Ndugu yangu kama wewe ni muislamu unasoma ujumbe huu, au mkristo ambaye bado hujayajua vizuri mamlaka Bwana Yesu aliyopewa na vigezo vya kuwa mrithi pamoja naye, na unasema moyoni ninasaidia masikini, ninawaheshimu wazazi, sidhulumu, sifanyi hichi sifanyi kile, ukijidanganya kuwa kwa mambo hayo tu upo karibu na Mungu na huku umemweka Kristo nyuma
Hujazaliwa mara pili katika damu yake, napenda nikuambie ndugu yangu UNAPOTEZA MUDA!!!! Matendo yako ni mazuri lakini hayatakusaidia huko mbeleni. Huko mbeleni ni UNDUGU ndio utakaojalisha kwanza na kisha ndio matendo yafuate!..Ni sawa na kwenda kumfanyia boss wako mema yote unayoyajua duniani na kumpendeza kwa viwango vyote ukitumai kuwa siku moja atakurithisha kampuni lake!!…hilo katika akili yako lifute, kwasababu hawezi kuacha kumrithisha mtoto wake (damu yake) akurithishe wewe?..hata kama mwanawe hana tabia nzuri kama za kwako, hata kama wewe ni mchapa kazi kuliko yeye, siku moja huyo mtoto atakuja kuwa boss wako tu…kwanini?? Kwasababu ya uhusiano wa kidamu uliopo kati ya yule mtoto na baba yake!!.