NINI MAANA YA KUSAGA MENO?
Kusaga meno ni kitendo cha kung’ata meno kwa nguvu kutokana na maumivu fulani au uchungu fulani. Kwamfano mtu aliyejikata na kisu au kujikwaa kwenye kidole utaona atang’ata meno kwa nguvu kutokana na maumuvi anayoyasikia au uchungu au hasira fulani (Soma Matendo 7:54).
Na hata wakati mwingine mpaka kung’ata huku yanasuguana. Sasa kitendo hicho ndicho kinachoitwa kusaga meno.
Katika biblia kuna sehemu kadha wa kadha zimezungumzia tendo hilo. Kwamfano utaona Bwana Yesu alipozungumzia juu ya mateso yaliyopo Jehanum hakuacha kuhusisha tendo la usagaji wa meno. Ikifunua kuwa Jehanamu sio mahali pa raha. Bali pa mateso makali sana.
Mathayo 13:41 “Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi, 42 na kuwatupa katika tanuru ya moto, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno”.
Mathayo 13:41 “Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi,
42 na kuwatupa katika tanuru ya moto, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno”.
Mathayo 25:30 “Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno”.
Mistari mingine inayofanana na hiyo, inayozungumzia kitendo cha kusaga meno ni pamoja na Zaburi 37:12, Mathayo 8:12, Mathayo 13:50. Mathayo 22:13, 25:30, Marko 9:18 na Luka 13:28.
Hiyo yote inalenga kutuonyesha ukali wa mateso yaliyopo Jehanum. Kwamba si sehemu nzuri, kutakuwa na maumivu makali na mateso kwa wale wote ambao hawajampokea Kristo na waliorudi nyuma.
Kama hujampa Yesu Kristo maisha yako, ni vyema ukafanya hivyo kabla muda wako wa kuishi duniani haujaisha. Unachopaswa kufanya ni kutubu tu mahali ulipo. Unatubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kisha unatafuta ubatizo sahihi wa maji tele na kwa jina la YESU KRISTO kulingana na Matendo 2:38. Kwa ajili ya kukamilisha wokovu wako.
Na kama ulishabatizwa katika vigezo hivyo hapo juu basi hauhitaji kubatizwa tena. Na mwisho kabisa Bwana mwenyewe atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu atakayekusaidia kushinda dhambi.
Bwana akubariki.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
USIZITEGEMEE NGUVU ZAKO KUKUSAIDIA!
KWA KUWA NGUVU ZA MBINGUNI ZITATIKISIKA.
JE ! BWANA YESU ALIKUJA DUNIANI KUAMUA NINI?
Kwanini Bwana Yesu alisema pale msalabani naona kiu?
Rudi Nyumbani:
Print this post