Mwaloni ni nini? Na je unafunua nini rohoni?

Mwaloni ni nini? Na je unafunua nini rohoni?

Kwa lugha ya kiingereza unajulikana kama OAK tree, Kisayansi Kuna ziadi ya jamii 600 za mti huu.. Na unapatikana sehemu mbalimbali duniani sana sana zile za baridi, lakini katika ukanda wa mediterenia yaani Maeneo yote ya mashariki ya kati ikiwemo Israeli mti huu unaota kwa asili.

Mti wa mwaloni unatoa mbao zinazosifika kwa ugumu, katika ujenzi, na matumizi mbalimbali ikiwemo kutengenezea mapipa ya kuhifadhia divai, na mbao za mashua..Vile vile Mti huu unaweza kuishi miaka hata zaidi ya elfu moja..

Lakini Mti  wa mwaloni unaonekana pia ukitajwa sehemu nyingi katika biblia na baadhi ya vifungu hivyo ni kama vifuatavyo..

Mwanzo 35: 8 Akafa Debora mlezi wa Rebeka, akazikwa chini ya Betheli, chini ya mwaloni; na jina lake likaitwa Alon-bakuthi.

 

Yoshua 2: 25 Basi Yoshua akafanya agano na wale watu siku ile, akawapa amri na agizo huko Shekemu.

 

26 Yoshua akayaandika maneno haya katika kitabu cha torati ya Mungu; kisha akatwaa jiwe kubwa, akalisimamisha huko, chini ya ule mwaloni uliokuwa karibu na patakatifu pa Bwana.

 

Waamuzi 6:11 Malaika wa Bwana akaenda akaketi chini ya mwaloni uliokuwa katika Ofra, uliokuwa mali yake Yoashi, Mwabiezeri; na mwanawe Gideoni alikuwa akipepeta ngano ndani ya shinikizo, ili kuificha machoni pa Wamidiani.

 

2Samweli 18: 9 Na kwa bahati Absalomu akakutana na watumishi wa Daudi. Naye Absalomu alikuwa amepanda nyumbu wake, na yule nyumbu akapita chini ya matawi manene ya mwaloni mkubwa, hata kichwa chake kikakwama katika mwaloni huo, akanyakuliwa juu kati ya mbingu na nchi; na yule nyumbu aliyekuwa chini yake akaenda mbele.

Nakadhalika, na kadhalika…

Lakini Swali ni, Je mti wa mwaloni unayo maana yoyote rohoni?

Mti yote tunayoiona ikitajwa kwenye maandiko, ilikuwa na  kwa kazi maalumu katika jamii, vilevile ikifunua jambo Fulani katika roho kwa mfano ukisoma

Waamuzi 9;8-15.. utaona mwandishi akieleza jamii ya miti akifananisha na jamii za watu waliopo..

  • Kwamfano ukisoma pale mti kama Mzeutuni anasema ulikuwa unatumika kwa ajili ya kutolea mafuta, jambo lililofunua katika agano jipya, watiwa mafuta, au watumishi wa Bwana.(Soma Zekaria 4;11-14, Ufunuo 11)
  • Vilevile Mzabibu ulikuwa unatoa divai,.Ukimfunua Yesu Kristo na Roho Mtakatifu, Na sisi pia kama matawi ya ya mzabibu huo tunapaswa kutoa matunda ya Roho ndani yetu pale Kristo anapokaa ndani yetu (Yohana 15)
  • Pia Mtini, ni mti unaotoa tini, ikifunua taifa la Israeli kwa ujumla(Yeremia 24)
  • Miiba, au michongoma..Ni miti iliyofunua watawala wabovu au watumishi waovu mfano Abimeleki Yule mtoto wa Gideoni…

Sasa tukirudi kwenye maandiko kile kitabu cha Isaya 6:1-4  kinasema..

1 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.

2 Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao;

3 kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji ya maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; WAPATE KUITWA MITI YA HAKI, iliyopandwa na Bwana, ili atukuzwe.

4 Nao watajenga mahali pa kale palipoharibiwa, watapainua mahali palipokuwa ukiwa zamani, watatengeneza miji iliyoharibiwa, mahali palipoachwa kizazi baada ya kizazi.

Ukisoma tafsiri nyingine nyingi za biblia, pale kwenye neno ‘miti ya haki’, limetumiwa neno mialoni ya haki..

Sasa kama tulivyokwisha kuona kule mwanzo mwaloni ni mti uliotumika hasahasa katika ujenzi, ni mti uliosifika kuwa na mbao ngumu, na zenye uwezo wa kuitunza divai vizuri.

Hivyo rohoni, ukiwa wewe ni mjenzi wa nyumba ya Mungu (Kanisa lake) unafananishwa na Mwaloni. Kama wewe ni mhubiri kwa Bwana ni mwaloni wake, kama wewe ni shujaa wa Bwana katika kuifanya kazi yake basi ni mwaloni kwa Bwana…Kama wewe unaifanya kazi kama ya Kristo ya kuhubiri injili basi ni mwaloni mzuri ufaaye kwa kazi ya ujezi wa nyumba ya Mungu inayodumu.. sawasawa na Isaya 61:4.

Ubarikiwe.

Mada Nyinginezo:

Pakanga ni nini?

Je! habari ya Yusufu, inabeba ujumbe gani kwa agano jipya?

JE! Kaini alimpatia mke wake wapi?

NINI KINATOKEA BAADA YA KIFO?

NINI MAANA YA KUSAGA MENO?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments