Je! kuna ubaya wowote kuwaombea ndugu zetu waliokufa katika dhambi, Mungu awakumbuke katika ufalme wa mbinguni?.

Je! kuna ubaya wowote kuwaombea ndugu zetu waliokufa katika dhambi, Mungu awakumbuke katika ufalme wa mbinguni?.

SWALI: Bwana wetu YESU ametuahidi tumuombe jambo lolote lile KWA JINA LAKE YESU naye atalifanya..Mahali pengine anatuambia maombi yetu Watakatifu ni harufu nzuri ya manukato mbele zake..(Sasa mfano mimi nanyi tunaye rafiki yetu mpendwa amefariki na kila siku tulikuwa tukimuomba Mungu amkumbuke kwenye ufalme wake wa mbinguni,unajua hili lipo ndani ya karibu binadamu wote kwamba mtu wako wa karibu akifa KITU FULANI kinakuwa kinaning’inia moyoni mwako KUMTAKIA HATIMA NZURI YA MAISHA YAKE MBELE ZA MUNGU..hivyo ukimtakia mpendwa wako wa karibu aliyefariki kwa KUMUOMBEA mbele za Mungu (aliyetuambia maombi yetu Watakatifu ni harufu nzuri ya manukato mbele zake hivyo tumuombe tu lolote kwa JINA LA YESU) AMUOKOE NA KUZIMU. Je! kuna ubaya gani hapo? ukimuombea mtu aliyefariki kila siku mbele za Mwenyezi Mungu amkumbuke kwenye ufalme wake wa mbinguni KWA JINA LA YESU?.


JIBU: NI kweli tunajua Mungu anaweza mambo yote, lakini sifa yake nyingine ni kuwa hafanyi mambo yote. Alivyotuumba sisi wanadamu hakutuumba kama Ma-robot kwamba lisipoongozwa na mwanadamu haliwezi kufanya jambo lolote lenyewe….Pale aliposema katuumba kwa mfano wake, alimaanisha kweli kweli kusema vile!!, ikiwa na maana kuwa kwa sehemu Fulani mtu anaweza akajiamulia mambo yake mwenyewe binafsi bila hata ya kuingiliwa na mtu yeyote kana kwamba kajiumba mwenyewe kama Mungu.. Na jambo kubwa ambalo Mungu kamuumbia mwanadamu ni uhuru wa MAAMUZI, ambayo hata yeye mwenyewe muumbaji, mwenye sifa ya kutoshindwa kufanya jambo lolote anayaheshimu, kiasi cha kutoyaingilia, au kuyaathiri MAAMUZI YA MTU ikiwa tu mtu anaridhika kuwa nayo.  

Mfano leo hii mtu akiamua kuwa mchawi kwa matakwa yake mwenyewe, Mungu haji kumwambia ni Nani amekupa ruhusa ya kuwa hivyo?, atakachofanya ni kumshawishi atoke huko, ataugua moyoni mwake kila kukicha ili aiache dhambi hiyo atampelekea mpaka watumishi wake kila kukicha kumuhubiria madhara ya kuwa mchawi, kwamba mwisho wa siku watu wa namna hiyo wataishia katika ziwa la moto..Hivyo mtu Yule akikubali kuitii ile sauti na kugeuka, Mungu ndio anatembea naye na kumwongoza katika njia sahihi zaidi, lakini kama hatakubali Mungu haji kumlazimisha kwa nguvu aache, hiyo haijawahi kuwa kanuni yake tangu mwanzo kwa viumbe vyake vyote..Hata shetani na mapepo yote hakuyafanyia hivyo.  

Hivyo maombi yetu hayawezi kuvuka maamuzi ya mtu binafsi, Kama tu vile uweza wa Mungu usivyoweza wa kugeuza maamuzi ya mtu binafsi, kwasababu Kumbuka biblia inasema pia si mapenzi ya Mungu watu wapotee, bali wote waifikie toba,(2Petro 3:9) lakini leo hii kwanini tunaona watu wanapotea, japo anao Uwezo wa kuwafanya wasipotee?..Ni kwasababu kuna mipaka kajiwekea hawezi kuivuka..

Kadhalika mtu aliyepo kwenye dhambi maombi yetu tunayomwombea sio kwamba yanakwenda moja kwa moja kutangua maamuzi yake ya kuacha dhambi hapana! Bali yanafanya kazi ya kuongeza ushawishi wa Roho Mtakatifu ndani ya mtu, na ushawishi unavyozidi kuwa mwingi..mtu yule ndipo anaamua kugeuka kwa hiyari yake na hivyo tunasema tumempata. Leo hii kama mtu kaamua kuwa mtumishi wa shetani kwa akili zake mwenyewe, anasema hamtaki Mungu, sisi tukimwombea Mungu atakachofanya ni kumshawishi ndani ya moyo wake..

Lakini zaidi ya hapo hafanyi..hivyo hata tumwombeeje, kama anazidi kuukataa ule ushawishi ndani yake hapo haiwezekani kumgeuza.   Sasa mpaka mtu amefikia hatua ya kufa, na ameenda kuzimu, ni wazi kuwa tangu akiwa hai aliichagua mwenyewe njia ya upotevuni, na sasa maisha yake yamekwisha akiwa katika hali hiyo, amefikia wakati wa mavuno wa kuvuna alichokipanda..Haiwezekani tena sio tu kumwombea, hata yeye mwenyewe kuweka nia ya kutoka huko, kama tu vile waliokufa katika haki haiwezekani tena wao kutoka kule peponi na kushuka kuzimu.  

Hivyo ni vizuri kuutumia wetu vizuri tukiwa hapa duniani, Kwani kuna baadhi ya Imani ikiwemo Imani ya kanisa Katoliki zinaamini kuwa watu waovu wanapitia TOHARANI, , ili kusafishwa kabla ya kwenda mbinguni, kwa maelezo marefu juu ya somo hilo nitumie ujumbe inbox nikutumie habari yake.. Lakini huo ni opotofu mkubwa wa shetani, kuwafanya watu wastarehe katika dhambi zao wakidhani kuwa ipo nafasi ya pili..Biblia inasema: Waebrania 9:27 “Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;” Hakuna tumaini lolote, kwa aliye kufa ikiwa, amekuta katika dhambi.  

Ubarikiwe sana.


Mada Nyinginezo:

NI SAHIHI KWA MKRISTO MTAKATIFU KUMWAMBIA BWANA AILAZE ROHO YA MTU ALIYEKUFA MAHALI PEMA PEPONI?

NAOMBA UFAFANUZI WA HUU MSTARI; 1WAKORITHO 15:29 “AU JE! WENYE KUBATIZWA KWA AJILI YA WAFU WATAFANYAJE? KAMA WAFU HAWAFUFULIWI KAMWE, KWANINI KUBATIZWA KWA AJILI YAO? “.

BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA “WAACHE WAFU WAZIKE WAFU WAO.(MATHAYO 8:21)?

MAOMBI KWA WENYE MAMLAKA.

AMEFANYIKA BORA KUPITA MALAIKA!


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments