KUOTA UNAJIFUNGUA.

KUOTA UNAJIFUNGUA.

Kuota unajifungua kuna maanisha nini?


Ndoto hii inaweza ikawa na maana mbili, maana ya kwanza ambayo ninaweza  kusema inawapata wengi, ni ile inayotokana na shughuli nyingi au mambo tuliyowahi kuyapitia, au kuyawaza, au kuyatenda mara kwa mara huko nyuma.

Biblia inasema.

Mhubiri 5:3 “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi;…….”.

Hivyo sishangai kama ndoto hii atakuwa anaotwa na mwanamke, kwasababu yeye kwa sehemu kubwa katika maisha yake, amekuwa akiwaza pengine siku moja atajifungua, au hivi karibuni anakwenda kujifungua au mwengine tayari huko nyuma alishawahi kujifungua,..

Hivyo matukio kama hayo kujirudia rudia katika ndoto zake litakuwa ni jambo la kawaida sana. Kwahiyo kama wewe ni mmojawapo wa wanaoyapitia hayo, basi ipuuzie tu ndoto ya namna hiyo, kwasababu haina maana yoyote rohoni.

Lakini maana ya pili, ambayo ni ya rohoni, ni kwamba ikiwa ndoto hii umekujia kwa namna ambayo sio ya kawaida, yaani kwa uzito mkubwa sana, na unahisi kuna uzito Fulani ndani ya moyo wako, basi ujue ndoto hiyo imebeba ujumbe. Na tafsiri yake ni kuwa lipo jambo zuri au baya linakwenda kukujia, kulingana na ulichokuwa unakifanya katika maisha yako.

Tunajua sikuzote mpaka mtu anafikia hatua ya kuzaa ni wazi kuwa tayari huko nyuma alishabeba mimba kwa muda mrefu, hivyo angalia katika maisha yako ni nini umekuwa ukikibeba, na ukikisubiria, basi ujue hivi karibuni utakwenda kukiona kikijidhihirisha (kukuletea matokeo fulani). Kama umekuwa ukifanya jambo jema basi tazamia kuona matunda ya wema wako hivi karibuni.

Luka 1:30 “Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.

31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.

Lakini kama wewe ni mwenye dhambi (yaani haupo ndani ya Kristo) basi jiandae hivi karibuni kukutana na matunda ya mambo maovu uliyokuwa unayafanya katika maisha yako,

biblia inasema..

Ayubu 15:35 “Wao hutunga mimba ya madhara, na kuzaa uovu, Nalo tumbo lao hutengeza udanganyifu”.

Zaburi 8:14 “Tazama, huyu ana utungu wa uovu, Amechukua mimba ya madhara, amezaa uongo”

Yakobo 114 “Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.

15 Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti”.

Unaona wanachozaa sikuzote watu waovu ? Na ndio maana sehemu nyingine inasema..

Mathayo 3:10 “Na shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni”.

Hivyo jiangalie wewe katika maisha yako yote, na mambo yako yote unayoyatenda Je, ni jambo gani unakwenda kulizaa hivi karibuni? Je! ni uzima, au mauti?

Lakini habari njema ni kuwa Yesu leo anaweza kukuokoa, na kukufanya umzalie matunda mazuri, na akabatilisha mabaya yote ambayo yamepangwa mbele yako, ikiwa tu utakubali kumruhusu ayageuze maisha yako, Yeye yupo tayari kukusamehe ikiwa utakuwa tayari kutubu kwa moyo wako wote, Hivyo ikiwa upo tayari kufanya hivyo leo, basi uamuzi huo ni wa busara sana. Unachotakiwa kufanya ni kufungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba.>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Na Mungu peke yake atakigeuza unachokizaa kiwe chema.

Bwana akubariki sana.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Au jiunge kwa kubofya link hii>> 

Group la whatsapp Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi

Mada Nyinginezo:

HERODE NA PILATO, MAADUI WAWILI WAPATANA.

Mwaloni ni nini? Na je unafunua nini rohoni?

Arabuni maana yake ni nini?

MOTO HUFA KWA KUKOSA KUNI.HATA UASHERATI NAO

UNYAKUO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments