Ni rahisi zaidi ngamia kupenya tundu ya sindano.

Ni rahisi zaidi ngamia kupenya tundu ya sindano.

SWALI: Hapo Bwana wa mabwana anamaanisha nini kusema ‘ Ni rahisi zaidi ngamia kupenya tundu ya sindano ’..Je! ni sindano ipi hiyo inayozungumziwa? Maana kisasa tuna sindano za kushona nguo,sindano za kushonea mwili wa binadamu,sindano yakushonea viatu,sindano yakumchoma mtu (za madawa) Ni sindano ya Aina gani ameizungumzia hapo kwenye Mathayo19:23).


JIBU: Kama tunavyoifahamu habari hiyo ni kuwa mtu tajiri alimfuata Bwana Yesu, na kumuuliza atende jambo gani jema ili aurithi uzima wa milele, Ndipo Bwana akamwambia Umezishika Amri? Yule kijana akasema hizo nimezishika tangu utoto wangu ,nimepungukiwa na nini tena?. Bwana akampenda sana lakini akamwambia ukitaka kuwa mkamilifu nenda kauze vyote ulivyonavyo kisha unifuate, lakini Yule kijana aliposikia vile aliondoka kwa huzuni kwasababu alikuwa na mali nyingi..Ndipo Bwana akawaambia wanafunzi wake maneno haya.

Mathayo 19:23 “Yesu akawaambia wanafunzi wake, Amin, nawaambieni, ya kwamba itakuwa shida tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni.

24 Nawaambia tena, Ni rahisi zaidi ngamia kupenya tundu ya sindano, kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.” 

Sasa tundu linalozungumziwa hapo, inaaminiwa na baadhi ya watafiti wa mambo ya kale kuwa ni mlango mdogo ambao ulijengwa katika kuta za Yerusalemu uliokuwa unafunguliwa wakati wa usiku muda ambao geti kubwa la mji limefungwa kwa usalama wa mji na ulinzi..…Mlango huo ulijulikana Kwa jina hilo TUNDU LA SINDANO.

Ulikuwa ni mdogo kiasi cha mtu na wanyama wadogo tu kupita, lakini kwa wanyama wakubwa kama ngamia haikuwa rahisi na kama ikitokea anapaswa apite basi ni lazima ngamia atolewe mizigo yake yote , na apitishwe kwa kupigishwa magoti kwa shida sana, haikuwa rahisi hata kidogo….

Lakini nadharia hiyo haina uthibitisho wa moja kwa moja kuwa kulishawahi kuwa na mlango kama huo Yerusalemu. Uwezekano mwingine ni kuwa Watafsiri na wachambuzi wa maandiko wamegundua kuwa Neno ngamia kwa lugha ya KIARAMU linakaribiana sana kufanana na neno UZI, Hivyo wanasema watafsiri wa kwanza wa vitabu vya Agano jipya, walipokuwa wanatafsiri baadhi ya maneno kutoka katika Lugha ya kiaramu kwenda kwenye lugha kiyunani, walilitafsiri tofuati neno hilo wakidhani ilimaanisha pale ngamia kumbe ni UZI mpana, na kwamba ingepaswa isomeke hivi… Nawaambia tena, Ni rahisi zaidi Uzi mpana kupenya tundu la sindano, kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.” Na hivyo sindano inayozungumziwa pale ni Sindano kama sindano halisi kabisa ile ya Kushonea.. 

Lakini kwa vyovyote vile, tunapaswa kufahamu kiini cha ujumbe ambacho tunakipata katika habari ile…Pale tunaona Bwana alikuwa anajaribu kutueleza ugumu uliopo kwa watu wenye kutegemea mali kuingia katika ufalme wa mbinguni ndipo akatumia mfano ule ili kutilia msisitizo zaidi…

 Ni sawa tu na pale aliposema “toa boriti iliyo katika jicho lako, ndipo uone vema kutoa kibanzi kilicho katika jicho la ndugu yako…Lakini kiuhalisia kibanzi au boriti haviwezi kukaa katika macho ya mtu…Lakini ili kufikisha ujumbe kwa uzito zaidi ilimpasa Bwana atoe mifano ya namna hiyo, ambayo kiuhalisia haiingia akilini, kama mahali pengine aliposema, mnachuja mbu, na kumeza ngamia… 

Na ndivyo ilivyo katika habari hii..hatushangai pia akimaanisha kama ilivyoandikwa pale ngamia kupenya katika sindano ya kushonea.

 Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:


NJIA YA ‘UTAJIRI MKUU’ KWA KIJANA.

MADHARA YA KUKOSA MAJI YA UZIMA BAADA YA KIFO.

NEHUSHTANI (NYOKA WA SHABA).

BWANA YESU ANAMAANISHA NINI KUSEMA “WALA MSIMWITE MTU BABA DUNIANI”?

TAFUTA KUMJUA MUNGU ZAIDI YA SHETANI

MAFUMBO YA MUNGU.

UNYAKUO.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Jackson Julius
Jackson Julius
1 year ago

Ubarikiwe sana mpendwa, naomba uniunge whatsap ili niwe napata masomo zaidi 0747465324