuwa ni sababu ya kutokuamini kwetu.. Tunalithibitisha hilo katika  

Yohana 3:12 “Ikiwa nimewaambia mambo ya duniani, wala hamsadiki, mtasadiki wapi niwaambiapo mambo ya mbinguni?”  

Hivyo fahamu tu malaika wanazo kazi nyingine nyingi mbele za Mungu tusizozijua sisi…Tukifika huko tutazifahamu..Sisi tumeishia tu kwenye hizo mbili zilizoandikwa kwenye biblia moja kwa moja yaani ile ya kutuhudumia sisi wanadamu (Waebrania 1:14), na nyingine ni kumsifu Mungu(Luka 2:13-14, Ufunuo 4:8), zaidi ya hapo hatujui…(Ikiwa utependa kujifunza kuwa upana somo lihusulo huduma ya malaika watakatifu kwetu sisi wanadamu, tutumie ujumbe inbox tutakutumia somo lake..)   Tunachopaswa kufanya sasa ni kuwa waaminifu na kutii kwanza haya tuliyopewa kuyaamini yahusuyo wokovu wetu, ili tukishashinda sasa, siku ile tutakapofika mbinguni tufunuliwe zaidi..   Na ndio maana mtume Paulo alisema:  

1Wakoritho 13:12 “Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana.”  

Hivyo malaika hawatatoweshwa, na wala hawatakosa kazi ya kufanya kwani hadi sasa zipo shughuli wanazozifanya ambazo hazina uhusiano wowote na sisi wanadamu.  

Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:

HUDUMU YA MALAIKA WATAKATIFU.

KUNDI LA MALAIKA WALETAO MABAYA.

JE NI HALALI KUOA WAKE WENGI, AU KUTOA TALAKA?

TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI:

JIWE LA KUKWAZA.

NI WAKATI GANI SHETANI ANAPENDA KUMSHAMBULIA MWAMINI?


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments